Mitazamo na tathmini ya Uchaguzi 2015

CUF & MAALIM WABEBA ZIGO

JECHA AJA NA MAPYA


Mazungumzo ya mufaka yamevunjika. Hakuna taarifa isipokuwa huyu anasema yule kasema

Kwa muda tulieleza jinsi mazungumzo yalivyolenga kuvuta muda, kupoza joto na kisha kushtukiza

Kama tulivyosema ndivyo ilivyojiri na tulisema, mwisho wa siku mzigo utakuwa mabegani mwa CUF

Leo Maalim ana vibarua viwili .

Kwanza, kuwaeleza wafuasiéwananchi nini kilitafutwa, kimekwama wapi na kwanini.

Pili, Jinsi gani ya kuondoka katika mkwamo unaolenga uhalali kwa CCM kufuatia uchaguzi marudio

Jecha ametangaza March 20 siku ya marudio.
Kama wakati anatangaza kufuta hili nalo limetokea katika njia ile ile.,bila kuambatana na wajumbe

Jecha anasema hakutakuwa na kampeni, na majina yaliyokuwepo ni yale yale.

Hapa kuna nadharia mbili au tatu

1. Kukataza kampeni ni kunaweza leta hisia kuzuia mikutano kwa njia ya kificho ili yaliyotokea yasijulikane zaidi.Kinachotakiwa ni watu kupiga kura si kupata habari nyingine

2. Majina ni yale yale imelenga mambo mawili kwa mtazamo na maoni yetu wengine

a) Kubakiza majina ili ikitokea watu wamesusa,uwepo wa majina utajenga uhalali wa uchaguzi.
Kwamba, kulikuwa na wagombea na X kashinda.

Hili pia linaungana na lile la kupiga marufuku kampeni.
Maana yake,watu wasijeuliza mbona jina lipo mgombea hakupiga kampeni au alitangaza kutoshiriki

b) Majina kubali yale yale kumelenga kuhakikisha hata kama chama au baadhi ya vyama havitashiriki, vile ``vinavyotaka`` ambavyo vingine vinaweza kuwa na ``ushirika`` vinaendelea na uchaguzi

Ikitokea mshiriki anafukuzwa katika Chama chake, bado jina lake litakuwepo.
Lengo ni kukabiliana na vyama vitakavyofukuza wanachama wao wanaotaka ``kushiriki`

Unaweza kuona hesabu zinavyopangwa kIufundi kuujengea uchaguzi sura na uhalali unaotakiwa.

CHANGAMOTO ANAZOKUMBANA NAZO JECHA

Kwanza, kuonyesha bila shaka kuwa maamuzi ni ya tume nzima na si kama alivyofuta peke yake

Hakuna kumbu kumbu zozote za kikao kilichofuta uchaguzi licha ya kutokuwa na mamlaka, je, kuna kikao au kumbu kumbu zozote za tume kutangaza tena siku ya uchaguzi!!

Wajumbe wa tume wakajitokeza na kutoa kauli tofauti a, tume itabaki Jecha

Ile akidi inayokamilisha tume au ule mchanganyiko utazua maswali mengine magumu sana kwa jecha

Pili, kwa wanachama wanaogombea wengine wamefukuzwa na vyama vyao.

Hivi karibuni habari za mgombea wa ADC kufukuzwa uanachama zimeandikwa kwa kirefu.

Maana yake, kiongozi huyo hata kama anataka kushiriki uchaguzi wa marduio kisheria hataweza.

Kisheria usajili wa vyama ni suala la muungano.
Msajili wa vyama anapelekewa taarifa za kufukuzwa wanachama .

Mwanachama akifukuzwa tayari anapoteza masilahi (privilege)ikiwemo kugombea uongozi

Katika mazingira hayo Jecha hatakuwa na la kufanya

Ili afaninikiwe anahitaji kufanya kazi na msajili kutengua kitendawili hicho

Vingievyo itabidi ajitokeze ku-clarify hali hiyo, na katika mazingira yaliyopo atavuruga Zaidi

Tusemezane
 
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KAIBUKA

NI BAADA YA KUKAA'' KIMYA'' SAKATA LA ZNZ LIKIENDELEA

AKUBALIANA NA MARUDIO, AFUMBIA MACHO UBAGUZI

Msajili wa vyana Jaji mstaafu Mutungi amevieleza vyama vya siasa kushiriki uchaguzi wa Zanzibar

Kama mtakavyosoma bandiko la hapo juu, ili Jecha afanikiwe zoezi la marudio anapaswa amshirikishe msajili. Hoja ni kuwa waliofukuzwa au wanaogoma kushiriki hawawezi kuchukuliwa hatua na Jecha

Na wala hakuna sheria inayolazimisha jina la mtu liwepo katika sanduku la kura.

Kkupiga marufuku shughuli za mikutano ya kisiasa si wajibu wa ZEC. Ikibidi msajili ashirikishwe

Katika muda wote wa malumbano kati ya CUF na CCM msajili ambaye ni mlezi alikuwa kimya.

Hakushiriki katika mazungumzo wala hakuchukua hatua kama msajili kutafuta ufumbuzi

Majuzi amejitokeza akivitaka vyama vishiriki uchaguzi wa marudio.

Bila kueleza sababu za kushauri alisema, uchaguzi ni sehemu ya uhai wa vyama na hivyo vishiriki

Kwa lugha nyingine, msajili anakubaliana na zoezi la kurudiwa uchaguzi.

Haieleweki kama kitakuwepo chama kitakachogomea matokeo msajili atatoa tena kauli ya marudio

Kauli ya msajili inakuja na 'gharama' nyingine. Kwamba, anateuliwa na Rais na kutengeneza 'kiungo' kati ya Rais wa JMT na suala la ZNZ.

