Pamoja na hayo , wengi wetu tumeruhusu mambo mengi kufanyika automatic. Yaani ile ukiweka bando basi shughuli za umalizaji bando zinaanza.
Kwenye simu una app zaidi ya 50, na kila app ina muda wake wa kua updated, so kila unapofika muda wake unakuta hata app 5 kwa siku zinajiupdate automatic coz umeset hivo.
Ama lah umeset kila picha ijisave kwenye google gallery, wakati huna bundle ukapiga picha kibao, ukascreenshort ishu kibao, ukarekodi video kadha wa kadha. Siku unaweka bundle hizo vitu zinaanza kujisave na kumbuka picha za kweny simu zina MB za kutosha.
Una bundle unafungua app kibao na umeziruhusu ziendelee kuoparate kwa kujua ama kutojua(wengi hawajui).
Ushauri. Ukinunua simu mpya, iweke vile wewe unataka sio unaanza tu kutumia itakulia bando sana.
Weka Data Sever ON, inasaidia sana.