Misumari, malighafi kwa ajili ya SGR ya Tanzania vitatoka Uturuki, halafu wanaicheka Kenya



Hii sasa inaitwa kuosha kinywa, huna hata aibu unaongea kumbe hujui chochote.









Eti hamna hata time frame ?

Designer : COWI & SENER
Consultant: KORAIL JV KOREA RAIL ROAD
Completion date:07/11/2019








 
Hajakosoa, ameuliza maswali muhimu sana yanayohitaji majibu, amekosa majibu hata kutoka kwa wizara zote husika, sasa nyie hapa JF huwa mpo kwenye automated gear, mnajibu hoja zake kwa kumshambulia bila hata kusoma anachokiuliza.
Hayo maswali yake ni mazuri, shida ni sehemu alipoyaulizia. Angeyauliza bungeni angepata majibu hapo hapo na ingetusaidia hata sisi watanzania kujua baadhi ya vitu. Hilo hakulifanya anaongelea kwenye press conference. Kwa utaratibu huo kweli atapata majibu?

Wewe ukijiuliza hayo maswali kwa nini hakuyauliza bungeni utapata jibu gani?
 
Hivi mbona huwa mnajitoa ufahamu kwa ushabiki na kugoma kumuelewa Zitto, jamaa hata huwa mnamkamata kamata badala ya kujibu hoja zake.
Hapa hajapinga mradi, ameuliza maswali ya msingi sana, na badala ya nyie kumjibu mnapambana kumjadili......
Kitendo cha serikali kupitia jeshi la polisi kuwakamata hawa wapinzani kinapingwa na watanzania walio wengi, sisi sote tunalipigia kelele hilo, lakini hata Zitto anapokuwa anafanya mambo ya hovyo ni lazima pia tumkemee, kwa mfano anadail tutmie chuma cha Lidanga badala ya kuagiza chuma toka nje, Liganga ni sehemu chuma kimegunduliwa, ni mlima mkubwa porini, serikali ipo mbioni kuchimba hicho chuma, ipo katika hatua za mwanzo hata pesa ya kuchimbia haijapata, ni sawa na mafuta ya Kenya ambayo bado yapo ardhini, hivi utamuelewa mtu anayesema kwanini Kenya inanunua mafuta toka nje wakati kuna mafuta huko Turkana?.

Reli hii ndiyo inayotegemewa kusafirisha hicho chuma cha Liganga ili kifike Bagamoyo kisafirishwe nje, kwa maana hiyo inabidi SGR imalizike haraka ili chuma kiweze kusafirishwa, sasa itakuwaje chuma kilichopo ardhini kitegemewe kujengea reli ambayo ujenzi wake unaendelea?, Zitto alikuwa enzi za Kikwete anajenga hoja nzuri kwa sababu serikali ya Kikwete ilikuwa na mapungufu mengi sana, ilikuwa rahisi kuichallenge, sasa hivu karibu madhahifu mengi sana, hasa upande wa uchumi na maendeleo Magufuli anafanya vizuri sana, wapinzani hawana hoja.

Mimi kitu kinachonishangaza kwenye huu upinzani wa Tanzania ni jambo moja, ikiwa wao wenyewe wanashindwa kujitetea, watawezaje kuwatetea wananchi?, ni ukweli kwamba Magufuli amekiuka katiba kwa kukataza mikutano ya vyama vya siasa na maandamano, kwanini wanashindwa kwenda kulipinga hili jambo muhimu kwa ustawi wa siasa za Tanzania, badala yake wanakimbilia kushabikia kukamatwa Bombadier na kusema taarifa za kukua uchumi sio za kweli, hayo yana umuhimu gani kwao zaidi ya hilo la kubanwa na Magufuli?.. Wanahitaji maombi hawa akina Zitto
 
Zitto ni mtu aliyekengeuka ambaye hata cku moja usitegemee atatoa hoja yenye kuonyesha upeo wa jambo kutatulika badala yake ni mtu wa Aina ya kutoa hoja zikwepazo majibu ya moja kwa moja Yaani ataongea hili akiona linakaribia kutatulika ataibua lingine akiona nalo linaanza kuwezekana atarukia lingine nk kwanza alisema uwezekano wa kujengwa reli haupo ameona kazi zimeanza anatafuta flaws ambazo hazijulikani kuna kampuni kibao za ndani ambazo zmekula shavu mfano kuna kampuni ya Becco Ltd ambayo ndio inachonga barabara na kutengeneza tuta pia kuna viwanda vya nondo na cement vya hapa ambavyo vimekula shavu kuleta materials wakat kiwanda cha soga cha concrete sleepers kikianza kufanya kazi sasa anachoongea ni kipi
 

Maswali yake yote ni muhimu sana, japo kama ilivyo kawaida yenu mpo kikazi huku kwenye mitandao, mumeishia kumshambulia yeye binafsi. Amesema mkataba hauna kifungu cha kufungamanisha na sekta nyingine, imekaa ovyo sana hiyo na haijalishi mtapindisha pindisha kivipi kwenye mitandao, uhalisia bado utaonekana wenye kunuka.

