Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Aahh!! Zingifuli zingifuli zinga mahala ukakaaa,
Usoo mila desituri usiyejua tongozwa ukakataaa,
Usio hiana fedhuri uongo umekujaaa,
Kujifanya mashuhuri kumbe chaka umechakaa,
Aagah!! Mwanzako mim turufu si garasa,
Mwenye nyota ya umaarufu si kupapasa.
=> Nimekaa nikautafari huu ubeti wa pili mawazo yakanijia kuwa alikuwa anampiga dongo madame Wema hasa baada ya Diamond Kummwaga...
Naeleza kama ifuatavyo...
Usoo mila desituri usiyejua tongozwa ukakataaa,
Usio hiana fedhuri uongo umekujaaa,
Kujifanya mashuhuri kumbe chaka umechakaa,
Aagah!! Mwanzako mim turufu si garasa,
Mwenye nyota ya umaarufu si kupapasa.
=> Nimekaa nikautafari huu ubeti wa pili mawazo yakanijia kuwa alikuwa anampiga dongo madame Wema hasa baada ya Diamond Kummwaga...
Naeleza kama ifuatavyo...
1. Aahh!! Zingifuli zingifuli zinga mahala ukakaaa,
Hapa anamwambia angetafuta mwanaume mmoja akakaa akatulia nae.
2. Usoo mila desituri usiyejua tongozwa ukakataaa
Anamwambia wema hajui mila na desturi,kila mwanaume anayemtongoza anampata. Hapa tunaona msululu wa wanaume ambao washawahi kutoka na wema kuanzia kwa Mr. Blu mpaka Mzee wa BMW pedeshee Mkongo.
3. Usio hiana fedhuri uongo umekujaaa
Hapa anamaanisha madame hana hiana fedhuri na Muongo. Hili sihitaji kulielezea kwa undani zaidi kila mmoja anajua.
4. Kujifanya mashuhuri kumbe chaka umechakaa
Hapa madame anajifanya maarufu kumbe ndani amechakaa chaka chaka kwa sababu ya tabia zake.
5. Aagah!! Mwanzako mim turufu si garasa 6.Mwenye nyota ya umaarufu si kupapasa
Namba sita na tano, Diamond anajisifia kuwa yeye ni maarufu hata kama asingekuwa na Wema. Anapendwa na mashabiki wala hakutumia ndumba.
Naam naomba tulijadili hili suala.Samahani kwa #TeamZingifuli kama ntakuwa nimewa-offend.
Moja ya sifa ya sanaa ni kuelimisha,kuburudisha na kukanya katika jamii.