Mita ya Kupima Mafuta Kurasini Oil Jetty Kutoka Melini ni Hujuma Tupu

Mita ya Kupima Mafuta Kurasini Oil Jetty Kutoka Melini ni Hujuma Tupu

VunjaMfupa

Senior Member
Joined
Feb 7, 2014
Posts
122
Reaction score
78
Mita za Kurasini Oil Jetty


"......
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), aliliambia Bunge mwishoni mwa wiki kuwa pamoja na TRA kufikia malengo kwenye makusanyo ya kodi katika mwaka wa fedha wa 2011/12, bado kumekuwapo na udanganyifu na mianya ya ukwepaji wa kulipa kodi katika maeneo kadhaa.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni kusitishwa kwa matumizi ya mita za kupima ujazo wa mafuta yanayoingia nchini kupitia kituo cha kupakulia mafuta cha Kurasini, jijini Dar es Salaam.

Alisema kamati yake imeitaka Serikali kulieleza Bunge sababu za msingi za kusitisha matumizi ya mita hizo na TRA kuainisha athari katika ukusanyaji wa mapato itokanayo na kusitishwa kwa matumizi ya mita hizo.

Alisema mpaka sasa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) baada ya kusitishwa kwa matumizi ya mita hizo inatumia vijiti vya kupimia ambavyo vipimo huchukuliwa wakati mafuta yako kwenye meli na baada ya kuwekwa kwenye matangi ya wafanyabiashara walioyaingiza mafuta hayo.

Alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika taarifa yake ya 2010/11 alihoji kuhusu sababu za kusitisha matumizi ya mita kupima ujazo wa mafuta katika bandari za Tanga na Dar es Salaam na hivyo kusababisha hasara kwa Serikali kwa kufanya manunuzi yasiyo na tija.

Alifafanua kuwa kamati yake iliwahoji maofisa masuuli wa TPA aliyeeleza kuwa mita hizo zilinunuliwa mwaka 2004 na TPA na kufungwa katika kituo cha kupakulia mafuta cha Kurasini (KOJ) mwaka 2004 na kuanza kutumia mwaka 2005 kwa lengo la kupima kiwango cha mafuta yanayoingizwa nchini kupitia Bandari za Tanga na Dar es Salaam.

Hata hivyo, alisema ilipofika Februari 2011, Wakala wa Vipimo nchini (WMA), iliyoridhia awali matumizi ya mita hizo, iliwaandikia TPA kusitisha matumizi ya mita hizo kwa sababu zimethibitika kutoa vipimo visivyo sahihi hivyo kusababisha walipa kodi kulalamika.

Zitto alisema wakati TPA ikisema mita hizo hazina matatizo yo yote na zinaweza kuendelea kutumika, WMA wanasisitiza kuwa mita hizo hazitoi vipimo sahihi vya ujazo wa mafuta na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa TRA na wafanyabiashara ambao wamekuwa wakilipa kodi kubwa kutokana na vipimo visivyo sahihi vya ujazo wa mafuta vinavyosomwa na mita hizo.

Hata hivyo, alisema TRA walishindwa kuieleza Kamati jinsi ambavyo usitishaji wa matumizi ya mita hizo umeathiri upatikanaji wa mapato yatokanayo na kodi ya kuingiza mafuta nchini......"


Source: Home

My take: Wenye uchungu na Jambo hili naomba maswali zaidi ili niwape ukweli wa mchezo wenyewe ulivyokuwa.
karibuni

Cc Zitto kabwe
CC @Mwingulu Nchemba
 
Nasikitika 43 people viewed lakini ....... No comments.......
 
Endelea na part II ya story maana amekulipa uiweke tena hii kazi aliyoifanya mwezi january .si vibaya kusema unachojuam
 
Kila mtu anawaza jinsi ya kukwepa kodi.
 
Hii Nchi itakuwa hivi mpaka lini?kwani nchi ni ya Viongozi au Wananchi
 
Back
Top Bottom