Mitihani ya darasa la SABA kuanza Jumatano

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
WANAFUNZI wa Darasa la Saba wanatarajiwa kuanza mtihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi kuanzia Jumatano ya wiki hii.
Mitihani hiyo inatarajiwa kufanyika kwa muda siku mbili ambapo humalizika Alhamisi nchini kote
Jumla ya Shule zipatazo
15,677 za umma na binafsi zinatarajiwa kutoa wanafunzi wapatao 868,030 watakaofanya mitihani hiyo.
Kati yao wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili ni 844,810 na wale watakaofanya kwa lugha ya Kiingereza ni 22,535.
===

...kutoka mikoani:

"ZAIDI ya wanafunzi 200 wa darasa la saba kutoka shule mbalimbali za msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, hawajui kusoma na kuandika.
Ofisa elimu shule za msingi wilayani hapa, Gideon Mwesiga, alitoa kauli hiyo juzi kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika mjini Kayanga.
Alisema jumla ya wanafunzi watahiniwa katika mtihani wa darasa la saba mwaka 2013 ni 13,863, ambapo kati yao 264 hawajui kusoma na kuandika.
Alisema idadi hiyo ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika ni changamoto kubwa ya maendeleo katika uboreshaji wa taaluma ya wanafunzi kwa masilahi ya taifa.
Aidha, alisema wilaya hiyo ina upungufu wa vyumba vya madarasa 857, wakati vilivyopo ni 872 na vinahitajika 1,729 katika shule za msingi 212 huku nyumba za walimu zikiwa na upungufu, zilizopo ni 309 na kuwa zinahitajika 1,758.
Alieleza kuwa mikakati mbalimbali ya kuboresha kiwango cha elimu kwa Wilaya ya Karagwe na Kyerwa imewekwa na kamati ya elimu, afya na maji ya baraza la madiwani kupitia halmashauri ya wilaya ili kuinua kiwango cha ufaulu.
Diwani wa Kibare, Elias Duda, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na maji, alisema wanafunzi wa kidato cha pili ambao hawatafikisha alama 30 hawataruhusiwa kuingia kidato cha tatu.

Source: freemedia
===
http://m.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/15019-mbatia-aibua-madudu-mitihani-darasa-la-7
 
Mbatia aibua madudu mitihani darasa la 7

Asante kwa taarifa. Lakini hauna maana yoyote kwa vile wote wanakwenda shule za Kata with an exception of those few who will be selected to join Ilboru, Kibaha, Kilakala, Msalato and the like. Otherwise business as usual!
 
Nategemea majanga mengine frm this Ministry...bt wish the best 4 all candidates
 
Nawatakia mtihani mwema maana wote tumetoka huko.
 
Mitihani ilikuwa zamani!siyo cku hizi! Bestwishes kwao!
 
Back
Top Bottom