Misri: 32 Wafariki na 63 wajeruhiwa kwenye ajali

Misri: 32 Wafariki na 63 wajeruhiwa kwenye ajali

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Watu 32 wamefariki na wengine 63 kujeruhiwa leo, katika ajali iliyohusisha basi la abiria na magari kadhaa kugongana na baadhi kuwaka moto katika mkoa wa Beheira nchini Misri kwenye barabara ya Cairo-Alexandria, kilomita 131 kaskazini mwa mji mkuu Cairo.

Ripoti zianaeleza wengi waliofariki vifo vyao vilisababishwa na mto uliozuka kwenye mgongano wa magari hayo ambapo jumla ya magari maalum ya kubeba wagonjwa 20 yalitumwa kwenye eneo la ajali kutoa msaada kwa majeruhi.

Waziri wa afya wa Nchi hiyo Dkt Khaled Abdel Ghaffar amesema waliojeruhiwa walihamishiwa hospitali moja huko Wadi al-Natrun, huku wengine wakipelekwa Al-Nubaria.
 
Nasikia ilikataa kuwapokea wakimbiz wa kipalestina? Mungu awaponye majeruhi...Amen
 
Back
Top Bottom