Mishikaki ya Nemba: Maoni na Ushauri

guwe_la_manga

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
2,820
Reaction score
2,758
Wakuu wasaalam,

Poleni na changamoto ya baa la korona. Mimi ni mchoma mishikaki ya ng'ombe inayotokana na nyama ile ya juu ya tumbo, ile yenye nyuzi nyuzi ijulikanayo kama Nemba.

Kwa hapa nilipo Nemba moja inakost kati ya 8k-12k. Na ukiikata vizuri inatoa mishikaki kati ya 100-200
Ukipata ng'ombe aliyenona mishikaki ufika hata 250. Hivyo ukitoa mkaa, viungo ,mishikaki ya nyongeza na gharama zongine ndogo,faida ipo na ni uwa kati ya 5k-15k

Kwa nia ya kukuza biashara yangu ningependa kujuzwa ni wapi naweza pata nyama hii kwa bei ya chini ya 10k?

Niko tayari kuhamia hapo ili kufanya kazi.

Meatu,Simiyu.
 

Attachments

  • 20200512_073024.jpg
    279.6 KB · Views: 13
  • 20200512_095118.jpg
    276.9 KB · Views: 13
  • 20200512_095101.jpg
    222.5 KB · Views: 12
  • 20200512_073116.jpg
    263.8 KB · Views: 12
Niko mbali kabisa. Kuna jamaa hapa ana laki hajui afanye nini nishampa dili hili.
Mwambie hii biashara hainaga hasara Sanasana ajitahidi ajumuie tangawizi,Limao na vitunguu swaumu vya kutosha,atafute jiko la kuchomea zuri na bei huwa ni kati ya 15k-25k

Apate mkaa gunia moja,nyanya za kachumbari debe moja afu kisha ataleta mrejesho
 
Naomba kuelimishwa 15k k inasimama badala ya nini?
 
Lakini K lazima ina kirefu Chake .kwa Hiyo any figure ikaishia 000 ina maana K?
 
Tangu 2020 iingie hakuna kitu nilichokiwaza ×nyingi sana kama hii Biashara, haipiti masaa 3 bila kuwaza mishikaki.

Hii Biashara ni utajiri mkubwa sana hata mtoa mada hajajua kivipi utajiri.

Yupo jamaa anatengeneza Million 6 kila mwezi ndio aliye ni Inspire.

Nilichojifunza Duniani kitu chochote kina pesa, itategemea “jinsi utavyokifanya tu”


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…