SoC02 Misingi ya Utawala Bora ni ipi? Tufanye nini ili tuwe na Utawala Bora?

SoC02 Misingi ya Utawala Bora ni ipi? Tufanye nini ili tuwe na Utawala Bora?

Stories of Change - 2022 Competition

Ms drya

New Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
3
Reaction score
3
Habari zenu Wana JAMII FORUMS, Hususa ni jukwaa la "STORIES OF CHANGE" Nimatumaini yangu kuwa nyote ni wazima na mnaendelea na majukumu ya kila siku.
Andiko hili litaangazia katika ngazi za utawala Hususa katika misingi ya utawala bora ni ipi?hali imekua tofauti kwa kipindi Hiki misingi ya utawala bora imebaki tu kuandikwa katika vitabu na sio mioyoni mwa viongozi wetu.

UTAWALA BORA
Kwanza kabisa, utawala ni matumizi ya kisiasa yanayo simamia masuala ya nchi katika ngazi zote,NA utawala bora ni matumizi ya mamlaka ,uwajibikaji na utendaji wa haki kwa kila raia kwa usawa na uadirifu. Mambo ya kutekeleza dhana ya utawala bora yapo lakini baadhi ya viongozi hawayafuati na kuyazingatia,Mambo hayo ni kama YAFUATAYO,:
; KUTAMBUA NA KUJUA MADARAKA NA MATUMIZI YAKE
Ili kutekeleza dhana ya utawala bora ni lazima uzingatie hili jambo,lakini baadhi ya viongozi wetu wamekua wakitumia madaraka yao vibaya na kuwakandamiza watu wa hali ya chini, MFANO;ukiangalia Afrika Mashariki na ya kati Tanzania ndiyo yenye bei ya chini kabisa ya mafuta na vitu vingine,lakini watu wanao simamia sekta hizo hawasemi na wala kutoa ushitukiano kwa kupanda na kushuka kwa bei na matokeo yake mafuta yakipanda bei na wao wanapandisha ya kwao. hapo kwa namna nyingne sisi wananchi wa hai ya chini wanatukandamiza, hivyo serikali tunaomba hili lifuatiliwe kwa undani zaidi.
Pia viongozi wetu watambue madaraka yao na matumizi yake,

; MADARAKA YATUMIKE KULINGANA NA MIPAKA ILIYO WEKWA NA SHERIA.
Viongozi wa ngazi za juu wamekua wakitumia nje na mipaka iliyo wekwa na sheria, hili pia limekua likiwaumiza wananchi wengi sana, MFANO; katiak ulipiaji wa pango/kodi serikali imetoa fursa katika ukusanyaji wa kodi kua watu walipe kodi kulingana na hali yake ilivyo,lakin viongozi baadhi walisahau hilo na kuwanyanyasa wananchi wa hali ya chini. Hivyo tunaiomba serikali iliangalie hilo katika ulipaji wa kodi/pango .

;MISINGI YA UTAWALA BORA NI IPI JAMANI??
NI kwanini viongozi wetu hawafuati misingi ya utawala bora na wananchi wengi wamekua wakiumia na kutoa malalamiko kwa viongozi wao na kupuuziwa, Misingi ya utawala bora IPO iliyo pitishwa na serikali lakini baadhi ya viongozi wetu wanasahau na baadhi yao kupuuzia kabisa na hiyo inawasababishia wananchi wengi kuuuma, MFANO; MISINGI YA UTAWALA BORA NI KAMA:
,✓USAWA
Usawa ni msingi wa utawala bora lakini viongozi baadhi hatendi haki ki usawa na kutowathamini wananchi wa hali ya chini na kuthamini pesa kuluko utu. Ninapo sema usawa namaanisha;
( 1 ) kuthamini watu bila kujali tofauti zao,
Baadhi ya viongozi wetu wanathamini sana pesa kuliko utu,na kuamini pesa ndio kila kitu MFANO; ukiangalia upande wa mahakamani watu wanathangaika sana na wengine kesi zao kufutwa na wengine kunyimwa haki yao ya kweli,na kuona kabisa Hakimu au Jaji akitoa hukumu kwa mtu asiye kua na makosa na kumuacha MTU mwenye makosa kua huru, kutokana na cheo cha mtu au kujuana kwao ndio kuna wapelekea kutotenda usawa na haki ya mtu kuizurumu. Sasa huo unaweza ukasema ni utawala bora,usawa umebaki kwa watu wenye hali ya juu tu kwa watu wa hali ya chini wanaumizwa .Hivyo serikali Tunaomba mliangalie hili kwa upande mwingine kwa sababu wananchi wanazurumiwa haki zao za msingi bila sababu yeyote.
( 2 ) kutambua makundi yote katikati jamii na kutoa fursa sawa kwa makundi yote katika kuboresha hali zao .
Viongozi inatakiwa watambue makundi yote na kutoa fursa mbalimbali ili kuboresha hali zao, MFANO WA MAKUNDI HAYO NI KAMA;
_Kundi la watu wasio jiweza
_vilema
_watoto wa mtaani na
_wazee
Hawa watu wanateseka sana wanakosa huduma za msingi na msaada ,tukiangalia mabarabarani tunakutana nao wengi sana , kwanini viongozi wetu wasikae chini na kutoa mchango wao walau hata kwa watu wachache tu na hili litatupunguzia kundi la wezi na vibaka, mfano serikali ikitoa elimu kwa watoto wa mtaani na kuwapa fursa za kazi walau kwa watu wachache tu kwa sababu naamini kama kundi kubwa la watu wakifanikiwa wizi,ubakaji,ukatili,na fitina zitapungua katika nchi yetu.

