Miss Tanzania 2018: Mimi ni Mlokole, nampenda Yesu Kristo

Miss Tanzania 2018: Mimi ni Mlokole, nampenda Yesu Kristo

Basi kupitia magotini pa bwana na atashinda miss world
aisee! Nadhani Bwana ana kipimo cha mwombaji ndipo huamua ampe yupi. Timu mbili zinaenda kwenye mechi halafu zote zinaomba ushindi kutoka kwa bwana sasa moja ikishinda hiyo ina maana gani imeomba zaidi au na je ikiwa sare maana maombi yamebalance au?
sasa wewe umesema tena mtindo ni huo huo hadi kombe la dunia, umenifikirisha sana!
 
View attachment 869985
Ameyasema hayo wakati akihojiwa na EATV. Kasema kila shindano alikuwa anashinda, na siri ya Ushindi ni Maomba ya Baba mchungaji wake wa Kiroho.

"Mimi naishi magotini mwa bwana".

Baada ya mashindano ya Miss Tanzania kukamilika na Queen Elizabeth Makune kuibuka mshindi wa taji hilo kwa mwaka 2018, wazazi wake wameibuka na kusema kwamba mtoto wao ameokoka na anamtumikia Mungu.

Akiongea kupitia eNewz mama wa mrembo huyo amesema kwamba mtoto wake amekuwa akipenda sana kuvaa ‘crown’ tangu akiwa mdogo, kwani hata wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa alikuwa anapenda kununuliwa keki ambayo ina ‘crown’ juu.

Hata hivyo mama Queen Elizabeth ameendelea kusema kwamba “Queen ni mtoto wa kanisa hata kabla hajawa ‘star’, alikuwa anakaa mlangoni kanisani kwa ajili ya kupokea na hata alipokuwa anachukua mataji mbalimbali kabla la Miss Tanzania alikuwa akienda kanisani na kuomba aombewe ili kuweza kufika mbali zaidi”

Kwa upande wake, Miss Tanzania Queen Elizabeth Makune amesema anajisikia furaha kupata nafasi hiyo na kudai atahakikisha kupambana na kuipigania Tanzania zaidi ya Miss Tanzania 2016/2018 Diana alivyokuwa
Point ya msingi ni nini? kwamba kashinda kutokana na maombi? kashinda kwa vile tangu mdogo anapenda kuvaa crown? kwamba kashinda umiss ila asihusishwe na mambo ya kihuni yatokanayo na umiss kwa vile yeye n mlokole? kwamba kashinda so watu wasimsumbue sumbue kutaka kumkita binti kaokoka?
 
Muda ni hakimu mzuri sana,ngoja kina Diamond waanze kumapproch tuone kama ataruka na ulokole wake...
 
kwa nini mfano wa miss Tanzania awe Nyumbu Wema tu...wakati Nancy record yake ya miss world namba 3 haijavunjwa mpaka Leo...
 
kwa nini mfano wa miss Tanzania awe Nyumbu Wema tu...wakati Irene Kiwia record yake ya miss world namba 3 haijavunjwa mpaka Leo...

Namba 3? Labda namba tatu ya kiatu!!.. Hakuna mbongo aliyewahi kutoka hata namba 10 wote wanaendaga kutingisha vikalio vyao vikavu huko na kurudi.. hata hicho kizushi nacho kitaishia hukohuko
 
Hata Queen Elizabeth mwenzake wa Uingereza ni mlokolole pia.
 
Back
Top Bottom