Mitihani kidato cha sita 2013: Vurugu vurugu, wanafunzi waanza kelele.

Mitihani kidato cha sita 2013: Vurugu vurugu, wanafunzi waanza kelele.

tenende

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
6,511
Reaction score
505
Wanafunzi wa form six katika shule mbalimbali za sekondari wameanza kupiga kelele kutokana na mkanganyiko wa tarehe ya kufanya mtihani mwaka 2013. Ratiba ya BARAZA LA MITIHANI (NECTA) inaonyesha mitihani itafanyika mwezi wa 2, lakini WARAKA WA ELIMU NA. 5 WA MWAKA 2012 KUHUSU MAREKEBISHO YA MIHULA YA SHULE ZA SEKONDARI NA VYUO uliotolewa na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi mwaka huu inaonyesha mitihani ya kidato cha sita itafanyika mwezi mei, 2013. Hivi sasa taarifa hizi zinaenea kwa kasi miongoni mwa wanafunzi, vikao mashuleni kujadili hali hii, maswali mengi yakiulizwa na wanafunzi na waalimu kukosa majibu!. Hali hii inaweza kupelekea maandamano na vurugu kwa wanafunzi kuongezewa miezi mitatu ya masomo.
 
Huu ni utamaduni mpya, yaani waniongezee muda wa kupiga msuli niache kufurahi?
 
Sa hapo sijui inafuatwa ratiba ipi ila me naona hii ya necta ndio latest coz imesainiwa tar 21/09
 
Waraka kutoka Wizarani una nguvu kuliko hiyo ratiba kutoka NECTA, kwani NECTA ipo chini ya Wizara.
 
1
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: ELIMU DAR ES
SALAAM.
Simu: 2120402, 2120413,
2120403/4/ 5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz
Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na. OKE/NYE/VOL.I/20
S. L. P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 21/09/2012
Makatibu Tawala wa Mkoa,
Makatibu Tawala wa Wilaya,
Wakurugenzi; Halmashauri za Miji/Manispaa/Jiji,
Wakurugenzi Watendaji; Halmashauri za Wilaya,
Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda,
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya,
Wakuu wa Vyuo vya Ualimu,
Wakuu wa Shule za Sekondari,
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi.
TANZANIA BARA.
WARAKA WA ELIMU NA 5 WA MWAKA 2012 KUHUSU MAREKEBISHO YA
MIHULA YA SHULE ZA SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU

Tangu mwaka 2005, kumekuwepo na tatizo la kutofautiana kwa Mihula ya
wanafunzi wa Kidato cha Kwanza mpaka cha Nne, Kidato cha Tano na Sita na
Vyuo vya Ualimu. Aidha, kipindi cha kufanya mitihani ya Taifa katika kidato cha
Nne na Sita hutofautiana vilevile, usahihishaji wa mitihani ya ngazi hizo za elimu
umekuwa ukifanyika wakati baadhi ya makundi ya wanafunzi wakiendelea na
masomo Shuleni/Vyuoni.

Kitendo hicho, kimekuwa kikiathiri maendeleo ya wanafunzi kimasomo.
Wasahihishaji wa mitihani hiyo pia, wamekuwa na muda mrefu wa kufanya kazi
hiyo na kukosa muda wa kupumzika na kujikuta wanafanya kazi hiyo kwa
mfululizo mwaka mzima. Hali hiyo, imesababisha baadhi ya walimu kushindwa
kufanya kazi za kitaaluma ipasavyo kwenye vituo vyao.

Ili kurekebisha hali hiyo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeamua
kurekebisha Mihula ya shule, ili wanafunzi wa ngazi zote katika shule za
Msingi,Sekondari na Vyuo vya Ualimu wawe na vipindi vya likizo vinavyofanana.
Aidha, urekebishaji wa Mihula utaendana sambamba na marekebisho ya vipindi
vya mitihani ya Taifa katika ngazi hizo kama ifuatavyo:


2

A: MITIHANI YA TAIFA
NGAZI YA ELIMU AINA YA MTIHANI
MUDA WA MITHANI
2012 Kuanzia 2013
Elimu ya Msingi
Darasa la 7
Mtihani wa kumaliza
Elimu ya Msingi(PSLE)
Septemba
Wiki ya 2
Septemba Wiki ya
2
Elimu ya
Sekondari Kidato
cha 4
Mtihani wa Kidato cha
4 (CSEE)
Oktoba Wiki
ya 2
Novemba Wiki ya
1
Elimu ya
Sekondari Kidato
cha 6
Mtihani wa Kidato cha
6 (ACSEE)
Februari Wiki
ya 2
Mei Wiki ya 1
Elimu ya Ualimu,
Stashahada na
Cheti
Mtihani wa Ualimu wa
Stashahada ya Elimu
(DSEE) na Mtihani wa
Ualimu Daraja la IIIA
(GATCE) na Mtihani wa
Ualimu Daraja la III A
Kozi maalum
(GATSCCE)
Mei Wiki ya 1 Mei Wiki ya 1
B: MIHULA YA SHULE/VYUO VYA UALIMU
NGAZI YA
ELIMU
MUDA WA MASOMO
2012 Kuanzia 2013
MUHULA
WA I
MUHULA WA 2 MUHULA WA
1
MUHULA WA 2
Kidato cha 1-4 Januari Wiki
ya 1 -Juni
Wiki ya 1
Julai Wiki ya 1-
Desemba Wiki ya
1
Januari Wiki ya
1 -Juni Wiki ya 1
Julai Wiki ya 1-
Desemba Wiki ya
1
Kidato cha 5-6 April Wiki ya
1- Septemba
Wiki ya 1
Septemba Wiki
ya 1 -Februari
Wiki ya 1
Julai Wiki ya 1-
Desemba Wiki
ya 1
Januari Wiki ya 1-
Juni Wiki ya 1
Ualimu
Stashahada na
Cheti
Julai Wiki ya
2-Desemba
Wiki ya 2
Januari Wiki ya 1-
Juni Wiki ya 1
Julai Wiki ya 1 –
Desemba Wiki
ya 1
Januari Wiki ya 1
-Juni Wiki ya 1
3
Tanbihi: Wanafunzi wote watapumzika Mwezi Juni na Desemba.
Waraka huu, unaanza kutumika tarehe 01 Januari, 2013 na kufuta Waraka wa
Elimu Na. 5 wa Mwaka 2004.
Prof. E.P. Bhalalusesa
KAMISHNA WA ELIMU
Nakala:
Katibu Mkuu.
OWM TAMISEMI,
S.L.P. 1923,
DODOMA.
Mkurugenzi,
Taasisi ya Elimu na Watu Wazima,
S.L.P. 20679,
DAR ES SALAAM.
Mkurugenzi,
Taasisi ya Elimu Tanzania
S.L.P. 35094,
DAR ES SALAAM.
Katibu Mtendaji,
Baraza la Mitihani la Tanzania,
S.L.P. 2624,
DAR ES SALAAM.
 
