DOKEZO Mitaa ya Daraja Mbili - Arusha kuna uhalifu kiasi kwamba hata Sungusungu nao wanaogopa kulinda

DOKEZO Mitaa ya Daraja Mbili - Arusha kuna uhalifu kiasi kwamba hata Sungusungu nao wanaogopa kulinda

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Arusha wanalea upumbavu saaana, matokeo yake ndo hiyoo wanalipa gharama ya upumbaf wanaoulea
 
Huku mtaani kwetu Kata ya Daraja Mbili pande za Arusha tuna changamoto ya uhalifu, yaani imefikia hatua hata Ulinzi Shirikishi wenyewe ambao wanajuliakana pia kwa jina la Sungudungu nao wanaogopa kulinda.

Inapofikia hatua ukaona hata Sungusungu wenyewe wamesanda ujue hapo mambo si mambo.

Kuna matukio kadhaa ya watu kupoteza maisha katika mzingira ambayo hata sisi wenyeji hatuyaelewi.

Serikali ije itusaidie huku, mambo si mambo la sivyo tujajikuta tunahama Mkoa.


===========


DIWANI AKIRI KUWA HALI NI MBAYA
JamiiForums imewasiliana na Diwani wa Kata ya Daraja Mbili, Prosper Msofe ambaye amekiri uwepo wa changamoto hiyo kwa kusema:

Ni kweli kuna changamoto kubwa sana ya uhalifu kiasi kwamba hii ni kama sio sehemu ya Tanzania tunayoijua na sababu kubwa ni kutokana na umasikini wa kiwango cha juu uliopo katika Kata hii.

Kwanza kuna unywaji na uuzwaji wa Pombe nyingi za kienyeji, wakazi wengi wa huku hasa vijana hawana ajira na wanategemea wapate fedha wakalewe, hivyo hali hiyo inachangia ongezeko la uhalifu wa mara kwa mara.

Neweza kusema mimi ndiye Diwani ambaye nina Kata yenye uhalifu mwingi kuliko wote Tanzania, hata leo hii nazungumza na wewe muda huu (Mei 27, 2024) kuna kijana ambaye ameuawa na tupo msibani.

Pia pembeni yangu kna vijana wanakunye pombe na bado ni asubuhi unaweza kupata picha mazingira yalivyo.

Nimeshatoa taarifa mara kadhaa Jeshi la Polisi lakini hakuna msaada wa kutosha, kuna wakati Polisi waliahidi kuweka Askari kila mtaa kulinda na kuzuia changamoto za uhalifu, lakini badala yake hao Askari wawaka wanapita tu kisha wanaondoka.

Hakuna msaada wa Jeshi la Polisi wa uhakika, nimemfikishia RPC taarifa lakini sijapata mrejesho, hata kuhusu mauaji haya yanayoendelea nimeshamfikishia taarifa kwa njia ya ujumbe wa SMS hajanijibu na nikapiga simu haikupokelewa.

Huku kwetu uuzwaji wa bangi unafanyika hadharani, hata Wananchi ambao wanatakiwa kujitokeza kulinda usiku kama Sungusungu nao hawalindi kwa kuwa wanahofia usalama wao, matokeo yake wanaochaguliwa kulinda ni Wahalifu pia.

Naomba ujumbe huu umfikie Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Rais Samia, watusaidie Kata ya Daraja Mbili, hali ni mbaya katika suala la usalama.
Hiyo daraja mbili ni kaeneo ka uhalifu wa kutisha tangu tanganganyika iumbwe, hata ikitokea kuna wababe wanataka kuitawala nchi upande mmoja naona itaanzia hapo, polisi wenyewe wanaogopa, wakipita ni wanapita juu ya madifenda hawathubutu kushuka chini wafanya msako wa mbwa kwa mbwa.
Kwa sasa daraja mbili ndio eneo hatari kuishi hapa tanzania, hiyo ni south africa in tanzania.
 
Nimekulia daraja mbili mtaa wa Jaluo - Arusha, huko kuna wahuni wengi na wapumbavu
Kwelii umetoka wap? jirani na kwa kina chingoli(yule kaka yao mbafu nimemsahau jina ila ata yy sasa ivi saa 12 ndani na milango inafungwa kama gerezani)😂😂😂,ngoma za mashetani,kwa malai,chemchem,bongonyooo au wap home boi....m mzee wangu walimkaba na kumuumiza kichwani hapafai kwa kwelii.
 
Shida ya Daraja mbili ….wahalifu wanafahamika….wazazi/ndugu wanawaficha kwa kigezo cha watoto ama ndugu zao…ni ngumu sana kumaliza uhalifu uko…sababu wanaishi nao na wanawafichaa
Hiyo n fact moja wapo ila mambo yamebadilika ilikua ni wageni ndio wanakumbwa na hayo madhila tuuu ila sasa ivi mwenyeji ,mgeni wote shughuli moja.
Kama unaenda hayo maeneo nenda mchana kweupe tena pita katikati ya barabara.
 
Shida ya daraja mbili ni jiografia yake

Ina vichochoro vingi ,migomba na miti ...mbaya zaidi inaungana na unga ltd asee ni hatari sana

Kipindi cha magu uhalifu ulipungua sana hayo maeneo lkn sasa hivi uhalifu umerudi kwa nguvu kupindukia yaani hata maeneo ambayo hayakuwa na uhalifu wa kutisha kama Usa napo pameanza kuwa na matukio

Sehemu ambazo zinaufadhali atleast ngaramtoni haina rate kubwa
 
Kwelii umetoka wap? jirani na kwa kina chingoli(yule kaka yao mbafu nimemsahau jina ila ata yy sasa ivi saa 12 ndani na milango inafungwa kama gerezani)😂😂😂,ngoma za mashetani,kwa malai,chemchem,bongonyooo au wap home boi....m mzee wangu walimkaba na kumuumiza kichwani hapafai kwa kwelii.
Mtaa wa Jaluo hapo bongonyoo nakumbuka kulikuwa na ukuta umeandikwa hvy ila badae badae pakajengwa nyumba.
Mm nilikuwa nakaa njia ya kwenda chemchem.
Kuna mama maarufu hapo anaitwa Mama Musa alikuwa anawauzia vijana bangi.

Lamomy
 
Acha uongo!! Avatar yako tyuu inaonyesha bado mjani upo kichwani.!! 🤣🤣🤣
Dah umenikumbusha kuna kipindi nilikuwa nafahamika humu JF kwa mada za kupiga punyeto, sasa nikaja kuandika mada ya kuomba kazi sasa kuna mtu akarepy ety anaogopa kunipa kazi mana naweza kupiga nyeto kwenye vikombe vya chai vya ofisini 😂
 
Back
Top Bottom