#COVID19 Misri kuwazuia wafanyakazi ambao hawajachanjwa kwenda kazini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Misri itawazuia wafanyikazi wa umma ambao hawajachanjwa dhidi ya kuingia katika majengo ya serikali kutoka katikati ya mwezi ujao.

Ilani ya baraza la mawaziri Jumapili ilisema wafanyikazi watalazimika kupewa chanjo au kufanyiwa vipimo vya Covid kila wiki ili waruhusiwe kuingia kwenye majengo ya serikali kutoka 15 Novemba.

Baraza la mawaziri pia liliruhusu kufunguliwa kwa bafu katika misikiti kutoka Jumatano.

Bafu zilifungwa mnamo Machi mwaka jana kama sehemu ya hatua za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona Serikali pia imetenga pauni bilioni Moja za Misri ($ 64m; £ 47m) kushughulikia janga hilo.

Misri imetoa chanjo zaidi ya milioni 30 kwa raia wake dhidi ya idadi ya watu zaidi ya milioni 100, kulingana na data kutoka kwa wizara yake ya afya.
 
Misri mbona wamechange ghafla,mwanzoni walikua wanakataa uwepo wa covid.

Misaada inabadilisha msimamo wao
 
Misri itawazuia wafanyikazi wa umma ambao hawajachanjwa dhidi ya kuingia katika majengo ya serikali kutoka katikati ya mwezi ujao.

Ilani ya baraza la mawaziri Jumapili ilisema wafanyikazi watalazimika kupewa chanjo au kufanyiwa vipimo vya Covid kila wiki ili waruhusiwe kuingia kwenye majengo ya serikali kutoka 15 Novemba.

Baraza la mawaziri pia liliruhusu kufunguliwa kwa bafu katika misikiti kutoka Jumatano.

Bafu zilifungwa mnamo Machi mwaka jana kama sehemu ya hatua za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona Serikali pia imetenga pauni bilioni Moja za Misri ($ 64m; £ 47m) kushughulikia janga hilo.

Misri imetoa chanjo zaidi ya milioni 30 kwa raia wake dhidi ya idadi ya watu zaidi ya milioni 100, kulingana na data kutoka kwa wizara yake ya afya.
Kama watazuiwa kwenda kazini means hawajagoma kwahiyo wataendelea kulipwa mishahara kwa mjibu wa sheria. Kwahilo sioni shida na Wafanyakazi wataibuka kidedea dhidi ya Serikali.
 
Mada nyingine unalazimika kupita kimya kimya ili usinukuliwe vibaya
 
Back
Top Bottom