Wale wanaosema tatizo halimhusu Rais wa JMT waNaweza kuona moja kati ya viungo hivyo

Usajili wa vyama ni suala la muungano. Tumesikia si mara moja ofisi ya msajili akikemea kukiukwa kwa maadili na taratibu za vyama. Hiyo ni jukumu na kazi kama mlezi wa vyama.

Katika hali inayoshangaza na kusitisha, CCM ilipita mbele ya uso wa nchi na dunia ikiwa na bango la ubaguzi dhidi ya Mschotara.

Sheria ya msajili inasema chama cha siasa hakipaswi kuwa na aina yoyote ya ubaguzi

Bango la Machotara halina shaka ni la kibaguzi. Hata CCM wamelaani ingawa ni katika kujikosha wakijua ni kinyume cha sheria, ubinadamu na maadili.

Wakati wote huo msajili alikuwa kimya landa kama alikemea bila sisi kuwa na kumbu kumbu zozote.

Leo anaingia wakati hali inazidi ni mbaya. Hakusikika akishiriki wakati wa mtafaruku. Maana yake nini?

Hili linaonyesha jinsi vyombo mbali mbali vinavyochukua upande katika sakata zima.

Ni vema msajili akae kimya vinginevyo atafungua ukurasa wa maswali na maoni katika wakati huu yasiyohitajika.

Tusemzane
 
BALOZI AMINA SALUM ALI

ANAMHITAJI MAALIM SEIF LAKINI ANAMTAJA KAMA TATIZO

KAULI ZAKE 'ZA KIBAGUZI' ZINAIWEKA ZNZ NJIA PANDA


Mgombea Urais wa CCM Balozi Amina Salum Ali ametoa kauli zinazozua maswali ya hali ya kisiasa ZN

Miongoni mwa kauli , ni ile aliyosema mgogoro wa ZNZ ulianza na historia ya mapinduzi 1964

Balozi kasema mapinduzi yaliwagawa wazanzibar katika makundi mawili, wa ndani na wa nje
Akasema waliokimbilia nje ndio wanataka kurudi

Balozi anatamani SUK ivunjike kwasababu CUF hawaelewi maana ya maelewano
Akasema mijadala iheshimiwe kwasababu ni suala la 'nipe nikupe' na kusema katika muafaka lazima kuwepo na kutoa na kupkea na CUF wanataka kupokea tu

Mazingira yanaonyesha Maalim Seif ana masilahi binafsi na ndiye tatizo.

Hata hivyo balozi anamtaka Maalim abadili mtazamo na kushiriki uchaguzi wa marudio!

TATHMINI YETU
Maneno ya Mh balozi yanasikitisha na kutisha. Akiwa mtu aliyewakilisha Afrika katika umoja wa mataifa na mtu aliyetArajiwa kuwa Rais wa JMT, kauli zake zinaonyesha tatizo na wingu nene visiwani

Balozi anaposema kuna kundi linataka kurudi inashangaza.

Iweje CUF iruhusiwa kufanya siasa miaka yote ikiwa inajulikana ni kundi la nje?
Mh balozi lini alilizungumzia hili?

Kinachoshangaza, Balozi anataka Maalim Seif abadili msimamo na kushiriki uchaguzi.

Yaani mtu anayesema ndiye tatizo na anatumika na kundi kutoka nje bado anamuhitaji ashiriki Urais akiwakilisha 'kundi kutoka nje'. Hivi kweli balozi alikuwa na ufahamu na alichoongelea?

Mh Balozi ana 'insinuate' lugha za kibaguzi. Ukimsoma kwa , pengine hawezi kulaani bango la uchotara. Mh Balozi hajiulizi, ni wazanzibar wangapi wasio na unasaba au uhusiano wa kidamu?

Maelezo ya balozi yanaashiria maana moja, ili nipe nikupe ikamilike ni lazima CCM washinde na CUF wasaidie serikali ya umoja wa kitaifa. Kama ni hivyo, kuna sababu gani za kufanya uchaguzi?

Endapo Seif ni tatizo, ni nani anayepaswa kushiriki siasa za Zanzibar na sifa zake ziwe ni zipi?

Kauli kama za balozi zinaashiria tatizo zito katika visiwa vya Zanzibar.

Linaonyesha kuwa waomba uongozi kutoka ZNZ wanaweza kuwa tatizo ndani ya JMT.

Kwavile siasa zao zimejikita katika rangi na ubaguzi ambao mtu kama balozi hawezi kuuona tahadhari ichukuliwe mapema.

Leo balozi Amina angalikuwa Rais wa JMT sijui tungekuwa tunazungumzia nini! Mungu ni mkubwa

Wahafidhina wa ZNZ ndilo tatizo na wamesahau kuwa hakuna marefu yasiyo na ncha.

Balozi ajiulize, wale wafadhili wa CCM wenye rangi zisizofanana na matakwa yake nao wanatoka nje ya upande gani?

Huko CCM hao wa 'nje' wana daraja gani? Na wanajisikiaje kwa kauli za mh Balozi?

Mbegu wanazopanda ni za hatari kwa vizazi vyao. Kwa maneno ya balozi mtu aliyechanganya damu si mzanzibar halisi na huyo ni 'wa nje'.

Haya ni mambo yakukemewa na kulaani. Lini tumefika mahali pa kuangalia ngozi kama kigezo cha uraia? Ni lini tumeanza kuwa na Raia first class na second class!

Mungu analipenda taifa la Tanzania!

