SI KWELI Mistari hii kwenye alama hii inamaanisha kila mstari ni mita 100

SI KWELI Mistari hii kwenye alama hii inamaanisha kila mstari ni mita 100

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na video ambayo inasambaa kwenye mitandao wa facebook pamoja tiktok ikielezea kuhusu matumizi ya alama yenye nembo 50 na matumzi yake katika barabara.

Kwa kutumia ufuatiliaji kupitia account rasmi ya RAS Tanzania (Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani Tanzania (Tanzani Road Safety Ambassadors) inaelezea kuwa ni kwamba hapo ni miwsho wa spidi 50 kutoka hapo dereva anatakiwa kuongeza mwendo kadiri atakavyohitaji

1768377191125.png
 
Tunachokijua
Alama za barabarani zinasaidia kutoa tahadhari, kurekebisha, kuongoza
na kuwapa taarifa watumiaji wa barabara. Zinajumuisha ishara za barabarani kwenye nguzo za wima, taa za barabarani, na michoro ya barabarani. Kuna makundi manne ya alama za barabarani:​
  • Alama za udhibiti kuwaambia madereva kipi wafanye na kipi wasifanye
  • Alama za tahadhari kuwatahadharisha madereva juu ya hatari au matatizo ya barabara mbele
  • Alama za taarifa kuwasaidia madereva kuangalia huduma namaeneo wanayoyataka
  • Alama za mwongozo kuwasaidia madereva kuona njia za wanakokwenda
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa TikTok amechapisha kipande cha video akieleza maana ya moja kati ya alama za barabarani iliyo katika muundo wa duara katikati ikiwa na namba iliyopitiwa na mistari ya mshazari na kueleza kuwa kila mstari mmoja ni sawa na mita 100. Hivyo Dereva anapaswa kufuata maelekezo ya kibao hicho baada ya umbali sawa na idadi ya mistari hiyo.

Je uhalisia ni upi?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa video hiyo inapotosha uhalisia. Mkufunzi Venance Zakaria Banda kutoka Ikwiriri Folk Development college anafafanua kuwa alama hiyo inamaanisha kukoma kwa amri ya kiwango cha mwendokasi iliyokuwapo awali.​


screenshot-2026-01-14-140042-png.3529740

screenshot-2026-01-14-140107-png.3529742
Maelezo zaidi kuhusiana na matumizi ya alama za barabarani
 

Attachments

  • ufafanuzi.mp4
    9.1 MB
Hawa walugaluga wa mikoani washamba sana
Wanavamia kila kitu ili waonekane kwenye mitandao
 
Back
Top Bottom