Misri yamwachia mwandishi wa habari wa Al Jazeera baada ya miaka minne

Misri yamwachia mwandishi wa habari wa Al Jazeera baada ya miaka minne

Tatizo moja kubwa la third world ni kutothaminiana sisi kwa sisi.

Egypt wana bifu na Al Jazeera, wakaogopa kumkamata mtu wa Al Jazeera foreigner, wakamkwida mwandishi raia wao wenyewe.

Formula hii hii ndio ilitumika bifu la Tanzania, The Economist na Kabendera.
Mambo ya kipuuzi sana wanayofanya hawa makaburu wa kizazi hiki
 
Baada ya kukaa kizuizini kwa zaidi ya miaka minne, mwandishi wa habari wa Al Jazeera, Mahmoud Hussein ameachiwa siku ya Ijumaa.

Hussein, raia wa Misri, alikamatwa mwezi Disemba mwaka 2016 kwa tuhuma za kuandika habari za uwongo. Shirika la Habari la Al Jazeera lilifanya kampeni kila siku kutaka kuachiwa kwake, likidai kuwa mfanyakazi wake alishikiliwa kinyume cha sheria bila kufunguliwa mashtaka.

Shirika hilo halijatoa taarifa kuthibitishwa kuachiwa kwake, lakini ripoti ya Shirika la Habari la AFP imesema kuwa taarifa ya mwandishi huyo kuachiwa imethibitishwa na Mtandao wa Kiarabu wa Taarifa za Haki za Binadamu, ikiongeza kuwa mwandishi huyo hajarejea nyumbani.

Shirika la habari la Al Jazeera lilijikuta katikati ya mzozo wa kisiasa kati ya Cairo na Doha baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais wa zamani na kiongozi wa vuguvugu la Udugu wa Kiislamu anayeungwa mkono na Qatar, Mohammed Morsi, huku tovuti ya Al Jazeera ikizuiwa nchini Misri tangu mwaka 2017.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameulaumu utawala wa Rais Abdel Fattah al-Sisi kwa ukandamizaji wa haki za binadamu, ukijihusisha na kuwakamata maelfu ya wafuasi wa Morsi, wakiwamo waandishi wa habari, wanasiasa na wanamuziki.
Misri ilikuwa na ushirika pamoja na Saudia,UAE, Bahrain wakaiwekea Qatar vikwazo majuzi wameyamaliza nazani ndo kilichopelekea mwandishi kuachiwa
 
Back
Top Bottom