Tusemezane
 
Dr SHEIN AMWEKA PAGUMU JECHA

CCM INA HAHA, BILA CUF ''UHALALI'' U-MASHAKANI


Home

Rais wa ZNZ amekaririwa na vyombo mbali mbali kutoka ZNZ

Gazeti la Habari leo limeandika Dr Shein amemtupia lawama Maalim Seif kwa kwenda kuzungumza mambo ya vikao katika vyombo vya habari. Kwamba, shArti la mazungumzo lilikuwa kuwa na vikao vya siri

Gazeti la Nipashe linamkariri akisema kushiriki uchaguzi ni hiari ya kila mmoja na CCM wanajpinga

Katika hali tuliyowahi kuizungumzia katika mabandiko haya, Rais Shein amekwepa kusema uchaguzi ulifutwa na Jecha. Wakati ZEC ikiendelea kuhesabu Jecha aliibuka katika TV kufuta uchaguzi

Wajumbe wawili wa tume walitoa ushuhuda wa kutoshiriki katika maamuzi.

Hakuna kumbu kumbu za kikao chochote cha ZEC kufuta uchaguzi.
Wala sheria inayomwezesha mwenyekiti kufuta uchaguzi wote
Hakuna malalamiko kutoka majimboni na matokeo yalisainiwa na wahusika wa vyama vyote

Lakini pia tujiulize, yale aliyozungumza Janury 12 kuhusu cuahguzi wa marudio hayakukiuka mazungumzo ya siri anayosema? Kakaririwa akisema yeye ni muungwana hajasema chochote! Jan 12 hakusema kitu?

Tulieleza huko nyuma CUF wasifikiri CCM inapotumia neno tume ni kwa bahati mbaya.

Wanajua baada ya muda hoja ya Jecha kufuta uchaguzi itapotea na tume itabeba mzigo

Akitangaza uchaguzi wa marudio Jecha alisema, hakutakuwepo na kampeni na majina ya wagombea ni yale yale yaliyokuwepo.

Tulieleza kuwa nia ya Jecha ni kuhakikisha kuwa majina yanakuwepo ili kujenga dhana ya kuwepo kwa ushiriki wa vyama. Jecha na CCM wanatambua bila hivyo, hali iliyopo sasa itazidi kutia aibu katika uso wa dunia

Kauli ya Rais Shein kuwa kushiriki ni hiari, imetoka wakati CCM wakihaha kutafuta 'washiriki' wa uchaguzi ili kujenga uhalali wa uchaguzi wa maurdio.

Hakuna asiyejua matokeo yake kinachotakiwa ni kujenga uhalali kwa ushiriki wa vyama

Kwa kauli hii, Dr Shein anafuta kauli ya Jecha kuwa majina yatabaki yale yale na kufungua mlango wa majina ya uchaguzi kuwa ya CCM.

Hivyo uchaguzi wa vyama vingi utakuwa wa CCM kama miaka ya chama kimoja

Kauli za kuchanganya mambo kutoka kwa wana CCM wanaoona mambo hayaendi kama wanavyotarajia.

Kauli ya Balozi Amina Salum Ali ya Seif ndiye tatizo halafu akimtaka ashiriki uchaguzi inaeleza zaidi.
Kwamba mtu ambaye ni tatizo anahitajika kuwa katika uchaguzi! sijui nani anaelewa hili

Sasa haya ya Rais wa ZNZ yanazidi kutoa picha kuwa uchaguzi unaelekea kuwaelemea.

Jumuiya ya kimataifa ikishupalia tatizo la ZNZ ni dhahiri tunaweza kujikuta na wakati mgumu kama Tanzania

Kwamba nchi inaweza kupita kipindi kigumu cha mahusiano na ustawi kwasababu tu kuna watu wachache wasiokubali demokrasia ichukue mkondo wake

Kwa hili tusema, mwenyekiti Jecha, Rais keshatoa raia ya majina kuwa hiari, kakuweka mahali pagumu maana hakuna jinsi ya kuweka majina mengine. Utaendesha uchaguzi kama wa CCM au mkutano mkuu wa CCM


Tusemezane
 
HAYA KAYASEMA JAJI LUBUVA, MWENYEKITI WA NEC

TUME YA(ZA) UCHAGUZI NI HURU , HAZIINGILIWII

RAIS WA JMT HANA MAMLAKA ZANZIBAR

Home
Home

Wanajamvi tumeweka baadhi ya magazeti yaliyomnukuu Jaji Lubuva, mwenyekiti wa NEC

Kwa ufupi Jaji anasema, tume za uchaguzi ni huru na haziingiliwi na mtu
Kaendele, suala la ZNZ Rais wa JMT hana mamlaka ya kuliingilia

Na mwisho kanena, wanaosema aingilie wakati huo huo wanataka tume huru wana jichanganya

Jaji Lubuva alikuwa mwanasheria mkuu kwa pande zote za muungano.

Heshima yake ya Ujaji inaelezwa na heshima kubwa waliyo nayo Majaji mbele ya jamii kama watu wenye weledi wa kutafsiri na kusimamia sharia.

Watu wanaoweza kutumia uwezo wao katika mambo si ya kitaaluma badi yanayogusa jamii

Jamii huwaona majaji ni wenye uwezo mkubwa , waadilifu na wa kweli ndani na nje ya taaluma yao

Kuna swali linalozuka miongoni mwa watu. Swali ni je majaji waachwe kuendelea na shughuli za taaluma yao ya sheria na wasishirikishwe katika mambo ya jamii?
Au iendelee kama hali tunayoiona sasa?

Swali hili lina maana moja, kwamba, heshima ya majaji ni kubwa, hakuna anayependelea kuona baadhi yao wakitiliwa shaka ima kwa maadili au weledi

Wapo wanaojiuliza, ni vipi majaji wanaweza kubaki nje ya mitego ya kisiasa au ni vipi wanaweza kuhudumiwa ili kukidhi haja na heshima yao.

