Mabinti wetu kukosa confidence kunatokana na tabia yetu ya uswahili tangu mitaani tunakokulia. Watanzania kwa jumla hatuna confidence na jambo lolote, ndiyo maana akija mtu mgeni tunatetemekea kama nini. Hebu angalia sasa hivi karibu nchi nzima imechukuliwa na wageni na wala hatusemi kitu. Viongozi wetu wanaiba halafu bado tunaandamana kuwapongeza. Kenya hawana ujinga wa namna hiyo, ndiyo maana hata walipoibiwa kura walipigana, sisi tunanyamanza na kusema huo ndio uzalendo. Waziri wa Kenya aliyekula rushwa alivuliwa madaraka papo kwa papo, juzi tumesikia uteuzi wa kijinga uliofanywa na Rais Bunge likakataa papo kwa papo. Mambo hayo hayawezi kutokea Tanzania. Tunajua kabisa kuwa mfanyakazi wa serikali anaiba pesa za serikali lakini ama tunamsifia au tunamwonea wivu.