Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
Tunafurahi kutumia huduma ya Mitandao ya Simu kama vile Tigo(Yas), Airtel, halotel na vodacom imekua iiturahisishia kwenye mambo mbalimbali kwenye huu ulimwengu wa intaneti.
Lakini changamoto kubwa sana kwenye hii Mitandao ni message za ujumbe wa promotion zinazo leta kero kwenye simu zetu , utakuta umetulia unaweza sema message yenye mchongo wa pesa au kitu Cha maana utakuta message za hovyo haswa kutoka mtandao wa Yas.
Mara "Ongea zaidi", "Tajiri unaachaje dau ili" "umejishindia milioni 1 cheza" " Data zaidi", " karibu huduma ya niwezeshe" au " #SITAPELIKI" ni message zinazo jirudia rudia sana kwenye simu zetu wajitahidi ku control mifumo yao ya kutuma message zao za promotion.
Wengine sio watu wa kubeti sasa utakuta sms za kubeti kibao inaboa sana Bora wawe wanaangalia na huduma unazopenda ndo wakutumie ujumbe kutokana na huduma unayopenda sana kujiunga lakini Sio kutujazia simu.
Mitandao ya Simu kama promotion message mnalipwa na wadhamini basi mtugawie na sisi ๐wateja wenu Sio kwa kutujazia simu pekee.
Ebu sema jambo Gani linakukera toka Mitandao ya Simu tuachie maoni yako watakuja kuyasoma โ๐พ
@yastanzania_
@airtel_tanzania
@halotel_tanzania
@vodacomtanzania
@tcra_tanzania
#bongotech255