Misiba ya matajiri vs misiba ya masikini

Misiba ya matajiri vs misiba ya masikini

Loading failed

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2023
Posts
2,603
Reaction score
7,501
Ndugu zangu..


Kumekua na tabia mbaya ya watu kuhudhuria kwenye misiba kwa kubagua kutokana na itikadi zao na hali ya kiuchumi ya marehemu au familia na ukoo wa harehemu husika kama tunavyojionea huko kwenye jamii zetu.


Ndugu utakuta kwenye misiba ya familia zinazojiweza kiuchumi watu wanaacha shughuli zao na wanajitokeza kuhudhuria kuliko misiba ya wasio navyo, asubuhi, mchana ,jioni na hata usiku wengine wanalala hapo kabisa hawaondoki hata iwaje iwe jua iwe mvua wanakomaa hapo. tofauti na misiba ya marehemu anaetoka kwenye familia za wasio jiweza hata mahudhurio yapo ya kusua sua sana na wakati mwingine hakuna kabisa labda tuu ile siku ya kuzika ndo utaona watu kwa kiasi kidogo


Ndugu zangu kwenye misiba ya matajiri hata ukitangazwa tuu leo, utakuta watu wapo kwa wingi wanazunguka zunguka hapo nyumbani na wengine kugeuza ndiyo vijiwe vya kupiga story kwa sababu wanajua asubuhi watapata chai, mchana watapata chakula na usiku pia kitapikwa chakula na chai itasambazwa au uji tofauti na misiba ya wasio navyo wanajua pale utaenda na rambi rambi yako na kurudi mtupu na njaa zako bila kula chochote hata maji ya kunywa hakuna labda tuu ya kudownload yasiyo ya uhakika kupatikana


Kwenye misiba ya matajiri na watu maharufu hata kama hawaendi kanisani, misikitini, na kwenye jumuiya au masinagogi utakuta viongozi wa dini kwa itikadi zao wanafanya unafiki kwenda kumzika kwa ibada na dua huku wakifumbia macho upande wapili kama hawajui kiimani hawakua akishiriki pamoja nao , hata kama alikana imani watajifanya wanafata itikadi za wazazi wao au watoto wao, tofauti na ilivyo kwa masikini (watu wa maisha ya chini) hata usipoenda jumuiya au kushiriki kijamii na wenzako huzikwi unasusiwa hapo haijalishi jina lako litasadifu imani husika ya kufikirika


Kwenye misiba ya matajiri na watu maarufu watajitokeza wakazi kwenda kuuza sura huko, kujitoa kwa bidii na hata wengine kugeuza ndiyo magenge ya kufanya biashara na kutafuta channel tofauti na misiba ya watu wasiojiweza watasingizia kule kumejaa wahuni au bodaboda wanaoleta fujo na vijana wavuta bangi wasio na maadili mema.


Kwenye misiba ya matajiri utakuta ni rahisi sana wazee kuchangamana na vijana ila kwenye misiba ya watu wa chini utakuta mara nyingi wazee wanajitenga na vijana huku wakipiga story kwamba vijana hawana maadili na wengi wakiopo hapo ni vijana wezi lengo ni kuhalalisha uharamu wao wa kuto kuhudhuria kwenye misiba ya wenzao wa hali ya chini.


Nb. Kila mwenye mwili atarudi mavumbini, udongo unakula na ndiyo kitanda cha watu wote haijalishi wewe ni tajiri au masikini, wale funza hawatokukula kwa kuangalia wewe una status gani na wakati mwingine hawajui hilo tubadilike tuache kuchagua misiba ya kwenda .
 
Kama Stivoo nilimwona juzi analeta zogo la story na vicheko wakati ibada ya mazishi inaendelea pale makaburininkwa Kondo
 
Tutafute hela.....

Unachokisema ni sahihi, mwenye hela akiumwa tu watu watajaa kumsalimia madaktari watamfata nyumbani kwake, ila masikini utasalimiwa na wanao tu. Tutafute hela.
 
Mwenye hela anaajiri watu wengi ana asaidi watu wengi ana shughuli za kukutana na watu wengi sadaka anatoa nyingi na anafahamika na waumini wengi ,mtaani wanamjua wengi nk unategema msiba wake ulingane na wa maskini? Ambaye kwanza wanaomjua wachache hana vitu vya mzunguko vya shughuli vya wengi
 
Hayo mambo labda yapo huko mujini kwenu dasalamu sisi huku kwetu kama unashirikiana na jamii hata uwe maskini vipi lkni msiba ukitokea kwako watu watafurik km kawaida
Dar misiba ikitokea watu wanaenda kufanya umalayer na kuuza sura ili waonekane na walimwengu.
 
Ukiwa na Hela utaogopa kifo tu.

Rostam aliikoromea mahakama, ikajibu kwa masijitiko tu wakati masikini hata simu ikiinguza meseji mahakamani unawekwa selo.
 
Na maskini akifa ibada itaendeshwa na housegirl wa mlinzi wa kanisa ila akifa tajiri Askofu atashirikiana na jopo huru la maaskofu na mapadri kuendesha ibada. UMASKINI NI FEDHEHA. Ndugu mleta uzi kamwe dunia haitakaa iwe na usawa.
 
Msiba wa mafuru ukionyeshwa clip kwa haraka hararaka hauwezi kujua kama ni msiba.
 
Msiba ama harusi, nitashiriki kwa namna ambavyo mimi na muhusika maisha yetu yalivyogusana, siangalii tajiri ama maskini..
 
Na maskini akifa ibada itaendeshwa na housegirl wa mlinzi wa kanisa ila akifa tajiri Askofu atashirikiana na jopo huru la maaskofu na mapadri kuendesha ibada. UMASKINI NI FEDHEHA. Ndugu mleta uzi kamwe dunia haitakaa iwe na usawa.
Duuuu ial watu jaman🤣🤣
 
Ndugu zangu kwenye misiba ya matajiri hata ukitangazwa tuu leo, utakuta watu wapo kwa wingi wanazunguka zunguka hapo nyumbani na wengine kugeuza ndiyo vijiwe vya kupiga story kwa sababu wanajua asubuhi watapata chai, mchana watapata chakula na usiku pia kitapikwa chakula na chai itasambazwa au uji tofauti na misiba ya wasio navyo wanajua pale utaenda na rambi rambi yako na kurudi mtupu na njaa zako bila kula chochote hata maji ya kunywa hakuna labda tuu ya kudownload yasiyo ya uhakika kupatikana
Sidhani kama kutakuwa na mtu mwenye akili timamu ataenda msibani na kuacha majukumu yake ili akapate chai ya bure ambayo kwa hakika haiwezi kuizidi chai ya buku2 uraiani.

kwanza chakula cha ngao sio.
 
Back
Top Bottom