Ni vipi wanaweza kuwa huru ili kuisdaida jamii bila kutegwa au kuzongwa ?

TURUDI NYUMA KIDOHO
Uchaguzi wa 2000 uliacha makovu makubwa na vifo vya watu kule Zanzibar.
Kwa mara ya kwanza, wakimbizi kutoka Tanzania walipatikana nchi jirani na za ulaya.

Walikuwa ni Watanzania, waltoka JMT wa Tanzania yenye kiti kimoja na Rais anayewakilisha. Hawakuwa wazanzibar katika uso wa dunia

Kwa kutambua ukubwa wa tatizo, Rais Mkapa aliunda tume ya kuchunguza nini kilikwenda kombo hadi watu wakapoteza maisha.

Mongoni wa wajumbe ,alikuwepo Rais Kikwete akiwa waziri wa mambo ya nje, na mwingine tunayemkumbuka alikuwa Prof Maghembe

Tume hiyo iliundwa na Rais wa JMT. Hili tunadhani linakumbukwa na wengi akiwemo Jaji

Tunajua Amir Jeshi mkuu ni mmoja tu, ambaye ana usaidizi wa mawaziri kadhaa kama wa mambo ya ndani , ulinzi na usalama, mambo ya nje na ofisi ya makamu wa Rais kwa uchache wa kutaja

Uwepo wa askari iwe Polisi au majeshi katika eneo lolote la JMT ni kwa kauli ya Rais wa JMT

Usajili wa vyama ni jambo la muungano. Msajili anateuliwa na Rais JMT, ana ofisi pande zote

Tunajua pia shughuli zote za kidiplomasia zinapitia JMT.

Meli za Iran zilizokuwa zinakwepa vikwazo na zilizosajiliwa ZNZ halikuwa suala la ZNZ bali Tanzania

Kuna wajumbe 5 ndani ya bunge la JMT kutoka baraza la wawakilishi.

Na wapo wabunge kutoka Znz kwa kuchaguliwa na kwa nafasi maalumu ndani ya bunge la JMT.

Wote wanashiriki shughuli za bunge la JMT ambalo pamoja na mengine ni kusimamia serikali ya JMT

Ndani ya baraza la mwaziri la JMT, Rais wa ZNZ ana kiti na ni mjumbe

Mwingiliano huu ni sehemu tu ya mambo mengi yanayounganisha JMT na Zanzibar.

Jaji Lubuva anaposema Rais wa JMT hana mamlaka Zanzibar, ni kitu gani anachokusudia kueleza?

Endapo Rais wa JMT hana mamlaka Zanzibar, nini maana ya Rais wa JMT?

Itaendelea.....
 
Inaendelea

JAJI LUBUVA NA UHURU WA TUME

Mwenyekiti wa NEC anasema, tume ya uchaguzi ni huru na haiingiliwii na mtu au chombo kingine

Kwa mtazamo , mwenyekiti anachokisema kwa kuangalia ZNZ na suala la Rais wa JMT kuingilia kati mzozo ni kutueleza kuwa Tume huru ya uchaguzi Zanzibar ZEC haiwezi kuingiliwa kimaamuzi na Rais

Kwa mujibu wa katiba ya JMT tume huchaguliwa na Rais wa JMT na haithibitishwi na chombo kingine

Ukiacha sifa chache zilizotajwa hakuna vigezo vingine vilivyoelezwa 'vetting' ya wajumbe
Ndivyo ilivyo kwa NEC na ZEC

Tume huru haina fungu maalumu la kuendesha shughuli zake. Inategemea pesa kutoka serikalini

Watendaji wa tume katika ngazi za chini huwahusisha maafisa ambao ni waajiriwa wa serikali

Hili limeeelzwa na kamisheni ya EAC iliyofanyia marejeo uchaguzi mkuu wa Tanzania Home

Huko nyuma tume ikiandaa daftari, kila mara serikali ilipotoa maelezo tume iliyachukua kama 'maagizo'

Tume ilibadili maafisa wakati kampeni za uchaguzi zikiendelea. Inasemwa, wajumbe walitoka serikalini

Katika kazingira hayo mwenyekiti anawezaje kuushawishi umma kuwa uhuru wa tume ulitimizwa?

Pia tujiulize, uhuru wa tume unatoka wapi ikiwa ZEC inaweza kuendeshwa kwa tamko la mtu mmoja?

Ilikuwaje Jecha akaibukia vyombo vya habari akiwa mwenyewe na serikali kutohoji uhuru wa tume ?

Tunasema hivyo kwasababu tume huru si mtu ni kundi la watu, je, Jecha aliwasilisha uhuru wa tume?

Kura zikiendelea kuhesabiwa, makamu mwenyekiti aliondolewa nawanaosaidikiwa wa vyombo vya dola. Ilikuwaje tume huru iingiliwe wakati nyeti wa kuhesabu kura? Uhuru wa tume anaousema upo wapi?

Tume zinafanya kazi kwa sheria. Linapotokea tatizo sheria za tume huru ndizo zinafanya kazi

Jaji hajatueleza suala la ZNZ kisheria limeakaaje. Kwamba, kuna uhalali wa kufutwa matokeo yote na mtu mmoja? Je, yeye kama mwenyekiti wa NEC anaweza kuchukua hatua kama za Jecha?

Tumalizie kwa kusema, katika muda wote wa NEC imekaa kimya hata pale madai mazito yalipotolewa.
Inashangaza mwenyekiti akiibuka kutoa maoni mengine yanakinzana na maoni yake siku zilizotangulia.

