diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
AWAMU ya kwanza ya mitambo ya Kampuni ya Kutengeneza Viatu ya Jeshi la Magereza imeshawasili nchini kutoka nchini Italia. Hayo yamebainishwa na Msemaji wa Jeshi la Magereza nchini, Amina Kavirondo alipozungumza na HabariLEO.
Kavirondo amesema makontena 15 kati ya 80 ya mitambo hiyo yaliwasili nchini mwisho wa mwezi uliopita na yameshafikishwa kwenye kiwanda hicho mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Amesema awamu ya pili itakuwa na kontena 23 na awamu ya tatu itakuwa na kontena 42, hivyo kufanya mzigo wote kuwa na jumla ya kontena 80.
Kuja kwa mitambo hiyo kutalifanya Jeshi la Magereza kupitia kampuni yake ya Karanga Leather Industries kuimarisha uwezo wake wa kujitegemea kutokana na uwezo litakaokuwa nao katika kuzalisha viatu vya kijeshi na viatu vya kiraia. Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Masoud Omari amesema mitambo hiyo haijafungwa kwa kuwa inasubiri awamu ya pili ya mitambo mingine ambayo iko njiani ili ifungwe kwa pamoja.
Kwa mujibu wa Omari, kampuni hiyo kwa sasa inazalisha buti za jeshi pekee lakini mitambo inayokuja itawapa fursa ya kuanza kutengeneza viatu vya kiraia vya wanawake, wanaume na watoto kuanzia Agosti mwaka huu endapo kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa