Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,466
Tukipita ubungo tunaona kila mwenye nia ya kuwekeza kupitia Tanesco na serikali akijiwekea mitambo pale. Hii ilisababishwa na serikali yetu kufanya mikataba ya kitapeli ya kuvuna gasi kutoka kusini na kuisafirisha hadi Dar es salaam kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na mambo mengine mengi.
Nikiwa naongea na baadhi ya wataalamu wa maswala ya gasi haswa ya songo songo walisema kilichofanyika ni utapeli tu kujenga mabomba yale badala ya kufunga ile mitambo huko huko kwenye chanzo cha gasi. Gharama za kuisafirisha ile gasi kwa mabomba, kutengeneza miundo mbinu ile ingepungua sana kwa kuiweka ile mitambo kwenye chanzo. Mabomba yaliyotumika hayaendani na kinachosafirishwa. Walifikia kusema ni sawa na kutumia basi kwendea kazini.
Kwanini mitambo isingefungwa kwenye chanzo na umeme kuingia kwenye grid ya taifa? moja kwa moja?