Uchaguzi 2020 Mitaani hoja "CHADEMA imekufa" sijui MATAGA ya humu!

Kasimba G

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Posts
3,428
Reaction score
2,612
Wana jamvi wasalaam,

Huku mtaani kwetu ile hoja maarufu iliyodumu takribani miaka mitatu ya kuwa upinzani especially CHADEMA imekufa imejifia na wapambe wa hoja hiyo wameingia hofu.

CCM wanajua sana kula na vipofu, kwa muono wangu nahisi waliitangaza hoja wakijua bwana Fulani hupenda kuskia mambo anayoyapenda yeye, wakaanza kumlia hela na kupewa mavyeo na kila aina ya mavuno.

Sasa bwana Fulani naona kishaanza kuhisi utapeli wa watu wake, hata watu wake wa karibu saana vilevile, nadhani kilichobaki ni kubadili gia angani kama uchaguzi wa Serikali za mitaa. Lakini pia anawasiwasi maana tapeli ni tapeli tuu haaminiki.

Sasa waliodhaniwa wamekufa kumbe ndio wako hai kiukweli na waliodhaniwa wako hai kumbe wako ahera. Nonino wamekufa kabisa kabisa, Hata wanowashabikia wanajua hill, je polisi wataingilia mchezo? Kazi kwao.
 
aliyempa wazo la kuawanunua watu alimpa ushauri mbovu kabisa usio na tija ianatakiwa amtafute ili amrudishie pesa zake maana work done ziko to zero,huyu jamaa atakuja waelewa watz akiwa keshachelewa kabisa wateule wake wanampa habari hazipendazo ili wampige pesa cheki kama idea ya kuwanunua kina waitara,lijuakali sijui wao wameingiza bei gani.
 
Ni rahisi sana kufanya ngono kuliko kuuwa upinzani
 
CCM inakufa polepole tusubiri mpasuko mkubwa wiki ajayo ndani ya ccm.
ccm bila mwenge zindiko limekiukwa,mwaka huu awatoboi kwa maana akili za wat hazichafuliwa na moshi wa mwenge wtafanya maamuzi yenye tija kwa taifa
 
Tulivyokuwa wadogo kuna watu tulikuwa tunaambiwa ni wanyonya damu.

Tuanze kuwafundisha watoto wetu wa sasa kuwaona ccm kama wanyonya damu wa kizazi hiki cha Kikwete.
 
ndiyo maana wale walionunuliwa wanalazimishwa kulipa gharama . Angalia wa kina katambi wanavyotakiwa kuichafua chadema kwa maneno mazito . je walikuwa wapi kusema yote hayo .kwani tumesikia mengi wakisema kuhusu chadema , kwa lengo la kuichafua
  1. mbowe alilewa na kuanguka .
  2. chadema wanaungana na mabeberu .
  3. lissu ana chip mwilini ,
  4. chasema ni watekaji na walitaka kumuua lisu
Na mengineyo unaweza kujazia . huu ni wakati kambi ile ya kijani inakuja na hoja nyingi sana ,kwa kutumia walionunuliwa . wanalipa gharama .

kama chadema waliweza kuruka vihunzi hivi , basi wameshinda . hivi vingine ni muendelezo wa kukwama kwa kambi ile ya kijani .
 
Kwa akili yako unaona chadema ile ya kabla ya 2015 ipo huku mitaani?
mbona hata huku CCM hatuko wamoja?

moja ya mambo yatakayotuangusha CCM October hii ni hujuma za wenyewe kwa wenyewe!!
 
Humu pia..
Wanalia wakiandika.. ila hawawezi kubadilika.. kisirisiri uraiani.. kura wanaenda kumpa Magufuli 💯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…