Misingi ya Mafanikio na Boaz Donard Mwakasaka

Misingi ya Mafanikio na Boaz Donard Mwakasaka

SOUND HEALTH

Member
Joined
Jul 8, 2014
Posts
82
Reaction score
25
Kuanzia mwezi June 2015 Boaz Donard Mwakasaka atatoa mafunzo kuhusu misingi ya mafanikio katika nyanja mbalimbali kama kilimo, biashara, elimu, ujasiliamali nk. Semina hizi zitaendeshwa chini ya tasisi iitwayo mount Rungwe mastermind. Semina zitaanzia wilayani Rungwe mkoani Mbeya na baadaye kusambaa nchi nzima kwa utaratibu utakao tolewa. Lengo kubwa ni kuchochea maendeleo kupitia elimu hiyo. Mafunzo hayo yatatolewa bure kabisa kwa yeyote atakaye penda kushiriki.

Mafunzo yatagusa.


  1. Namna ya kuweka lengo kubwa sana na kutengeneza mikakati ya kitaalamu kufikia lengo hilo
  2. Ufahamu mkuu
  3. Jinsi ya kuondokana na hofu mbalimbali
  4. Elimu ya fedha
  5. Uongozi
  6. Nguvu ya fikra
  7. Namna ya kujenga ari ya kufanya kazi
  8. Jinsi ya kujitawala mwenyewe
  9. Kanuni ya kuvuna zaidi ya unachopanda
  10. Namna ya kuwa mtu mwenye mvuto mkubwa
  11. Namna ya kujenga uwezo wa kufikiri kwa ufasaha
  12. Ushirikiano
  13. Namna ya kukabili changamoto
  14. Jinsi ya kuchukuliana na wengine
  15. Nguvu inayoongoza dunia

Wakazi wa Rungwe mkoani Mbeya kaeni mkao wa kula kwa uamsho mkuu wa mafanikio. Wenye nia ya kushiriki watume majina kwenye namba 0716 60 99 16. Kumbuka hakuna gharama yoyote, mtarifu na mwenzako.
 
Yeye ana mafanikio gani?
Aina hii ya ujasiliamali naona imeshika kasi.
Sasa hivi kila mtu ni mhamasishaji.
Mtu anafundisha kufuga kuku wakati yeye mwenyewe hata njiwa hajawahi kufuga.
 
Yeye ana mafanikio gani?
Aina hii ya ujasiliamali naona imeshika kasi.
Sasa hivi kila mtu ni mhamasishaji.
Mtu anafundisha kufuga kuku wakati yeye mwenyewe hata njiwa hajawahi kufuga.
Ni bora mara mia kuliko kukalia umbea na kujadili Manchester na arsenal ujinga mtupu.
 
i think source ni success book
Hakuna jipya sasa hivi hakuna kwenye uwanja wa biashara unaloweza kulivumbua jipya ndio mana wataalam wote duniani wamesoma vyuo mbalimbali wote wanajifunza mawazo ya wengine waliopita. Labda kama unataka akawaadisie ndoto za usiku.
 
Hakuna jipya sasa hivi hakuna kwenye uwanja wa biashara unaloweza kulivumbua jipya ndio mana wataalam wote duniani wamesoma vyuo mbalimbali wote wanajifunza mawazo ya wengine waliopita. Labda kama unataka akawaadisie ndoto za usiku.
Yapo mengi tu mapya ila ni uvivu
 
Motivational speaker wengi ni watu wenye mafanikio makubwa wakina kayosaki, trimphy wakina carson.. Sasa hapa bongo mtu hana hata kibanda cha nyanya anakueleza mafanikio
 
hatafundisha kufuga kuku.Atafundisha namna ya kutengeneza lengo na mikakati ya kulifikia.lengo lolote katika biashara elimu,kilimo siasa na mengineyo.kwa hiyo watu wote ni walengwa.hapa hakuna ubaguzi
 
Back
Top Bottom