Hapo umenena vema mkuu!. Nimepita pita katika ofisi hizi leo na kuthibitisha mabadiliko haya yanaanza na form six hawa tulionao!.

Waraka kutoka Wizarani una nguvu kuliko hiyo ratiba kutoka NECTA, kwani NECTA ipo chini ya Wizara.
 
MIHULA YA SHULE YA HIGH SCHOOLS
MUHULA WA I: Julai Wiki ya 1Desemba Wiki ya1
MUHULA WA II: Januari Wiki ya 1Juni Wiki ya 1 (FORM SIX - MAY).
 
LIKIZO O-LEVEL NA A-LEVEL: Wanafunzi wote watapumzika Mwezi Juni na Desemba.Waraka huu, unaanza kutumika tarehe 01 Januari, 2013 na kufuta Waraka wa
Elimu Na. 5 wa Mwaka 2004.
 
SABABU ZILIZOLETA MABADILIKO
WARAKA WA ELIMU NA 5 WA MWAKA 2012 KUHUSU MAREKEBISHO YA
MIHULA YA SHULE ZA SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU
1. Tangu mwaka 2005, kumekuwepo na tatizo la kutofautiana kwa Mihula ya
wanafunzi wa Kidato cha Kwanza mpaka cha Nne, Kidato cha Tano na Sita na
Vyuo vya Ualimu.

2.
Aidha, kipindi cha kufanya mitihani ya Taifa katika kidato cha
Nne na Sita hutofautiana vilevile, usahihishaji wa mitihani ya ngazi hizo za elimu
umekuwa ukifanyika wakati baadhi ya makundi ya wanafunzi wakiendelea na
masomo Shuleni/Vyuoni.
3. Kitendo hicho, kimekuwa kikiathiri maendeleo ya wanafunzi kimasomo.
4. Wasahihishaji wa mitihani hiyo pia, wamekuwa na muda mrefu wa kufanya kazi
hiyo na kukosa muda wa kupumzika na kujikuta wanafanya kazi hiyo kwa
mfululizo mwaka mzima. Hali hiyo, imesababisha baadhi ya walimu kushindwa
kufanya kazi za kitaaluma ipasavyo kwenye vituo vyao.
Ili kurekebisha hali hiyo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeamua
kurekebisha Mihula ya shule, ili wanafunzi wa ngazi zote katika shule za
Msingi,Sekondari na Vyuo vya Ualimu wawe na vipindi vya likizo vinavyofanana.
 
Najua wanafunzi wengi mmeumia saana kwa taarifa ya mabadiliko haya. Lakini mjue miezi mitatu si mingi sana. Nawashauri wanafunzi woote wa kidato cha sita msivunjike moyo. Vumilieni. Endeleeni kujiandaa zaidi ya vile mlivyokuwa mmejipanga awali. Kuacha kusoma hakutakuwa na manufaa kwenu!.
 
usishangae wale bording school wakaambiwa waongeze hela kwa hiyo miezi mitatu!
 
Bado inatuchanganya kwa kweli sisi ambao tupo form six mwaka huu kwa sababu hata wakuu wetu wa shule wapo pia kwenye sintofahamu kama inaanza na sisi au hawa walio nyuma yetu.
 
Sintofahamu inatoka wapi wakati waraka wa Naamani or sorry wa wizara unataja mwaka 2013
Kwa mwanafunzi ambaye amekuja kusoma kwake ni furaha as you have more time to study na haujastukizwa waraka umetoka 5month before iyo Feb
Ila kwa wanafunzi ambao wamekuja shule kukua wao kwao kumaliza shule ni muhimu kuliko suala la unamalizaje shule ie Matokea
 
niulize swali je vyuo navyo si watachelewa fungua maana matokeo yatachelewa toka
 
niulize swali je vyuo navyo si watachelewa fungua maana matokeo yatachelewa toka
Mitihani ikifanyika mwezi wa tano, usahihishaji mwezi wa sita, matokeo mwezi wa saba, application mwezi wa nane, na kujiunga vyuo vikuu itakuwa septemba mwishoni na oktoba mwanzoni.
 
Back
Top Bottom