° ✓ UWAZI.
HUU pia bi msingi wa utawala bora, ninapo sema uwazi namaanisha ni kuendesha shughuli za umma bila usiri wowote,ili wananchi wawe na uwezo wa kuelewa nakupima utendaji kazi wa viongozi wao,pia tunapo sema uwazi tunamaanisha;
( 1 ) Wananchi kupewa Taarifa za Mapato na Matumizi Yote.
MFANO WA MAPATO NI KAMA ;TRA wananchi tunapaswa kujua mapato hayo na Matumizi Yote ili kujihakikishia kua serikali ipo katika kipindi gani?
( 2 ) Wananchi kufagamishwa huduma zitolewazo bila malipo na huduma zinazopaswa kuchangia Na utaratibu wote wa kupata huduma hizo.
Wananchi tufahamishwa huduma mbalimbali zitolewazo na serikali Bure, MFANO; huduma kwa watu wenye uhitaji, walemavu na wazee,. Huduma hutolewa kama pesa,chakula na mavazi hivyo tunaiomba serikali tutambue utaratibu wote wa kupata huduma hizo.kwa sababu huduma hizo ni muhimu sana katika maisha yetu. pia ukija upande wa huduma zinazopaswa kuchangia ni kama kutoa msaada pia kwa watu hao sisi kama wananchi Tunapaswa kutoa mchango wetu pia na ni vyema kama serikali itakaa chini na kuliangalia hilo na tungependa tupewe Taarifa ni namna gani sisi wananchi tunaweza kutoa mchango wetu pia kwa utaratibu upi?
°✓ UADIRIFU.
Huu pia ni msingi wa utawala bora, hivyo ukiwa kama kiongozi ni lazima uwe mwadirifu . ninapo sema mwadirifu namaanisha ni kua na mwenendo mzuri katika utendaji kazi yako. pia uadirifu inajumuisha mambo yafuatayo
_ Kujali watu, ukiwa kama kiongozi kujali watu wako ni lazima
_Kufanya kazi kwa kuzingatia sheria .
_Kuwa mkweli.
_Kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
_Kuepuka vitendo vya rushwa.


MCHANGO WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI KATIAK KUJENGA NA KUDUMISHA UTAWALA BORA.;
ILI nchi yetu iwe na utawala bora ni lazima serikali itoe uhuru katika ngazi zifuatazo;

Uhuru huo ni kila Jaji au Hakimu awe huru kuamua kesi iliyopo mbele yake ki usawa bila kushinikizwa au kulazimishwa na mtu wa ngazi za juu au mwenye cheo kikubwa. Hivyo serikali itoe uhuru huo ili mahakama kutekeleza majukumu yake bila uwoga wala upendeleo wowote.

Kila mwanadamu anapaswa apate haki yake bila kuzurumiwa ,hivyo ili kujenga nguzo ya utawala bora ni lazima kila binadamu apate haki na mahitaji yake yote ya kimsingi kama vile;Haki ya kuishi,Haki ya kuongea,Haki ya kusikilizwa,Haki ya kuchangia hoja mbalimbali katika mikutano na mijadala mbalimbali.
Pia ili kuzingatia UTAWALA BORA katika utoaji wa haki za BINADAMU ni lazima pia vyombo vya kutoa haki vizingatie na kufuata misingi ifuatayo:
_Haki ya kulipwa fidia stahiki kwa watu wanaoathirika kutokana na makosa ya watu wengine.MFANO; kuchomwa kwa masoko dar es salaam,wananchi walio athirika walipwe fidia zao, Hivyo tunaiomba ilitazame hilo pia.
_ Kutenda Haki kwa wote bila kujali hali ya mtu kijamii na kiuchumi.
Pia serikali itambue mchango wa wananchi wote na kila mtu apewe haki stahiki bila ubaguzi wa rangi,kabila,na karia ya mtu.


>;MWISHO KABISA NIMALIZE NA KUSEMA KUA;
ILI kudumisha nchi yetu ni lazima tuwe na utawala ulio bora Na ili tuwe na utawala bora ni lazima tufuate na tuzingatie misingi na nguzo zote za utawala bora..pia serikali Tunaomba hilo kua misingi ya ya UTAWALA BORA ipo lakini viongozi baadhi hawaitendi ipasavyo., Hivyo serikali Tunaomba itoe mchango katika hilo...
;NISEME AKHSANTE SANA WEWE ULIE TUMIA MUDA WAKO KUPITIA ANDIKO HILI, PIA NINGEPENDA NIPOKEE USHAURI, NA MAONI KATIKA CHAPISHO HILI... AKHSANTENI SANA..
 
Upvote 1
Back
Top Bottom