Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MISINGI MIKUU UNAYOTAKIWA KUIJENGA KWA AJILI YAKO AU FAMILIA YAKO
Anaandika, Robert Heriel
Mjenzi huru
Andiko hili lamfaa mtu yeyote, wa umri wowote, wa jinsia yoyote, wa Hali na hadhi yoyote, wa mbari na jamii yoyote naam yeyote yule. Kwani kila nilichokiandika nimekipima, tena lugha niliyotumia ni njema isiyo na ukali, wala ukakasi, wala haikeri. Maneno yote yametolewa hesabu, ni yenye manufaa Kwa wapenda manufaa, ni yenye ufahamu Kwa wapendao maarifa.
Niite Taikon wa Fasihi, mjenzi huru.
Kila mmoja anatarajia kuwa na maisha Bora. Ni ndoto yetu bila Shaka kuwa na kizazi Bora. Tunatamani watoto wetu waishi maisha yenye mafanikia yenye maana. Familia bora, jamii Bora, na taifa Bora ni ndoto iliyootwa na Wazee wetu waliotutangulia. Hata sasa tungali tunaishi ni ndoto yetu kuwa na taifa Bora lenye mafanikio katika dunia hii. Kuwa mfano Bora Kwa mataifa mengine.
Hatuna mkataba na Muda; wenyewe hufanya upendavyo pasipo kutushirikisha. Unaenda mbio kama upepo ukituachia kilio pale tusipotimiza malengo yetu tulioyapanga. Muda! Wakati! Nyakati ndio utaamua yote tuyafanyao kama tutafanikiwa ama Laa!
Sisemi muda ni mchache Kwa maana hatujui akiba yake. Hata hivyo tunafahamu muda wetu umewekewa mipaka, labda kuna wakati tukaiona mipaka hiyo haitoshi kutimiza Yale tuliyoyapanga, wapo waishio miaka tisini na kenda, na wapo waishio nusu au Robo ya Karne na kutoweka katika njia ya wote wenye mwili. Je tuyaone maisha hayana maana, na tuseme maisha ni ubatili yasiyofaa kitu. Hapana, hatuwezi kuwaza Kwa namna hiyo achilia mbali kusema. Huko ni kukata tamaa na kukosa matumaini, zaidi ya yote ni kutokuwa na upendo Kwa watoto wetu.
Sisi tuliishi zamani kupitia Wazee wetu waliotutangulia, na sasa tunaishi badala Yao baada ya wao kuondoka, na tutaishi baada ya kufa kupitia Kwa watoto na wajukuu wetu. Sema "Tutaishi, naam Tutaishi Milele"
Ikiwa tutaishi milele kupitia miili hii, na kupitia Wale waishio ndani ya miili yetu, wengine tuliwazaa na wengine watazaliwa kupitia Sisi au watoto au wajukuu zetu. Hiyo inatupa kazi muhimu na yalazima ya kufanya. Ulazima huo ndio huyafanya maisha yetu yawe ya thamani na yenye maana. Kwa sababu "TUTAISHI MILELE"
Taikon, ndimi mjenzi huru, labda nimeongea kirefu lakini sikusudii kuwachosha ndugu zangu, kama ingekuwa hivyo basi Mimi mwenyewe ningechoka kabla yenu. Ila dhamiri njema inanituma kusema kila ninachoona kinafaa ambacho ni muhimu na lazima.
Kila Jambo lina misingi yake lakini maisha msingi wake ni upi? Subiri! Ngoja kidogo.
Katika maisha ya mwanadamu kuna mambo makuu manne;
i. Akili/Utashi
ii. Roho
iii. Hisia/Nafsi
iv. Mwili
Mambo hayo manne hushirikiana Kwa pamoja katika kumfanya mwanadamu aweze kuishi Kwa Raha mustarehe au Kwa huzuni na taabu.
Mambo hayo makuu manne hujengwa kwa misingi mikuu minne.
i. Akili/Utashi msingi wake Mkuu ni UFAHAMU.
ii. Roho. Msingi wake Mkuu ni IMANI.
iii. Hisia/Nafsi. Msingi wake Mkuu ni UPENDO
iv. Mwili. Msingi wake Mkuu ni AFYA
Hivyo maisha ya mwanadamu yanamisingi Mikuu minne kama nilivyoitaja hapo, naam Ndio Ufahamu, Imani, Upendo na Afya.
Mwanadamu Kama moja ya viumbe hai kila kitu amekijenga katika msingi, yaani mwanadamu hawezi kujenga kitu pasipo kuwa na msingi/chanzo au kianzio au mtaji.
Mungu pekee ndiye anaweza kujenga kitu pasipo msingi, yaani anayeweza kuunda kitu pasipo ya kitu. From nothing to something. Ndio maana Mhenga mmoja ninayempenda Sana aitwaye Yesu wa Nazareth aliwahi kusema; Mwenye nacho atazidi kuongezewa; asiye nacho hata kile kidogo anachodhani anacho atanyang'anywa. Falsafa hiyo ni moja ya nyongeza muhimu katika andiko langu. Kwa maana Sisi Wajenzi tunafahamu hatuwezi kujenga Nyumba bila ya Msingi.
Sikatai ipo msingi Imara na misingi dhaifu hiyo ni mada nyingine lakini muhimu hapa lazima pawepo na Msingi, foundation, Pioneering.
Taikon sipendagi kuzungumzia mambo yasiyo relevant na maisha halisi. Moja ya tabia zangu ninazozipendelea ni kuzungumza mambo halisi yanayotokea katika maisha ya kila mmoja wetu. Ili kufanya kila mtu aelewe hata kama angekuwa na Uelewa mdogo kiasi gani.