Kama alivyonukuliwa , Chadema wanadai wakati wa kukusanya maoni ya tume ya Warioba, Jaji alitilia shaka uhuru wa tume ya uchaguzi. Leo shaka imeondoka na sasa anaafiki uhuru ule ule alioutilia shaka

Muhimu zaidi ni mwenyekiti wa tume anapoongea bila kuwa na misingi ya kisheria akijua kazi yake imejengwa sheria na haki.

Pengine akiwa Jaji ingependeza kuainisha kitaalamu na kitaaluma kuhusu madaia ya Rais kutoingilia uchaguzi wa ZNZ na uhuru wa tume akipangua hoja zinazotolewa na watu wanaoweza kuwa na mapungufu ya kujua sheria

Mwenyekiti wa NEC hakufanya hivyo, naye kama raia wengine akaingia katika malumbano rahisi

Kauli za mwenyekiti wa tume hazina tofauti na za Msajili wa vyama Jaji Mutungi.

Jaji mutungi akiwa mlezi wa vyama alikaa kimya hadi majuzi alipojitokeza kuvitaka vyama vishiriki uchaguzi wa marudio

Hakueleza au kufafanua misingi ya kisheria katika eneo lake inayotokana na matatizo ya Zanzibar

Anachotueleza msajili ni kuwa uchaguzi wa marudio ukiwa na malalamiko, njia rahisi ni kuitisha mwingine na vyama vishiriki tu.

Ukimya wake unatueleza mengi na uhuru wa vyombo vinavyosimamia uchaguzi katika nchi yetu

Hapa ndipo lile swali linalohusu Majaji linapojirudia. Tunaamini majaji ni watu wenye weledi, wanaoijua jamii na changamoto zake, lakini je, kuwapa majukumu mengine nje ya taaluma yao kuna matokeo yoyote tofauti?

Kuwaingiza katika shughuli za kisiasa hakukinzani na majukumu yao yanayohitaji ukweli, uadilifu na uaminifu?hasa tukizingatia kuwa siasa na wanasiasa hucheza 'mchezo mchafu' na uadilifu wao unahojiwa kila siku?

Ni mjadala mrefu na wenye utata, lakini ni bora kuuzungumza

Tusemezane
 
November 15 2015 tuliandika hayo hapo juu. Tulisema, suala la ZNZ linagusa nchi nzima na tutajikuta tunawatia wananchi shida zisizo na sababu kisa tu kulinda CCM Zanzibar ambayo ni kundi la watu wachache wasiotaka kuona demokrasia, waliojipa haki ya kutawala na wanaodhani ni raia wa daraja la kwanza

Muda wote CCM na serikali yake walidhani mbinu za kuupumbaza ulimwengu za kila mara zitafanikiwa
Inaonekana mataifa yamebaini udanganyifu na sasa tupo njia panda

Soma habari hii ya Mahiga

Bandiko linalofuata tutapitia hoja tulizozikazia ili kuonyesha namna ambavyo CUF walikosea na namna ambavyo makosa yao yanatumika kubadilisha hoja nzima. Tutaangalia kauli za waziri na jinsi zinavyopingana na za viongozi wengine hata kufikia kukana baadhi ya wahsiriki wa mazungumzo

Tutaendelea
 
KAULI YA BALOZI MAHIGA

Tuliandika kosa la CUF la kuzungumzia ZEC na kuacha itamkwe kila siku kana kwamba ndio tatizo.

Uchaguzi haukufutwa na ZEC na hivyo ilikuwa muhimu kusema uchaguzi uliofutwa na Jecha.

CUF hawakuliona hilo na sasa kibao kimegeuzwa kuwa tume iliyofuta ni ZEC hata pale baadhi ya wajumbe walipokana, na hakuna kumbu kumbu zozote za kikao chochote cha ZEC kilichokaa kufuta uchaguzi. Kauli hiyo kaitumia sana balozi Mahiga

Pili, iliandikwa hapa duru, tatizo ni kubwa na litaitumbukiza nchi nzima, tunaona kauli za balozi zikieleza wazi jinsi Tanzania inavyoathirika na si Zanzibar.

Athari haziishi nje ya nchi, hadi sasa uchaguzi utarudiwa kwa gharama za mabilioni ambazo tutazibeba sote. Tukumbuke mgogoro umeathiri sana uchumi wa ZNZ na ukweli kuwa makusanyo ya kodi za ZNZ hayazidi bilioni 12/mwezi, ni wazi wanahitaji msaada ambao hatujui unatoka wapi.

Kwa mantiki, Mtanzani wa bara anabeba mzigo kwa jambo lisilomhusu ndani na nje hadi tutakpoambiwa chanzo cha pesa za marudio ya uchaguzi na athari za mahusiano ya kimataifa

Tatu, balozi anawataka wahisani washawishi CUF kurudi katika uchaguzi.
Halafu anatoa ushauri mazungumzo ya kuaminiana yaendelee.
Haa! kama msimamo ni CUF kurudi katika uchaguzi, mazungumzo yanahusu nini tena?

Nne, balozi anasema ZEC ilifuta matokeo baada ya watu kujiandikisha zaidi.
Hilo halikuonekana wakati wa kuhesabu kura vituoni hadi washindi kupatikana.
Lilionekanje na tume inayojumlisha namba siku 2 baada ya kupiga kura?
Kuna ushahidi wa aina yoyote?

Nne, kama watu walijiandikisha zaidi, na kwa utaratibu hao hao ni sehemu ya wanaomchagua Rais wa JMT, kwanini matokeo ya JMT yawe halali?

Tano,balozi anasema walishitisha kuhesabu kura. Balozi hajaeleza ni kwa kikao gani au kumbu gani zinazoonyesha ZEC ililsitisha kuhesabu kura.

Na kwanini Jecha aliibuka mwenyewe huku makamu akichukuliwa na watu wasiojulikana?

Ilikuwaje makamu aendelee na kazi ya kuhesabu wakati Jecha anakwenda kutanagaza ikiwa ilikuwa uamuzi wa pamoja?

Sita, hatuna uhakika kama Mkapa hakushiriki mazungumzo. Ali Hassan mwinyi alishiriki kama Rais wa ZNZ na wa JMT. Inapotokea balozi kusema Marais wa JMT hawakushiriki, kauli hiyo inaukweli?

Saba, Balozi anasema 'kuwatendea haki watanzania' wengine kwa CUF kushiriki.
Kwanini wanaokataa matokeo wasikubali ili kuwatendea haki Watanzania wengine?

Nane, balozi anasema CCM iliungana na ZEC kuwa lazima uchaguzi urudiwe.
Juzi Mwenyekiti wa CCM anasema hata CCM haikuataka marudio. Kauli hizi mbili zinatoa picha gani?

Tisa, mwenyekiti wa ZEC alisema majina yatabaki yale yale katika uchaguzi wa marudio.
Rais wa SMZ akasema watakaosusa wasuse shauri yao.
Balozi Mahiga nanasema 'itakuwaje miaka 5 bila chama kikubwa kama CUF?
Hapa unaweza kuona kuchanganyikiwa kwa viongozi, na hili dilo linasumbua akili za wananchi

Kumi, Balozi Mahiga anataka kuwaeleza nini wale wana CCM wanaotaka matokeo yatangazwe tena wakiwa wameshika nyadhifa mbali mbali kitaifa na kimataifa?

Balozi anasema kama CUF walishinda basi warudi katika uchaguzi kwavile watashinda tena.
Kauli hii inashangaza sana.

Tunaamini balozi ni mwanadiplomasia, anajua taratibu nyingi za demokrasia
Ameshuhudia migogoro mingi, kauli rahisi kama hii inatia shaka sana

Hivi CUF wakishindwa, nao pia waombe uchaguzi tena kwasababu CCM walioshinda watashinda tena?
Tutakuwa taifa gani na kutakuwa na kosa gani tukiitwa taifa la wendawazimu?

Kinachoendelea ZNZ sasa kuhusu 'mzombi' kinaeleza kwa undani.
Hii hoja haikupaswa kutolewa na balozi wetu ambaye ni waziri.

Ni hoja nyepesi na rahisi ikijibu hoja nzito yenye hatari.
Ni hoja tunayoiona ilitoka kwa bahati mbaya, kama alidhamiria basi tuamini tatizo ni kubwa

CCM na serikali yake itawaadhibu wananchi wa Tanzania hasa bara bila sababu

Tumetoka kuwa taifa la mfano, sasa tupo viwango sawa na akina Madagascar.

Tumepoteza ushawishi wetu na tahamani zetu. Inasikitisha sana!
 
CCM YACHAGANYIKIWA
KILA MTU NA KAULI YAKE
masilahi mapana yataifa yafumbiwa macho, lengo ni kutawala iwe iwavyo


Tangu CUF walipotangaza kutoshiriki uchaguzi-marudio, CCM wamekumbwa na kiwewe

Kauli zinazotoka kwa makada zinachanganya umma, hazieleweki na zingine ni za hatari

Baadhi ya wastaafu wa CCM , wamenukuliwa wakisema kura zimalizwe kuhesabiwa

Hawa walimaanisha haki itendeke na kila mmoja aridhike hata kama hakupenda

Mwenyekiti wa CCM,kwa muda mrefu amekaa pembeni, alinukuliwa akisema CCM haikupenda marudio yanayoligharimu taifa. Hakuungana na CUF uchaguzi umalizwe

Rais wa JMT kasema hakuna suluhu isipokuwa marudio ya uchaguzi.

Tunajiuliza, suluhu ya marudio hatma yake ni ipi? CCM wakishindwa watakubali matokeo?
CUF wakishindwa wakaomba marudio itawezekana?

Kwanini suluhu iwe kurudia uchaguzi na si kumalizia kuhesabu kura.

Kama lipo eneo lenye matatizo uchaguzi unaweza kurudiwa ingawa hakuna lililoripotiwa

Waziri wa mambo ya nje, kaja na suala la marudio kwavile tu tume ilifuta uchaguzi.

Hakwenda kwa kina kuanisha sababu zilizotolewa na tume ambazo ni taribani 9.

Hoja ni kuwa uchaguzi umefutwa na tume hata kama dunia inajua ni Jecha

Waziri aliwataka CUF washiriki uchaguzi maana'tuatendelea kuishi hivi kwa miaka 5"?
Hapa alitambua kurudia uchaguzi si jibu, kama hakuna maelewano na ridhaa

Akaenda mbali kuwaomba wahisani waingilie kati kuwashawishi CUF kurudia uchaguzi

Katibu mwenezi CCM amesema hata CUF wasiposhiriki uchaguzi wa maruido upo pale pale
Tunakumbuka 'goli la mkono' . Tumesema mara nyingi kauli zake zinatia shaka

Katika mazingira ya kisiasa ya visiwani, vyama vyenye wafuasi ni CCM na CUF.
Kauli za mudhi zinazochochea hali ya hasira tukijua utulivu unahitajika sana

Visiwani si salama kama wananchi wakigawanywa na kugawanyika katika makundi
Amani ya visiwani inahusu taifa zima kwa muundo wa nchi yetu.

Athari za ZNZ zinawafikiwa Watanzania wote popote walipo

Maswali,CCM watarudia uchaguzi na kujihakikishia ushindi, wanahitaji CUF ya nini?

