Mitandao ya simu Tanzania ipo 'compromised'?

Kubishana na huyo kunahitajika moyo wa uvumilivu mkubwa sana
 
Umesema kweli. Kinachotofautisha kati ya ushushushu wa Bongo na nchi nyingine ni kuwa, ushushushu wa Bongo wana-deal na pet issues na mbaya zaidi wanataka wawe ndiyo mapolisi na mahakimu pia. Hawahangaiki na maslahi ya Taifa bali ya viongozi wachache. Usalama wa Taifa ulianza kuharibiwa kipindi cha Mkapa, wakati walipokubali kutrumiwa na Lowassa na Kikwete kuingia madarakani.
 
Kuna bid deals hizi wanazifumbia macho..hakuna wezi kama makampuni ya simu, yanaibia wateja yanaibia serikali lakini sijawahi kuona reaction yoyote
 
Nimesoma mjadala nashangaa umeshindwa kabisa kueleza wazi kabisa kuwa sheria ya mawasiliano na posta inatoa mamlaka kwa serikali na taasisi za usalama kupata taarifa za wateja au mteja yeyote kutoka kwa mtoa huduma yeyote yule......
Sheria hiko wazi na inalazimisha wamiliki wa mitandao kutoa taarifa za mteja na kuwa tayari kuwasilisha ushahidi mahakamani inapo hitajika na mamlaka.

Badala ya kuparamia mitandao ya simu na mitandao basi tuparamie sheria inayo lazimisha watoa huduma kutoa taarifa za wateja.... hakuna mtandao ambao unaweza kugomea sheria iliyo ikubali.........
Tujisumbue kujua chanzo na kufatilia tusitoe lawama pasipo stahili.. hata wewe ungekuwa mmiliki wa mtandao wa tigo usingelikwenda kinyume na sheria husika....

Hawa tunawaonea tuu tu deal na sheria...
 
Leak hii sentence umeisoma na kuielewa? .....Tunapowatia ndimu machoni Tigo tusisayasahau na haya mengine mengi.….
 
Wala si Jambo la kushangaza Sana nambuka hapa tz 1998 alipokuja FBI kuchunga matukio ya kulipia ubarozi wake hapa tz na kushindwa kupata ushahid wa kutosha kupitia kwenye mawasiano ya sim vyombo vyetu vya habari kikaripoti hapa kila sim inayopigwa marekan kuna sikio la FBI sasa kwa kuwa hapa hatujafikia hatua hiyo nini chakushangaza hapo kampun husika kutoa ushirikiano kwa kesi za selikali?
 
Mkuu Mshana Jr umeongea ukweli kuntu. Nchi hii imefikia mahali pabaya sana, hasa linapokuja suala la chuki za kiitikadi za kisiasa. Mwendazake na genge lake la Sukuma Gang ndio waliofikisha nchi hii mahali hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…