Uchaguzi 2020 Misingi imara ambayo Mwl. Julius Nyerere aliwaachia watanzania imesababisha CHADEMA ipoteane wakati wa kampeni

Mkiwa hamna hoja acheni wengine waandike!Ika ukitaka kuandika wewe tu mwisho wa siku unajikuta unaandika vitu vya kawaida kabisa ambavyo unadhani ni propaganda yenye uhai,kumbe watu wanakuona ni "walewale"!
Ahaaa. Bado siku 52 watu tutashuhudia mengi.
 
Kwa sasa kama ni kwenye mpira unaweza kusema Chadema wamepoteana. Maana hawajui mpira waanzie wapi! Waanzie pembeni nyuma au waanzie mbele. Maana kila hoja wanayoibua imeonekana ni hoja mfu na haiuziki.

Lakini yote ya haya yanayowakuta Chadema ni kwa sababu muasisi wa taifa letu Mwl Julius kambarage Nyererea aliacha misingi imara ndani ya mioyo ya Watanzania. Na misingi hiyo ni kuwa wazalendo. Maana taifa huwa linajengwa ndani ya mioyo ya wanananchi wake.

Kwa uzalendo walionao watanzania kila hoja ambayo imekuwa ikiibuliwa na Chadema wamekuwa wakiipuuza na kuwaona kuwa hawafai. Mfano walikuja na hoja ya kuwa hivi sasa kinachofanyika ni maendeleo ya vitu na sio watu. Kwa uzalendo wa watanzania, Chadema imepuuzwa sana. Maana huwezi kusema ujenzi wa kituo cha afya au barabara sio maendeleo ya watu, maana vinajengwa ili vitumiwe na watu.

Walikuja na hoja ya kipuuzi eti kujenga miundo mbinu,shule na hospital si kitu si chochote. Maana hata mkoloni alijenga. Pia walienda mbali na kudai eti, maendeleo katika sekta hizi hayana maana sababu hivi sasa hakuna uhuru. Maneno haya yamewaudhi sana watanzania wazalendo. Yaani Chadema hawajui kuwa mkoloni alikuwa anatunyonya kwa kila kitu? Kuwa alijenga miundo mbinu sehemu ambazo alikuwa na maslahi, kama sehemu ambazo kuna malighafi. Na kuhusu uhuru unaweza kusema hakuna uhuru hapa Tanzania? Watu wanafanya shughuli na kujadili mambo usiku na mchana!

Wamekuja kuona wamebugi wakaja na hoja ya bima ya afya kwa kila mtanzania. Watu wakahoji mtaitekeleza vipi? Wakakosa majibu. Kumbe ilani ya Ccm imelitanabaisha hili suala vizuri kabisa na limewekwa wazi namna ambavyo litatekelezwa. Hapo ndio wameishiwa nguvu.

Kuharibu kabisa pale walipowadhalilisha watanzania kuwa nchi hii inalishwa kila kitu na mabeberu. Hili limewakera sana watanzania. Sababu misingi aliyoiacha mwl Nyerere ni kuwa taifa linalojitegemea. Ndio maana ukienda kila kona watanzania wanajishulisha na kilimo,biashara na ufugaji. Na hii imewavunja nguvu Chadema maana wananchi wamewapuuza sana. Hata moto walionza nao kwenye kampeni umeanza kufifia.
Mkuu huu ujinga uko ccm pekee tu, waweza kuta na wewe ni mtu mzima. Mimi kama ningekuwa Polepole leo usingepata hiyo buku7
 
Wengine hawajui wanasimamia hoja gani,binadamu anayo mahitaji muhimu mengi.
Kwa mfano sioni shida ya Magufuli kujigamba kwa kuharakisha umeme wa REA au kutafuta vyanzo vipya vya kuzalisha umeme rahisi kama Ujenzi wa Bwawa la Nyerere.

Sisi tungehoji uhakika wa kupata umeme masaa 24 bila kukosa,na salama.Pia tutahoji bei yake kama ni nafuu.Vile vile tutahoji kama huduma ipo wazi bila mizengwe.Ajira ngapi za kudumu na za muda zimetengenezwa kwa miradi hiyo.Je serikali imeifanya kwa ufanisi au hapana.Je makampuni ya wazawa yanashiriki kikamilifu.
Hayo ndio tungewabana wakatoa majibu lakini sisi tunasema sio maendeleo hivyo hayana maana.
 