Kwanini kila siku kuna kauli dhidi ya CUF zingine zikijenga chuki?

Kauli zinazopingana na kubadilika kila asubuhi ni dalili njema za kuchanganyikiwa.

Kila mtu na lake, kauli hazichujwi au kupimwa kwa matokeo mabaya!ni kusema tu ilimradi

Tusemezane
 
WACHAMBUZI WAMESAHAU HESABU ZA CCM!

UCHAGUZI WA MARUDIO HAUTAATHIRI KATIBA YA ZNZ


SUK INAWEZA KUUNDWA KATI YA CCM na ''KWAMTIPURA TEA PARTY''

Kwa hisani ya gazeti la Mwananchi Katiba yaiweka Zbar njia panda

Wachambuzi wana hofu na jinsi serikali ya SUK itakavyofanya kazi ikiwa CUF wametangaza kutoshiriki

Wachambuzi wanakariri vifungu vya katiba ya ZNZ vinavyonyesha ugumu kutengeneza SUK

Wanasema kufukuzwa kwa Hamad Rashid ADC, mtu anayeonekana 'angepachikwa' umakamu na pengine kupewa kakikundi ka wawakilishi kunazidisha ugumu

Washiriki akina Jaji Manento, Prof Sherrif na Mama Penina Mlama wanasahau jambo

CCM-ZNZ wanataka marudio ,wana uhakika CCM-Bara itakuja na 'zana zote muhimu'

Kushindwa CCM-ZNZ ni pressure iliyokuwepo bara hivyo 'kutosaidia' visiwani. hali imetulia

Hesabu za CCM ni kurudiwa uchaguzi tu. Serikali ya SUK itapatikana kwa njia rahisi sana

Uchaguzi utarudiwa kwa 'mchuano' mkali na vyama ambavyo leo hatujui hata majina

Namba zitafuata. CCM itashinda asilimia nyingi na vingine asilimia kidogo lakini muhimu.

Na chama pinzani kinaweza kushinda majimbo ya Pemba ili kujenga uhalali wa ushindi kuwa ilikuwa ngome ya CUF wananchi wameamua 'kuiadhibu' CCM kwa kumpa yayote

CCM ikipoteza viti 5, 'upinzani' utakuwa asilimia 10, makamu atapatikana na wawakilishi

Kulikuwa na plan A na B. Plan A ilikuwa kubakiza majina kama ilivyokuwa oktoba 25.

Kwa bahati mbaya likakwama na CUF wameshtuka mapema.
Pengine uhalali ungejengwa kwa uwepo wa majina ya CUF

Plan B ndiyo ni ya kutumia vyama tusivyojua halafu kupoteza majimbo 5 tu , SUK inakuja

Kwani SUK ni CCM na CUF tu? Hivi haiwezekani kuwa 'CCM na Jahazi asilia au Kwamtipura tea party'?

Wapo wenye namba, CCM imekamata calculator!

Tusezane
 
Katika pita pita zetu tumekutana na hiki file:///C:/Users/CEP/AppData/Local/Microsoft/Windows/INetCache/IE/ZVL554E5/Kanuni.pdf
Tunatumaini hili litakuwa toleo la mwisho kama ni sahihi.
Tunaomba masahihisho kwenye weledi kuhusu sharia ya mwisho kutumika kama ipo

Wanajamvi pitieni hapo kupata ufahamu wa nini kinaendelea Zanzibar

Tutajadili
 
MBINU ZIMEKWISHA, SASA NI UONGO BILA HAYA

WAZIRI: NCHI ZA AFRIKA ZINAKWENDA KUJIFUNZA YA JECHA

CCM-ZNZ WACHANGANYIKIWA


Polls observers: We won’t go to Zanzibar

Takribani magazeti yamemkariri waziri ofisi ya makamu wa pili wa Rais wa SMZ akizungumzia kura za marudio wiki ijayo

Waziri amefedheheka na taasisi, jumuiya na nchi za dunia kutopeleka waangalizi

Hizo n pamoja na taasisi za ndani chini ya CEMOT, EAC,AU,EU na nchi za magharibi

Katika 'kuchanganyikiwa', ametoa kauli ya kuhojiwa uwezo wake au sifa zake kielimu

1. Amesema kushiriki uchaguzi ni hiari hakuna anyelazimishwa.
Kwamba, tume ya ZEC ni huru. Alichosahau waziri, uchaguzi ulifutwa na Jecha si ZEC

Waziri amesahau, ZEC imelezimisha kuweka majina ili kukamilisha azma yao.

Hata wahusika walipopeleka barua, ZEC imekataa na kuwa majina yapo bila hiari.
Waziri anaposema ni hiari, ni ipi hiyo anayozungumzia mbali na ile ya ''ZEC huru''?

2. Katika kauli ya kushangaza, waziri anasema ilichokifanya ZEC ni halali na ndiyo maana nchi nyingi za Afrika zinapeleka watu Zanzibar kujifunza.

Waziri wa SMZ anaamini madudu yaliyokataliwa na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla, ni sehemu ya 'elimu' kwa nchi za Kiafrika.

Kwamba, wanaokwenda ZNZ ni kujifunza jinsi ya kufuta uchaguzi , Jecha n.k.
Kweli katika dunia hii lipo taifa linalojifunza haya ya CCM-Jecha na SMZ ?

Pengine wageni wanaokwenda ZNZ, asichojua waziri ni kujionea 'Maajabu'
kila mmoja angependa kushuhudia, kama wanaokuja kushangaa simba wanavyowinda.

Jumuiya ya Mataifa na taasis za ndani zimegoma kurudi Zanzibar kuona aibu ikitendeka

Kwamba, Jumuiya hizo kwenda kushuhudia ya ZNZ ni kujitoa ufahamu na kudharaulika.