Maisha ya kila mmoja wetu yamejengwa katika misingi Fulani. Aidha misingi hiyo ni kutoka Kwa wazazi au walezi na hata kwenye jamii inayotuzunguka.
Ili mtu uwe mtu Bora unayehitaji kurejea katika Yale mambo makuu manne niliyoyataja hapo juu.
Hapana Shaka watu hufikiri maisha mazuri ni kuwa na mafanikio ya kifedha pekee, ndio hayo pia ni sehemu ya mafanikio ambayo bila Shaka yamelengwa kufurahisha Miili yetu hasa Afya na uzima wetu.
Mwili na Afya ambapo mafanikio yake yamejengwa katika ndoto ya mafanikio ya majumba mazuri, chakula kitamu chenye virutubishl, maji Safi na salama, mavazi pamoja na mashine zote zinazomrahisishia mwanadamu kazi na shughuli zake kama Magari, simu, n.k. pia zina misingi yake.
Mambo hayo yanahitaji msingi bora.
Ukiona mtu yeyote amefanikiwa au taifa lolote limefanikiwa basi jua litafuata misingi hiyo minne niliyoitaja katika kuyafanya Yale mambo makuu manne yanayoendesha maisha ya mwanadamu naam ndio Akili, roho, hisia/Nafsi na mwili. Ambayo misinbi Yao ni Ufahamu, Imani, Upendo na Afya.
Katika ujenzi kuna hatua za ujenzi, nazo ni;
i. Kuandaa kiwanja/eneo la ujenzi
ii. Kujenga msingi
iii. Kupandisha Boma
iv. Kupaua
V. Kufanya Finishing
Katika Yale mambo manne wakati unayajenga lazima ujue upo hatua ya ngapi.
Kama upo katika ujenzi wa mambo ya kimwili, hasa mambo ya kiuchumi lazima ujue upo hatua ipi. Je wazazi wako walifika wapi, kama walifikia kwenye Msingi, ukague msingi kuwa upo Imara au laa. Kama upo Imara automatically wewe utapandisha Boma bila tatizo. Lakini kama Msingi haupo Imara automatically Boma kulijenga litakushinda na ukilazimisha sio ajabu nyumba ukaikuta inanyufa na wakati mwingine utaangukiwa.
Ili ufanikiwe kiuchumi wewe na kizazi chako lazima ujenge msingi mzuri kwenye masuala ya ufahamu/akili na utashi, utambuzi, alafu Imani/kiroho Kwa kadiri ya unavyoamini, Hisia/Nafsi usiendeshwe na mihemko moyo uwe umetulia, kisha Mwili, nguvu zako.
Imani hujengwa Kwa kuona na kusikia matukio uliyoyafanya au kufanyiwa. Imani msingi wake Mkuu ni kuona na kusikia, lakini unasaidiwa na Akili katika kutunza kumbukumbu. Imani ili ifanye kazi lazima mtu awe na kumbukumbu na kumbukumbu ipo katika msingi wa ufahamu.
Huwezi kuwa na Imani ya kushinda Jambo Fulani Kama hauna kumbukumbu yoyote ya kitu ambacho uliwahi kushinda. Hiyo haijawahi kutokea na haitokuja kutokea. Ili Imani iwepo lazima Akili iwepo. Imani pasipo akili mi upumbavu, ni Ile mtu kujiaminisha ujinga, yaani kujiaminisha kitu kisichowezekana. Na Imani pasipo matendo ya Mwili imekufa.
Hii ni kusema Imani ni sehemu ya lazima ya mafanikio ya kimwili. Jambo lolote la kimwili limetokana na Imani na AKILI.
Ndio maana ili ufanikiwe lazima uanze na mambo madogo ili yakujenge kiimani na kiakili. Huwezi miliki Kampuni kubwa kabla hujaanza kumiliki biashara ndogo hiyo haipo na haijawahi kutokea.
Wahenga walisema; Majaribu ni mtaji wa Imani. Yaani kadiri unavyofanikiwa kushinda majaribu unajenga msingi wa Imani yako. Mfano; ukifanikiwa mtihani wa Darasa la Saba hiyo inakupa Imani kuwa utafaulu mtihani wa Kidato cha nne. Kwamba Kama nilifaulu pale basi hata hapa nitafaulu.
Daudi alipokuwa anaenda kupigana na Goliathi, yeye alikuwa na Imani atampiga Goliath Kwa sababu hapo nyuma alishamuua Dubu na Simba. Hivyo kumbukumbu/ufahamu huo ndio ulijenga Imani yake kumpiga Goliath. Kama asingekumbuka Jambo hilo ni wazi asingekuwa na ujasiri na Imani ya kutaka kupigana na Goliath.
Mambo unayoyapitia hivi leo ni muhimu katika kukujenga katika mambo makubwa yanayokuja. Ni lazima uhakikishe unayashinda ili iwe reference nzuri kwa Yale yanayokuja. Hata ukienda kuomba kazi lazima uwape CV yako wakujue wewe ni Nani na uliwahi kufanya nini. Ili wawe na Imani na wewe kwamba utatenda mambo ya Akili na nguvu watakayokupa.
Mtu asiye na kumbukumbu hawezi kufanikiwa, hata hivyo ni muhimu kila mara kupata wasaa wa kukumbushana ili kujua wapi tunaenda/mafanikio yetu tunayoyahitaji ni yapi.
Nimeandika Sana, pengine wengine wakaona nimewachosha, nitaendelea kipande kingine siku nyingine. Leo nimeongea Kwa ujumla.
Ni Yule mjenzi huru.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam.