Misri na Jordan ndio walinzi wa Israel ili isifutike

Misri na Jordan ndio walinzi wa Israel ili isifutike

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Israel ilijua zamani kuwa bila kuzitumia nchi mbili zilizo jirani yake kama kinga dhidi ya uvamizi wa taifa la Palestina basi hawataweza kuendelea kuwapo pale kama taifa.Nguvu ya kijeshi wanayojilimbikizia kwa msaada wa taifa la Marekani wala hazina athari kubwa kuliko unafiki wa viongozi wa nchi mbili hizi zinazopakana nayo ambazo ni Jordan na Misri.

Ushahidi wa manufaa ya mikataba hiyo imeonekana katika vita vya mwaka huu 2021 baina ya Israel na Palestina.Kule Sudan na Misri siku mbili kabla ya kusitishwa vita tayari wananchi wa nchi hizo walikuwa wamepandwa na hasira wake kwa waume wakitaka wafunguliwe mpaka ili waingie Israel wakajitoe muhanga.

Hali ilikuwa kama hiyo nchini Jordan ambako mara kadhaa jeshi la nchi hiyo lilipambana na wananchi waliojaribu kuvuka daraja la mfalme Hussein linalozitenganisha Jordan na upande wa Palestina uliozingirwa na Israel wa Ukingo wa magharibi.

Mkataba wa Jordan na Israel ulitiwa saini mwaka 1994 wakati wa uhai wa mfalme Hussein na waziri mkuu Yitzhak Rabin ulioshuhudiwa na raisi Bill Clinton.

1621779224097.png

Mkataba baina ya Misri na Israel ulitiwa saina mwaka 1979
1621780644235.png

Egyptian president Anwar Sadat, US president Jimmy Carter, center, and Israeli prime minister Menachem Begin clasp hands on the north lawn of the White House as they sign the peace treaty between Egypt and Israel, March 26, 1979. (AP/Bob Daugherty)
 
The so called Israel inakaliwa na walowezi wa kizungu wanaojiita waisraeli
Ndiyo, ni sahihi unachokisema.. Lakini leo hii wa Israeli halisi weusi kama ushahidi unavyo onyesha wakiamua kurudi hapo Yerusalemu wapelestna watakuwa na amani nao?.

Kwamba leo sijui mmatumbi akaishi hapo Yerusalemu inayokaliwa na Ashkenazi, wapalestina watawaacha mkae kwa amani et tu kwasababu wa Israeli halisi mmerudi?.

Ujue kwamba ili dai la wa Israeli fake linatumika kwa dhumni jingine, lakini hao Ashkanez wakitoka hapo hakuna mmatumbi wakutia pua yakw hapo, mtakufa wote kwa siku 1.
 
Israel ilijua zamani kuwa bila kuzitumia nchi mbili zilizo jirani yake kama kinga dhidi ya uvamizi wa taifa la Palestina basi hawataweza kuendelea kuwapo pale kama taifa.Nguvu ya kijeshi wanayojilimbikizia kwa msaada wa taifa la Marekani wala hazina athari kubwa kuliko unafiki wa viongozi wa nchi mbili hizi zinazopakana nayo ambazo ni Jordan na Misri...
Ila unaongoza kwa propaganda vile vita vya 1967 misri na Jordan wote walimvamia Israel na wakapigwa utasemaje wanamlinda Israel

Jews diaspora Wana ela ni matajiri na wavumbuzi ndo wanaoibeba Israeli acha propaganda
 
Ila unaongoza kwa propaganda vile vya 1967 misri na Jordan wote walimvamia Israel na wakapigwa utasemaje wanamlinda Israel

Jews diaspora Wana ela ni matajiri na wavumbuzi ndo wanaoibeba Israeli acha propaganda
Walowezi wa kizungu wamewekwa pale na USA&UK kwa manufaa wanayoyajua wao sasa huo mwaka 1967 hayo mataifa 6 ya kiarabu yangewezaje kuwashinda USA&UK huku unajua kabisa ndio mataifa makubwa duniani yenye nguvu za kijeshi???.

Anacho kisema huyo Jamaa yupo sahihi Jordan na Egypt ndio walinzi wakuu ndio ndio maana USA anatoa misaada ya pesa nyingi kwa Egypt ili tu asilete chokochoko kwa Israel na sio hivyo tu U.S.A huwa ana monitor uchaguzi wa Egypt nadhani unafahamu kilichompata Rais Mohamed Morsi mwaka 2012-2013.
 
Walowezi wa kizungu wamewekwa pale na USA&UK kwa manufaa wanayoyajua wao sasa huo mwaka 1967 hayo mataifa 6 ya kiarabu yangewezaje kuwashinda USA&UK huku unajua kabisa ndio mataifa makubwa duniani yenye nguvu za kijeshi???...
Ebu ntajie wafalme na Marais wa palestina waliokuwepo kabla ya 1947 sababu umesema Israeli ni walowezi wa kizungu waliowekwa pale
 
Ebu ntajie wafalme na Marais wa palestina waliokuwepo kabla ya 1947 sababu umesema Israeli ni walowezi wa kizungu waliowekwa pale
Kabla ya hapo Palestina ilikuwa ikitawaliwa na watawala tofauti tofauti na si lazima waitwe wafalme au maraisi.Mara ya mwisho ilikuwa ni sehemu ya utawala wa kiislamu wa Ottoman ambao ulianzia nchi za kiarabu mpaka Ulaya na Asia.
 
Ndo wakina Nani hao wataje majina nahakika huwezi wataja sababu hawakuwepo

Kabla ya mwaka 1947 hakukua na taifa linaloitwa palestina ottoman ilitawala kipindi Fulani tu, falme tofauti tofauti zilitawala kama roman empire na mtu wa mwisho alikua mwingireza hakukua na taifa linaloitwa palestina ndo maana hakuna mtawala wa palestina aliyekuwepo kabla ya 1947
 
Acha ungo, Ottoman empire ilianguka na Palestina ikaangukia mikononi mwa Mwingereza.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Ndo wakina Nani hao wataje majina nahakika huwezi wataja sababu hawakuwepo

Kabla ya mwaka 1947 hakukua na taifa linaloitwa palestina ottoman ilitawala kipindi Fulani tu, falme tofauti tofauti zilitawala kama roman empire na mtu wa mwisho alikua mwingireza hakukua na taifa linaloitwa palestina ndo maana hakuna mtawala wa palestina aliyekuwepo kabla ya 1947
Duh?!?!
 
Jifunze kutumia akili japo hata kidogo.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Wewe ndio utumie hiyo akili kama bado ipo lakini. Ameulizwa awataje watawala wa hilo eneo jamaa ametaja ottoman empire wewe unakurupuka kusema muongo hapo uongo wake upo wapi? Kutawaliwa na uingereza haifuti kwamba walitawaliwa na uturuki pia. Punguza ujuaji na kutafuta kukosoa ilimradi tu.
 
Hapo ndio naposema akili huna afu unashupaza shingo. Kasema mara ya MWISHO walitawaliwa na Ottoman empire, nikamwambia aache uongo, mara ya walitawaliwa na Uingereza, na ndio maana Uingereza ilishiriki (kama colonial master) kuigawa Palestina ili kuunda taifa la Israel.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Hapo ndio naposema akili huna afu unashupaza shingo. Kasema mara ya MWISHO walitawaliwa na Ottoman empire, nikamwambia aache uongo, mara ya walitawaliwa na Uingereza, na ndio maana Uingereza ilishiriki (kama colonial master) kuigawa Palestina ili kuunda taifa la Israel.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Kuigawaje palestina Tena hakukua na nchi inayoitwa palestina Bali kulikua na jamii za warabu na waisrael

Kama kulikua na taifa la palestina ntajie wafalme angalau watano wa palestina waliotawala kabla ya 1947
 
Basi mzee umeshashinda
 
Back
Top Bottom