Jambo hilo ni mwiba mkali kwa CCM, Zanzibar na Tanzania.
Kwa maneno mengine ZNZ inasusiwa,ambukizo litaikumba bara kama Tanzania.

Tutalipa gharama za kuendesha SMZ pale susio litakpo ng'ata

Walichokitaka CCM/ZEC ni uchaguzi wa marudio kuhalalisha matokeo wanayotaka wao
Dunia imekataa, kinachotokea CCM wamekuwa frustrated.

Waziri anaposema mataifa yametuma watu kujifunza ya Jecha, kama si kuchanganyikiwa ni kichekesho cha mwaka, aibu na tusi kwa Zanzibar!!

Tunauliza tena na tena, huyu ni waziri! Kama hawezi ''spinning'' hadi kusema ya Jecha ni somo zuuuri sana kuna walakini mkubwa. Waziri ana elimu gani ana ufahamu upi?

Tusemezane
 
MAONI

KAULI YA WAZIRI WA SMZ NI HATARI

INACHOCHEA HASIRA KWA WZNZ NA WATANGANYIKA


Waziri SMZ amekaririwa 'Znz ipo tayari kufa njaa kuliko kuwanyenyekea wazungu'

Kauli imekuja baada ya ''marudio ya kura' yaliyoacha makovu katika jamii ya WZNZ

Kwa miezi mitano hali ya kisiasa na kiuchumi ZNZ imeathiri maisha ya wananchi
Waathirika ni wa kipato cha chini ambao shughuli za kipato ziliathiriwa na siasa.

Biashara na shughuli za utalii zikakwama na kufanya maisha kuwa magumu

Waathirika ni wale wasio na account Uswiss, Ujerumani au kwingineko.
Ni wasioweza kununua aspirin kwani kwao ni bidhaa inayohitaji kutafuta kpato

Ni wale wasioweza kujiuguza India au Uingereza, kwao mardhi ni 'Tangazo la kifo'

Ungewauliza wanataka nini, kwao Amani ndicho kitu cha kwanza.
Wanajua kupitia Amani, heshima ,utu na ubinadamu wao unatimia kwa kiwango kikubwa.

Hawana habari nani anakaa hekalu gani, anakula biryani au anasaza makaimati. Wanachojua ni jua litoke na kuzama wakiwa salama

Uchumi wa ZNZ unategemea huduma za jamii kama Utalii na biashara.
Kuathirika kwa biashara na kuzorota huduma za jamii ni pigo kwa wananchi

Kauli ya kuwabeza wazungu inatia shaka. Lau kana mataifa hayo yasingekuwa na nguvu, waziri hakUwa na sababu za kuyaongelea.

Na wala mataifa ya Magharibi hayana sababu za kukaa kikao cha kujadili ZNZ.

Wanaweza kutafuta Kamba fupi na rahisi kufikia wanachokitaka.

Kwa mfano, wakitoa tahadhari ya usalama wa visiwani, biashara ya Utalii ambayo ni uti wa uchumi wa ZNZ itaathirika kikamilifu. Kauli kuhusu ZNZ inatosha kuumiza ZNZ

Kuanguka kwa utalii kuna athari katika kipato cha mwananchi na athari katika biashara

SMZ itakujikuta katika wakati mgumu katika kutoa huduma, kujiendesha na kutimiza malengo ya maendeleo. Kukiwa na mgawanyiko uliopo, hali itazidi kuwa mbaya

Mwisho wa siku atakayebeba mzigo ni mwananchi wa kawaida.
Mwananchi asiyeweza kukubaliana na waziri kuhusu ZNZ kufa njaa.

Hakukuwa na sababu ya ZNZ kufa njaa, kwanini wawekewe maneno ya kufa njaa?

Ni kikao gani cha wznz kimeazimia hayo?
Na mznz gani wa kufa njaa, mwenye account Uswiss au mfuma madema?

Athari za kipato kwa SMZ zitaathiri Tanganyika. Kwamba, huenda tukalazimika kuendesha serikali tatu kwa gharama za wananchi wa serikali moja.

Tunasema tatu kwa mantiki ya serikali ya ''Tanganyika'' kama ilivyo kwa miezi 5, serikali ya muungano baada ya mazingaombwe na SMZ

Mwananchi wa Iramba, Mtimbira, Isevya, Nakapanya, Najilinji,Magila, Kicheba na Katoma watalazimika kulipia gharama za SMZ ambayo viongozi wake wameamua ife njaa

Hili litachochea hasira pande mbili.

Upande wa Zanzibar kwenye moshi unaofuka na Tanganyika unaoona hauhusiki

Waznz walidharua Tanganyika katika marekebisho ya katiba ya 1984 marekebisho 2010
Ipo siku Watanganyika watakuwa na haki ya kuuliza, kwanini wabebe mzigo usiowahusu

Watahoji kama si ujinga kugharamia Zanzibar iliyoamua kufa njaa yenyewe
Watahoji kwanini walipe kodi kwa watu walio tayari kufa njaa

Tayari mgogoro umeppoteza pesa za millennium, waendelee kufa njaa kama wale walioamua kufa njaa kwa mapenzi yao? Kosa la Mtanganyika ni lipi hadi alipe gharama?

Hapo tutakuwa na tatizo jingine jipya

Tusemezane
 
Waziri wa SMZ alisema 'ZNZ wapo tayari kufa njaa'' kauli hiyo tulisema si njema. Leo tunaona tatizo linavyozidi kuwa kubwa
 
Wahafidhina wachache wametuweka 'rehani'
Tulionya, yanatokea sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…