Mnaposema "Panya Road" ni wahalifu wenye mapanga na silaha zingine za jadi kuwa wamekuwa wahalifu kwa sababu ya "Mitaala" mibovu basi mnamaana wananchi wote wanaosoma katika shule za Serikali ni 'Wahalifu' Kuwa wanachosomea huko ni kubeba silaha na kujifunza uhalifu-yaani matusi makubwa haya kwaJamii, wanafunzi, walimu, Serikali na Wananchi wake- isitoshe Mwafrika.
Hii imekaaje? Mitaala mibovu ya Elimu ndio inazalisha wahalifu?
Hii research ilifanywa wapi??
Wazungu na wawekezaji uchwara hapa nchini ndio Panya kabisa. Kila kukicha ni kutafuta njia za kutuhadaa na kutuibia kwa njia za chini chini, kwa panya road.
Hayo maadili na misamiati ya wazungu msituletee Tanzania yetu.