Kwa sasa kama ni kwenye mpira unaweza kusema Chadema wamepoteana. Maana hawajui mpira waanzie wapi! Waanzie pembeni nyuma au waanzie mbele. Maana kila hoja wanayoibua imeonekana ni hoja mfu na haiuziki.

Lakini yote ya haya yanayowakuta Chadema ni kwa sababu muasisi wa taifa letu Mwl Julius kambarage Nyererea aliacha misingi imara ndani ya mioyo ya Watanzania. Na misingi hiyo ni kuwa wazalendo. Maana taifa huwa linajengwa ndani ya mioyo ya wanananchi wake.

Kwa uzalendo walionao watanzania kila hoja ambayo imekuwa ikiibuliwa na Chadema wamekuwa wakiipuuza na kuwaona kuwa hawafai. Mfano walikuja na hoja ya kuwa hivi sasa kinachofanyika ni maendeleo ya vitu na sio watu. Kwa uzalendo wa watanzania, Chadema imepuuzwa sana. Maana huwezi kusema ujenzi wa kituo cha afya au barabara sio maendeleo ya watu, maana vinajengwa ili vitumiwe na watu.

Walikuja na hoja ya kipuuzi eti kujenga miundo mbinu,shule na hospital si kitu si chochote. Maana hata mkoloni alijenga. Pia walienda mbali na kudai eti, maendeleo katika sekta hizi hayana maana sababu hivi sasa hakuna uhuru. Maneno haya yamewaudhi sana watanzania wazalendo. Yaani Chadema hawajui kuwa mkoloni alikuwa anatunyonya kwa kila kitu? Kuwa alijenga miundo mbinu sehemu ambazo alikuwa na maslahi, kama sehemu ambazo kuna malighafi. Na kuhusu uhuru unaweza kusema hakuna uhuru hapa Tanzania? Watu wanafanya shughuli na kujadili mambo usiku na mchana!

Wamekuja kuona wamebugi wakaja na hoja ya bima ya afya kwa kila mtanzania. Watu wakahoji mtaitekeleza vipi? Wakakosa majibu. Kumbe ilani ya Ccm imelitanabaisha hili suala vizuri kabisa na limewekwa wazi namna ambavyo litatekelezwa. Hapo ndio wameishiwa nguvu.

Kuharibu kabisa pale walipowadhalilisha watanzania kuwa nchi hii inalishwa kila kitu na mabeberu. Hili limewakera sana watanzania. Sababu misingi aliyoiacha mwl Nyerere ni kuwa taifa linalojitegemea. Ndio maana ukienda kila kona watanzania wanajishulisha na kilimo,biashara na ufugaji. Na hii imewavunja nguvu Chadema maana wananchi wamewapuuza sana. Hata moto walionza nao kwenye kampeni umeanza kufifia.

Huna akili....hoja mfu mkulu wenu angehangaika kujibu kwa kutapa tapa..hani imefikia hatua akipanda jukwaani anajibu hotuba za wenzake...

Nyie mmeisha
 
Watz wanataka mabadiliko...... Hawamtaki kidudumtu aliyeharivu nchi Kw miaka 5
 
Ni vigumu saana kwa watanzania kuchagua upinzani hii inasababishwa na mfumo wa kijamaa

watanzania wengi wanaamini wapinzani wapo kwa maslahi ya wazungu
Hata hivyo ni kweli..ukitazama kwa makini unaona wazi wapinzani wana uchu tu wa kujiona ni Rais au waziri mkuu,wana uchu wa madaraka na pesa na wala siyo uchungu wa wananchi,hawawezi kufanya chochote cha maana zaidi ya yote baada ya muda utasikia tena wananchi hawa hawa wanalalamika na wao kama wapiga dili wataishia kusema muda hautoshi CCM iliharibu inchi...yani kiufupi tukisema kuwapa wapinzani ili inchi ifanyiwe majaribio tumekwisha
 
Back
Top Bottom