Kama hataki kuulizwa kuhusu mshahara wake na achape lapa.
Jamani kuna malalamiko miongoni mwa wanaume waliooa wanawake wafanyakazi kuhusu mchango wa mishahara yao ktk matumizi ya familia. Nina marafiki wangu kadhaa (waliooa wake wafanyakazi) wote wanadai eti ukitaka kuishi kwa amani na mkeo usimuulize kuhusu mshahara wake. Nilishangaa sana kusikia hivi kwani mara nyingi huwa nasikia vijana wengi wanataka kuoa wasichana wenye kazi ili waweze kusaidia ktk kupunguza ukali wa maisha. Naombeni uzoefu wenu ktk hili jamani. Natanguliza samahani kama topic ilishaongelewa huko nyuma, ila ningetamani kuona hizo sred ili nisome maoni ya wadau!
Anadamka asubuhi kwenda kibaruani, anachelewa kurudi kibaruani sababu ya foleni afu nisiujue mshahara wake na unatumikaje?....... I better marry my mom!
Othetwise akae nyumbani anilelee wanangu.... PERIOD!
ni vitu muhimu sana kuvijadili kipindi cha uchumba. lazima muelewane how to save our salary, kiasi gani tule. panga mipango yenu kwa pamoja ya siku, ya mwezi , ya miezi mitatu, ya nusu mwaka, ya mwaka, ya miaka mitatu nk hayo yote yatajiseth. lazima awepo accountant nk ndo maana kuna aina nyingi za account.
kama ataki kushare salary, basi na wewe wako usitumia kila mtu ale mshaala wake
...................JINO..... kwa..........JINO bana......., ndiyo maisha ya Dot.COM
Mkuu sioni kwanini niulize mshahara wa wife unakwendaje..., lakini tashangaa kama kila siku naulizwa chumvi na vitu vidogo vidogo.., siwezi kumpangia matumizi lakini yeye mwenyewe kwa busara nina uhakika kuna mengi atafanya na pindi nikiwa juu ya mawe sidhani kama ataniangalia tu..
Cha maana put your cards on the table.., kwamba this is what we have..., here is where we need to go.., and here is where we are..., kwahio kufika huko tunakotaka and the way we are spending something needs to be done. Kwahio mnapanga jinsi ya kutumia na ku-invest na sio kumuuliza pesa yako ipo wapi utafikiri wewe ndio benki ya kumuwekea (mshirikishe kwenye miradi yenu na mshauriane)
Inategemea busara zako , kwa maana ukianza maisha na busara ya matumizi ya pesa, mkeo pia atakuwa na busara katika pesa na kushiriki moja kwa moja katika kuchangia maendeleo ya familia. hii inamaanisha kama matumizi ya pesa zako yatoonekana yanaleta maendeleo, mkeo atafuta nyayo. msiogope kuoa wafanyakazi.
Inategemea busara zako , kwa maana ukianza maisha na busara ya matumizi ya pesa, mkeo pia atakuwa na busara katika pesa na kushiriki moja kwa moja katika kuchangia maendeleo ya familia. hii inamaanisha kama matumizi ya pesa zako yatoonekana yanaleta maendeleo, mkeo atafuta nyayo. msiogope kuoa wafanyakazi.
mshahara wa mwanamke ni kuishia saluuni babu,hujui sie wanawake ni mapambo ya nyumba lazima tupendeze muda wote?lol....
ukiwa una date na mtu jaribu kuwa muwazi kwa mkeo mtarajiwa,mipango yako ya baadae na kumshirikisha pia. ....eg umeona kiwanja na unataka kununua,unaweza ukamshirikisha kwa kumwambia akuongezee kiasi fulani cha pesa...sio lazima iwe nusu kwa nusu.................,na hata mkitoka sio ujionyeshe wwe ndio kidume kwa kulipia kila kitu...unaweza kumwambia unalipia chakula yeye alipie drinks....ukijenga tabia hii tangu mwanzo...utamfanya achukue rensponsibilities na yeye,awajibike hata kwa mambo yanayofuata ktk ndoa yenu....wengi wanakosea tangia mwanzo anamjenga mpenzi wake kuwa tegemezi kila kitu hadi vocha baadaye inakuwa ngumu kubadilisha system........
na pia mkeo ni rafiki yako,tangu mwanzo kuwa na tabia ya kuwasiliana naye jambo unalopenda na usilopenda....hii itakurahisishia baadae kumface na kumwambia jambo lolote kama unaona anaenda sivyo.usiwe mtu wa kunyamaza kimya au kujifanyia mambo mwenyewe itakucost siku moja.
.... mkeo ana HEKIMA..... nawewe una HEKIMA........ halafu..... UMEMZIDI KIPATO.......!!!!simuuliz mke wangu mshahara coz she is
da best house keeper and budgeter ever!
Hajawahi lalama nimempa pesa ndogo so it means mayb anaongeza na zake samtimes.