Hata hivyo nakubaliana na wewe kwenye issue moja tu, kwamba alifaa kuuliza hayo maswali bungeni kama hoja ili ashinikize majibu. Sasa yeye kama ilivyo wapinzani hata wa huku kwetu ametafuta kiki kwenye press conference, ndivyo tulivyowazoea wapinzani hapa, hawaulizi bungeni, wataita wana habari na kutoa matamko ambayo hayajathibitishwa na huwa inabidi wajibiwe kwenye magazeti, wakati maswali yakiulizwa bungeni, serikali inalazimka kutoa majibu yaliyotuia.
 
Hoja muflisi. Ni defence mechanism ya mkosa hoja
 
Hapo kwenye aya ya pili ndo kuna mzizi wote wa hoja hii. Huu ndio huwa ni udhaifu wa baadhi ya wanasiasa hasa hawa wa kiafrika. Hivi inakuwaje mtu ambaye ni mbunge kushindwa kutumia haki yake ya kibunge kuuuliza hoja nzito kama ile bungeni?


Kuhusu kumshambulia zito kwenye mitandao, japo wengine halituhusu, lakini ni kwa sababu njia aliyoitumia kufikisha ujumbe wake sio muafaka. Lakini pia sio wote wanaomshambulia, kuna wanaomuunga mkono. Pengine ni suala la mtazamo juu ya hoja yake.

Lakini yote hayo yanakuja kutokana na mambo yake. nimekupa mfano wa mambo ambayo alishawaahidi watanzania na akashindwa kuyatekeleza. Hilo lilisababisha aondolewe imani kwenye mambo anayosema bila ushahidi.
 
Kama ni kweli basi serikali wamebugi sana.
Ila it is hard to believe huyo mtoa hoja (ZZK).
 
Nivizuri kumjibu
lakini sio kila kichaa lazima ajibiwe
 
Wakenya hatua hizi zinazochukuliwa na nchi ya Tanzania katika kukuza uchumi ni lazima roho ziwaume sana. Kenya ni miongoni mwa nchi ambazo zilikuwa zinatuibia mali zetu. Mfano madini ya Tanzanite, mbunga zetu za wanyama, kuutangaza mlima Kilimanjaro hata ardhi yetu wanaionea wivu maana huko kwao ni jangwa hasa sehemu za kasikazini.. Juzi tu tumewanyang'anya mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda. Hivyo, kwa sasa wakenya hawawezi kuisema vizuri Tanzania.
 
Boss hii nchi inaenda ilimradi kuna kucha! Mkuu wetu wa serikali ubongo wake uko na shida kubwa sana...






Hao wanaodiss bila ushahidi thabiti ndio hao hao wanaomtetea Baba Ubaya kila ujinga aufanyao so isikushangaze buda
 
Zitto sio Mkenya wewe, acha kutuaibisha...hoja za Zitto zimekuwa NZITO hadi tunatafuta Wakenya wa kuwalaumu.
 
Duh hatari!!!!!! sana naona wegi hamjamuelewa Zito, wtzania walio wegi hatujui macro economics au micro economics hata fiscal policy hatuzielewi kabisa tumejaa siasa na ushabiki wa vyama kuenda mbele hatuwezi kufanya uchambuzi wa economic issues hata kame wegi tulisoma comb HKL HGL basi tu some vitabu tuongeze maarifa tuwe na upeo wakuelewa na kuchangia mambo mengine ya kitaifa........7trion kunjenga reli kwa kutumia kampuni za kigeni na mari ghafi za kigeni inakua "capital fright" ni hatari kwa unchumu we ndani na thamani ya shilling viza vie dollor ineleta economic stagnation kwa mda huo.....
 

Madini ya Tanzanite, Kenya na hoja ya Zitto wapi na wapi, mkilipwa kutetea serikali kwenye figisu zake muwe mnashirikisha na ubongo pia, sio kuandika andika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…