Miss Kenya V/S Miss Tanzania

Miss Kenya V/S Miss Tanzania

FirstLady1

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2009
Posts
16,789
Reaction score
5,401
JF niliangalia miss kenya na kwa aliyebahatika kuiona lol wenzetu kidogo naona wame advance na mabinti wanaconfidance sijawahi kuona

watoto wanajieleza kama hawana akili nzuri mengineyo yalikuwa makosa madogo madogo

Mbona warembo wetu wa Kitanzania upeo wa kujieleza ni mgumu sana???
 
nafikiri tatizo ni kukaririshwa vitu ambavyo havina tija mashuleni.
 
Na mi nawaombea wasiwe na uwezo wa kujieleza zaidi ya walio nao hivi sasa, manake tutashindwa kujiexpress nao kirahisi. Na bado hatujapata products za shule za Lowassa (Sekondari za kata), hapo ndipo tutazidi pata burdani nzuri zaidi.
 
JF niliangalia miss kenya na kwa aliyebahatika kuiona lol wenzetu kidogo naona wame advance na mabinti wanaconfidance sijawahi kuona

watoto wanajieleza kama hawana akili nzuri mengineyo yalikuwa makosa madogo madogo

Mbona warembo wetu wa Kitanzania upeo wa kujieleza ni mgumu sana???

Nilidhani kwako ingekuwa rahisi kulijua hili, hiyo sample ya hao unao waita wa tz hai wakilishi vizuri warembo wa ki tz, kutokana na maskendo na tamaduni zetu ambazo ziko strictly zadi ukilinganisha na kenya warembo wenye akili huwa hawashiriki miss Tanzania na hata wakishiriki hutolewa katika hatua za mwanzo kwani huwa ni wagumu kutoa rushwa za ngono na pia huwa wanamisimamo ambayo akina lundenga wanaiogopa, wanahoji zawadi, maisha ya kambi na hata huduma hivyo akina lundenga huamua kuwapiga chini na kuwaweka mambumbumbu wa yes uncle hasim kwenye kila kitu.
 
haaaa ahaaaa ahhha akili yako unaijuwa mwenyewe🙂
 
Kuna ukweli wowote kama TZ kuna rushwa ya ngono?? mmh
 
rushwa huwa iko nje nje (wazix2) ndo maana tunapata product hii first lady!!!!!!
Umeona ile gari ya zawadi? kweli ni ya thamani ya 52mil? wizi mtupu
 
Kuna ukweli wowote kama TZ kuna rushwa ya ngono?? mmh

Kuna dada aliwahi kuwa miss Tanzania anaitwa Faraja Kota, yeye ameandika kitabu nadhani kinaitwa Faraja ya Usichana(sina uhakika) ameeleza hayo kutokana na experience yake katika mashindano haya, nadhani unahitaji kukisoma pia kama una binti mdogo mnunulie kopi.
 
Hakuna cha kuuliza zaidi. Answer is YES!

KWA STYLE HII SITARUHUSU UZAO WANGU UENDE HUKO KUSHINDANA -THE REASON BEHIND

Inaumaaaaaa kwa nini watuharibie watoto wetu??. na watoto nao wanakubali bila hiana kisa wanataka gari la 50m mm
 
Kuna dada aliwahi kuwa miss Tanzania anaitwa Faraja Kota, yeye ameandika kitabu nadhani kinaitwa Faraja ya Usichana(sina uhakika) ameeleza hayo kutokana na experience yake katika mashindano haya, nadhani unahitaji kukisoma pia kama una binti mdogo mnunulie kopi.

ni lazima nipate kopi ya kitabu kwa faida ya familia yangu ni hatari sana
 
KWA STYLE HII SITARUHUSU UZAO WANGU UENDE HUKO KUSHINDANA -THE REASON BEHIND

Inaumaaaaaa kwa nini watuharibie watoto wetu??. na watoto nao wanakubali bila hiana kisa wanataka gari la 50m mm

Anza kukesha ukiomba darling. Watoto wa siku hizi hawashikiki. We utakataza yeye ataenda. Lakini si bora akajaribu bahati yake kwa kina Lundenga kuliko kulaghaiwa na kina Liyumba?
 
huna rafiki aliyewahi kuutafuta umiss umuulize yaliyomsibu?? Hupigi nao story? Jaribu kugombea utupe evidence

mie sitaki hata kujaribu kwanza sifa sina 🙂
 
Tatizo la wtz wameingia kwa rushwa ya ngono,ila firstlady unaonekana bomba sana mwakani ingia basi ulingoni ili tupate maevidensi,si unajua siku hizi simu zina video recorder?Natamani tumwone Lundenga akiitaka kweli hiyo rushwa ya ngono tumsulubishe!
 
THE ANSWER IS BIG YEEEESSS! Lundega mpaka kavunja ndoa yake na kuoa humohumo!
Wakishamaliza kushioriki kunakuwa na sherehe ya kuwapongeza! Hebu jipenyeze ukaone yanayoendelea baaday, ni SODOMA NA GOMORA!!
 
JF niliangalia miss kenya na kwa aliyebahatika kuiona lol wenzetu kidogo naona wame advance na mabinti wanaconfidance sijawahi kuona

watoto wanajieleza kama hawana akili nzuri mengineyo yalikuwa makosa madogo madogo

Mbona warembo wetu wa Kitanzania upeo wa kujieleza ni mgumu sana???

Mabinti wetu kukosa confidence kunatokana na tabia yetu ya uswahili tangu mitaani tunakokulia. Watanzania kwa jumla hatuna confidence na jambo lolote, ndiyo maana akija mtu mgeni tunatetemekea kama nini. Hebu angalia sasa hivi karibu nchi nzima imechukuliwa na wageni na wala hatusemi kitu. Viongozi wetu wanaiba halafu bado tunaandamana kuwapongeza. Kenya hawana ujinga wa namna hiyo, ndiyo maana hata walipoibiwa kura walipigana, sisi tunanyamanza na kusema huo ndio uzalendo. Waziri wa Kenya aliyekula rushwa alivuliwa madaraka papo kwa papo, juzi tumesikia uteuzi wa kijinga uliofanywa na Rais Bunge likakataa papo kwa papo. Mambo hayo hayawezi kutokea Tanzania. Tunajua kabisa kuwa mfanyakazi wa serikali anaiba pesa za serikali lakini ama tunamsifia au tunamwonea wivu.
 
Back
Top Bottom