Mistari ya kujiliwaza na Maisha

Mistari ya kujiliwaza na Maisha

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,291
Najikuta nimekaa naota
Naota nina guta nachoka
nakurupuka kumekucha hapa hopa,
Ajira baba ajira, umesepa.


Nielekee wapi ,hapa nachoka
Natamani kuruka, tumbo linawaka
Hapana nitabaki hapa hapa,mwasika.
Ajira baba, ajira imesepa.

Twenzetu msera, pita majalala.
Anzia ufipa, kinyerezi hadi goba
Okota mizoga, makopo na machupa
Ajira baba, ajira imesepa.

Weka lumbaso hadi hopa kichupa
Wataweseka, zangu zinapita, nikichoka nauchapa
mzigo weka kichwa hadi bega, jasho linatoka.
Ajira baba, ajira imesepa.

Nifanyeje naogopa jela na machela.
Bisimisi, visu, mapanga na bakora,
Navuja jasho mwenyewe bora mpera mpera ,sitaki masighara.
Ajira baba, ajira imesepa.
 
Back
Top Bottom