Mitaro ya maji katika paa la flat roof

Mitaro ya maji katika paa la flat roof

Kitumburee

Senior Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
142
Reaction score
88
Habari zenu wanajamvi. Nimefanikiwa kujenga nyumba ya flat roof, nyumba ina mitaro darini inayokinga maji ya mvua ila mitaro inaonekana kwa ndani kama mnavyoona ktk hii picha.

Mtaro uko kulia (sebuleni) na kushoto (dining) . Dari haina muonekani mzuri, Naomba mawazo yenu juu ya design nzuri ya dari (gypsum board) itakayoficha mitaro na nyumba ikapedeza. Ukiweza kunitumia picha ya sammple itapendeza.

Shukrani.

CE0E71CA-7221-422D-A9AF-19F6EF69B5B2.jpeg
 
Sasa mbona hii ulitakiwa kufanya kabla hujagonga hizo mbao? Hapa tafuta mafundi wazuri wa kuweka hizo style waangalie jinsi ya kufanya. Isikupe shida sana inawezekana kufanyika either kwa kuongezea mbao au wavunje sehemu nyingine waweke upya
 
Asante mkuu, kupavunja haiwezekani lakini,
 
Hapo iltakiwa maji yavyunwe katikati kwa kuweka mtaro ,yaani bati Kama ni futi kumi upande wa kusho na kulia
 
Habari zenu wanajamvi. Nimefanikiwa kujenga nyumba ya flat roof, nyumba ina mitaro darini inayokinga maji ya mvua ila mitaro inaonekana kwa ndani kama mnavyoona ktk hii picha...
Mbona pic kwangu hazifunguki?
 
mkuu unatakiwa udesign ndo upige draft. maji jaribu kuyavuna kati kati. bora uingie gharama ya marekebiaho sasa. maana ramani inaweza kukunyima raha mpaka ukakosa amani kwenye nyumba yako.
 
Saa nyingine wakati unataka kushauri kitu, fikiria kwanza kichwani kwako kabla ya kuandika, sasa hapo ashapiga gutter, kupaua mpaka kapiga draft wewe unamwambia maji ayavunie kati kati? si unaona nyumba ishakamilika hapo? Avunje gutter na kutoa bati halafu aweke gutter jingine?
 
wewe unafikiri nafikiria kichwani kwako?
 
Hii mitaro ilitakiwa kuwa pembeni yani hapo gutter inapoanzia ndio ukuta wenye madirisha ukitakiwa uwe hapo gutter ikae kwa nje, sijajua iyo slab nao inamwaga maji kwenye hiyo gutter?
 
Zipo za style hiyo unayosema, zipo za gutter kati kati na zipo hizi pia. Maji yanamwagika nje kama kawaida
 
Nafahamu vizuri, naongelea specific kwa hii, huoni kuwa uwepo wa hiyo gutter hapo unamuumiza kichwa muda huu?je hizo zenye gutter katikati huwa gutturs zinaonekana kwa ndani kama hivi?
Zipo za style hiyo unayosema, zipo za gutter kati kati na zipo hizi pia. Maji yanamwagika nje kama kawaida
 
Naamanisha kuvunja hizo mbao, siyo gutter, tafuta designer wanaotengeneza maua ya gypsum, siyo hawa wagonga gypsum.
Mkuu hizo mbao ni flat surface ya ceiling. Shida sio hizo mbao shida ni huo mtaro nauficha vipi bila kuharibu nyumba
 
Hii mitaro ilitakiwa kuwa pembeni yani hapo gutter inapoanzia ndio ukuta wenye madirisha ukitakiwa uwe hapo gutter ikae kwa nje, sijajua iyo slab nao inamwaga maji kwenye hiyo gutter?
Slub ina bomba za kushusha maji chini, haimwagi ktk gutter
 
Mfano, unaweza kujenga Box linalofanana na hiyo gutter kwa hizi pande nyingine, then hapo katikati ukatengeneza urembo wowote. Ukija kupiga rangi mtu hajui ipi gutter ipi board.
Asante mkuu, hii ilikua option ya haraka kufikiria ila itafanya nyumba iwe fupi sana. Ndio naumiza kichwa kutafuta option nyingine
 
Hii mitaro ilitakiwa kuwa pembeni yani hapo gutter inapoanzia ndio ukuta wenye madirisha ukitakiwa uwe hapo gutter ikae kwa nje, sijajua iyo slab nao inamwaga maji kwenye hiyo gutter?
Kwa ramani ilivyo gutter inakaa pembeni ina sijui kwanini mchora ramamni na fundi hawakushautiana gutter ikae nje. Na mimi niliona sawa tu ila kwa sasa ndio nagundua when it is too late
 
Back
Top Bottom