Mitaala ya shule ifundishe maisha halisi Ili kumfanya mwanafunzi kuyamudu maisha pindi arudipo mtaani

Mitaala ya shule ifundishe maisha halisi Ili kumfanya mwanafunzi kuyamudu maisha pindi arudipo mtaani

Imkisokiso

New Member
Joined
May 15, 2022
Posts
3
Reaction score
1
Ni wazo langu kwamba Serikali iangalie mitaala yetu Ili kuwafundisha WATOTO maisha halisi Ili warudipo mtaani wasihangaike kutafuta ajira.

Kwa mfano masomo ambayo yamechukua nafasi ya SoMo la sayansikimu ya miaka ya tisini kwa sasa ni butu kabisa kwa sababu WATOTO hawajui hata kufua na kupasi wenyewe.

Kuwe na masomo ya kilimo na ufugaji halisi Ili WATOTO wajifunze kwa vitendo mambo hayo, mambo ya ufundi stadi mbalimbali yafundishwe kianzia mwanzo kabisa Ili kuwajenga WATOTO wangali wadogo ni msingi mzuri kabla ya kwenda vyuo.

Nadhani tukifanya haya na mengine tutaepuka wimbi Hili la kukosa ajira Kila Kona.
 
Kufundisha watoto mambo ya Kimweri sijui Zwagendaba alikufa lini ni upuuzi.
 
Ni rahisi kusema elimu yetu iwe inafundisha vitendo, wenzio tunataabika watoto wetu wajue kusoma, kuandika na kuhesabu kwanza, hayo unayoyataka wewe watajifunza technical colleges
 
Kwahiyo unataka watoto wafundishwe kufua na kupasi shuleni? Huu ni upupu wa kiwango cha lami nausikia for the first time.

Tatizo hamtaki kufanya majukumu yenu nyumbani mnataka walimu shuleni wawafanyie kila kitu.

Mambo mengi mnayotaka yafundishwe shuleni ni jukumu la walezi nyumbani sio shuleni japo mitaala nayo inabidi ifanyiwe marekebisho kuendana na wakati ila sio upuuuzi wa kufundisha watoto kupasi shuleni, kupasi kutamsaidia nini?
 
Unafikiri maisha halisi kama unavosema yanafanana kote?

Maisha ya dar wanafunzi kuning'inia kwenye daladala ni tofauti na inyonga ambapo wanafunzi wengi wanaona kuchunga ng'ombe kuna faida kuliko shule.

In short tunatakiwa tuwe na mitaala zaidi ya 120....kulingana na mawazo yako. Its impossible
 
Back
Top Bottom