SoC02 Mitandao ya kijamii na usalama wako

SoC02 Mitandao ya kijamii na usalama wako

Stories of Change - 2022 Competition

fikirakali

Member
Joined
Sep 15, 2014
Posts
15
Reaction score
18
MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA MITANDAO YA KIJAMII
Mara nyingi tumekua tunatumia mitandao ya kijamii bila kujiuliza juu ya usalama wa taarifa zetu. Tumekuwa kama mateka katika mitandao hii ya kijamii kiasi cha kusahau kuwa kuna hali ambayo tunaruhusu taarifa zetu muhimu kuwafikia watu wasio sahihi.

Kwa pamoja tutakubaliana kuwa kuna faida nyingi sana zinazoweza kupatikana kama tutaitumia vyema mitandao ya kijamii, faida hizo zinaweza zikawa elimu, biashara au burudani. Katika elimu mtu anaweza kujielimisha kwa kupata elimu ya kidunia au hata ya kidini. Watu wengi wameingeiza kipato kwa kukuza biashara na brandi zao. Mtandao wa Facebook ambao unakadiriwa kuwa na watumuaji zaidi ya bilioni mbili kwa siku ni eneo au uwanja tosha kama ukitumiwa vizuri kujitangaza na kutangaza bidhaa mbalimbali. Inashauriwa kufungua ukurasa wa bishara badala ya kutumi ukurasa wako binafsi, hii itakusaidia kufanya mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuweza kufanya uchambuzi wa mtiririko wa watu katika ukurasa, kujua ni watu wa umri gani wanapenda kutembelea ukurasa, watu wa eneo gani hasa wanatembelea ukurasa na mambo mengine mengi. Jambo hili linaweza kufanikiwa hata kama umeamua kutolipia tangazo lako, kama utatumia maudhui nzuri pamoja na picha itasaidia zaidi kuvuta watu katika tangazo lako.

Pamoja na faida nyingi zinazopatikana katika mitandao ya kijamii, bado kuna hasara pia ambazo kama hatutakuwa makini. Lengo la andiko hili ni kukufunulia kuhusu hatari kubwa zilizo katika matumuzi ya mitandao kiusalsma hasa hatari za taarifa na data binafsi. Ulishawahi kujiuliza jinsi taarifa zako zinavyolindwa wakati unajiunga katika mtandao fulani?

Taarifa zako binafsi zinazotafutwa na wadukuzi ni pamoja na :- taarifa za afya, taarifa za ajira, taarifa za kifedha, taarifa za elimu na utambulisho wako kwa ujumla. Mdukuzi akishajua haya yote anaweza kuja kwako kama mwanajamii wako na wewe ukidhani unawasiliana na mtu mnaefahamiana ukajikuta unaibiwa au kupata janga lingine. Kwa sababu hii mtu unatakiwa kujiuliza kwanza wewe ni nani na jinsi gani tunavyojionyesha katika mitandao ya kijamii kabla ya kujihusisha nayo.

Jiulize kwa kwanza kwa nini inaitwa mitandao ya kijamii, kwani hizi njia nyingine za kupashana habari kama tv, redio, magazet si vya kijamii? Jibu utapata kuwa unapokuwa katika mitandao ya kijamii kuna uhuru mwingi na kila mtu anajihisi kuhusika hivyo hapo kuna hatari kubwa kwa kuwa maadui wamo ndani yetu.

Maadili katika mitandao ya kijamii
Tunatakiwa kuzingatia maadili ya maudhui mtandaoni. Ni vigumu sana kueleza nini ni maadili ya kimtandao lakini Ukijiuliza kuhusu faragha ya taarifa zako, itakurudisha kuzingatia matumuzi yenye uaminifu na usafi katika mitandao ya kijamii. Hapo juu nilizungumza juu ya taariafa muhimu za watu mitandaoni, ni wajibu wetu kujiuliza mambo kama haya: kwa nini mitandao mingi ya kijamii ni bure kujiunga, taarifa zangu zinahifadhiwaje, nani anachungulia mawasiliano yako katika mtandao, huyu anaweza kuwa mtu wa masoko?, ni maafisa wa serikali?, ukilizingatia hilo unaweza kuwa salama katika kuvinjari mitandao ya kijamii.

Vihatarishi vya kawaida katikab mitandao.
Sasa tuangalie kidogo aina za vihatarishi unavyoweza kukutana navyo na ajinsi ya kuepuka, kwanza kabisa nianze na hizi wifi za bure, mara nyingi hizi zimekuwa zikitolewa katka sehemu nyingi za starehe kama baa na maduka makubwa. Kama hutakuwa makini unaweza kujikuta ukiuza taarifa zako kwa sababu wadukuzi
hutumia maeneo hayo kama sehemu za mawindo, epuka kufanya mambo muhimu kama kufanya miamala ya kibenki wakati uko katika mtandao. Wadukuzi wakitumia vinasa taarifa kama sniffers huiba taarifa zako muhimu. Pili epuka kupakua mafaili yanayotumwa kwako na watu msiokuwa na makubakiano ya kutumiana faili. Mafaili mengine huwa yanatumwa na wadukuzi na pindi upakuapo faili husika na kulihifadhi lenyewe litakua linafuatilia mienendo yako ya uvinjari katika mitandao na anaweza kupata taarifa kama vile nywila. Tatu acha kuazima chaja za simu kwa watu usiowafahamu, chaja za simu zinaweza kufungwa vifaa vya kunasa taarifa maarufu kama sniffers, wakati unatumia simu huku ikiwa katika kuchaji na ukaingia katika taarifa kama kufanya miamala, taarifa zako zitanaswa na mdukuzi.

Mwandishi Wa makala hii ni mshauri wa usalama Wa masuala ya mitandao na anapatikana kwa kutumia email: fikirakali@gmail.com.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom