A
Anonymous
Guest
Huku mtaani kwetu Kata ya Daraja Mbili pande za Arusha tuna changamoto ya uhalifu, yaani imefikia hatua hata Ulinzi Shirikishi wenyewe ambao wanajuliakana pia kwa jina la Sungudungu nao wanaogopa kulinda.
Inapofikia hatua ukaona hata Sungusungu wenyewe wamesanda ujue hapo mambo si mambo.
Kuna matukio kadhaa ya watu kupoteza maisha katika mzingira ambayo hata sisi wenyeji hatuyaelewi.
Serikali ije itusaidie huku, mambo si mambo la sivyo tujajikuta tunahama Mkoa.
===========
DIWANI AKIRI KUWA HALI NI MBAYA
JamiiForums imewasiliana na Diwani wa Kata ya Daraja Mbili, Prosper Msofe ambaye amekiri uwepo wa changamoto hiyo kwa kusema:
Ni kweli kuna changamoto kubwa sana ya uhalifu kiasi kwamba hii ni kama sio sehemu ya Tanzania tunayoijua na sababu kubwa ni kutokana na umasikini wa kiwango cha juu uliopo katika Kata hii.
Kwanza kuna unywaji na uuzwaji wa Pombe nyingi za kienyeji, wakazi wengi wa huku hasa vijana hawana ajira na wanategemea wapate fedha wakalewe, hivyo hali hiyo inachangia ongezeko la uhalifu wa mara kwa mara.
Neweza kusema mimi ndiye Diwani ambaye nina Kata yenye uhalifu mwingi kuliko wote Tanzania, hata leo hii nazungumza na wewe muda huu (Mei 27, 2024) kuna kijana ambaye ameuawa na tupo msibani.
Pia pembeni yangu kna vijana wanakunye pombe na bado ni asubuhi unaweza kupata picha mazingira yalivyo.
Nimeshatoa taarifa mara kadhaa Jeshi la Polisi lakini hakuna msaada wa kutosha, kuna wakati Polisi waliahidi kuweka Askari kila mtaa kulinda na kuzuia changamoto za uhalifu, lakini badala yake hao Askari wawaka wanapita tu kisha wanaondoka.
Hakuna msaada wa Jeshi la Polisi wa uhakika, nimemfikishia RPC taarifa lakini sijapata mrejesho, hata kuhusu mauaji haya yanayoendelea nimeshamfikishia taarifa kwa njia ya ujumbe wa SMS hajanijibu na nikapiga simu haikupokelewa.
Huku kwetu uuzwaji wa bangi unafanyika hadharani, hata Wananchi ambao wanatakiwa kujitokeza kulinda usiku kama Sungusungu nao hawalindi kwa kuwa wanahofia usalama wao, matokeo yake wanaochaguliwa kulinda ni Wahalifu pia.
Naomba ujumbe huu umfikie Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Rais Samia, watusaidie Kata ya Daraja Mbili, hali ni mbaya katika suala la usalama.