Mishahara ya walimu

Baba Hellen

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2012
Posts
763
Reaction score
91
sijui ninini? kwani wilaya ya ngorongoro mishahara imeingia nusu na wengi wao hawajapata ingawa tayari wapo kwenye pay roll. wengi wanasema kwasababu imetoka hazina direct hebu wenye uelewa zaid watujuze
 
Hata hapa Tarime kuna walimu hawajapata. Kwa taarifa zilizopo ni kwamba pesa ililipwa moja kwa moja toka hazina, payroll haikuja hapa Tarime. Sijui tatizo la walio kosa ni nini!
 
Wavute subila mambo yatakuwa poa soon, poleni walimu wangu!!!
 
wamezpeleka kweny bajeti ya mapokez ya rais na kinana
 
Kongwa mkoani dodoma waalimu 800 hawajapata kitu hadi sasa,kweli haya nayo ni maajabu ya nchi hii
 
Vumilieni jamani, najua sisi walimu ni wavumilivu, tunafanya uhakiki kama kweli mpo makazini mana hili li mshahar likubwa tulilowaongeza isije tunalipa watu hewa.

Makofi kidogo kwa serikali sikivu.
 
Dah huku kasulu na buhigwe napo hali ni hvyo hivyo walimu kibao hatuja pata hiyo salary sijui ni nini tatizo
 
Hata wilaya ya Mbeya vijijini tupo wengi hatujapata yaani sijui tatizo ni nini
 
Hata wilaya ya Mbeya vijijini tupo wengi hatujapata yaani sijui tatizo ni nini

Japo Mimi sio mwalimu ila napenda fani hii kwa sababu kuu moja: Walimu wanapendana.

Huku kwa wenzangu wauguzi hhali ni ngumu lakini kwasababu ya ubinafsi na kubaguana kila MTU yupo kimya kama vile hakuna tatizo.

Watu Wa afya MNA laana ya kubaguana nyieee"
 
Wapendwa mimi nadhani hawa watu wa hazina wana malengo safi tu kwa kuamua kuwawekea watu mishahara moja kwa moja kwani watakuwa wamefanya uhakiki wa kutosha kuhusu mishahara hewa na wale wanaolipwa mara mbili mbili, lkn tatizo lao hawajajipanga kwa hilo, kwani watumishi ni wengi mno kuwawekea mishahara lwa timu ndogo kama ya hazina, ninaeongea hapa nami si mwalimu wala si nesi, lkn ninamajanga.

Tuvumilieni hata kama Idd itakiwa dolo hatuna jinsi, twende tukope kwa waliopata ili mambo yafanane siku ya sikukuu wapendwa.
 
hii serikali kila kukicha inatufanya tuichukie huku mbozi waalimu wapya karibia wote hawajapata salary ya mwezi huu huku ya mwezi wa 4 hadi leo na yenyewe kama utani vile.

Dah! Inauma sana
 
Ni kweli watumishi wengi ambao hawajapata mishahara na juzi nimeulizia maafisa wetu wakadai payrall bado, lakini mchana wengine wakaanza kuchukua zao huku wakisema hakuna ongezeko la mishahara kama jinsi serikali ilivyotuzuga zaidi ya increment ya kila mwaka
 
Hili tatizo ni nchi nzima, hapa matumaini yetu ni wiki hii maana mishahara iliingia ijumaa jioni. Labda zoezi litaendelea baada ya wikend kuisha.
 
imetokea kwenye halmashauri nyingi jipeni moyo mambo yatakuwa vizuri soon.
 
walimu tusipifanya maamuzi magumu kuitoa ccm kwenye madaraka basi mishahara yetu haitapanda na maisha yetu yataendelea kuwa magumu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…