Mitihani ya mwaka wa 5 udakitari yarudiwa upya baada ya wanafunzi kufaulu wote mhimbili

MissM4C

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2012
Posts
1,740
Reaction score
1,005
wAKUU heshima kwenu....

JUzi ilifanyika mitihani ya kwa wanafunzi wa mwaka 5 udaktari, baada ya kusahihishwa wanafunzi wote walioonekana kufaulu tena kwa wastani mkubwa, jambo ambalo lilimfanya mkuu wa isara husika professa lutale kuuufuta na kuamua kutunga mtihani mwingine kwani kwa madai yake anasema haiwezekani wanafunzi wote wafaulu kwani idara yake ndio inaongoza kwa kufelisha wanafunzi na discontinuation kila mwaka,,, huyu mama(prof. lutale, mhaya) imekuwa ni kawaida kwake kuona wanafunzi wakifeli na kurudi kufanya sup au kupata disco kila mwaka,,, wanaharakati tusaidieni wanafunzi wa mhimbili,,, hawa walimu wetu wamejigeuza miungu.
 
Anyway yawezekana, lakini ukifika mwaka wa 5 huwa hakuna disco, nambie nani aliyewahi kudisco. Ukifika clinical mdogo wangu huwezi dico tena, may be sheria zimebadilika coz Muhas sasa kipo kipo tu kiungozi. Kwani mkifaulu written si bado kuna clinical exam nazo mmefulu pia. Kitu kingine hadi sasa ninavyofahamu ndo group moja tu limeshapita bado kuna makundi mawili bado, afu huo mtihani ni UE AU CA. coz kama ue mtapata wapi muda wa kurudia wakati mnatakiwa kuanza rotation nyingine, yawezekana pia mmeiba mtihani pia. Jibu maswali yangu. Otherwise malalamiko yako si ya kweli.
 
ila wangefeli wote angerudia kutunga upya au angeona hiyo ni sawa?
 
kwa hili wanafunzi wana kosa gani hadi walazimishwe kurudia???
 
May be kutrend ya kuibia mitahani. Ni vizuri kwa udaktari ukatoka uko competent kuliko kwenda kuchezea maisha ya watu.
 
Prof. ana uelewa wa wanafunzi wake. huenda the way walivyojibu ikaonekana kuwa waliiba mtihani. Haiwezekani akajitesa kutunga mtihani mwingine. kwanza nia yake atoe wanafunzi hodari
 
Prof. ana uelewa wa wanafunzi wake. huenda the way walivyojibu ikaonekana kuwa waliiba mtihani. Haiwezekani akajitesa kutunga mtihani mwingine. kwanza nia yake atoe wanafunzi hodari

hivi wagonjwa wakipona/wakifa wote ana review prescription/medical examination/investigation?!
 
hivi lengo la mtihani uwa ni watu wa fail au ni kupima kiwango cha uelewa wa mwanafunzi?
Kama lengo ni kufail hapo sawa
 

Ndio Kashawaambia mrudie..Kwa Mwalimu Mwenye Uelewa Kama wake...Sidhani kama ni mjinga kujisumbua kurudia mtihani alioutunga mwenyewe. Walimu wa chuo wenye weredi kutunga mitihani kwa ajiri ya supplementary is the last thing they wanna do.

Soma kama ulifauru kwa uelewa wako utafauru tena.
 
na huo wa pili siwapatii picha wadogo zangu...mtafeliiiii mpaka mumjue ni nani!!!
 
waambie wadada wenu waache kumsarandia mumewe!!
 
hivi wagonjwa wakipona/wakifa wote ana review prescription/medical examination/investigation?!

kwa taarifa nilizopata ni kwamba madogo walikuwa na marking scheme ya huo mtihani. Mtihani wenyewe ulirudiwa wa group iliyopita na walifanyiwa masahihisho hivyo kuna watu walichomoka na marking scheme wakaenda kuitoa copy na kurudisha original. Huwa wanaasume kwamba pepa ikishakusanywa hakuna mwanafunzi anabaki nayo. Yawezekana ameshtuka baada ya kulinganisha marks za theory na clinical na kuona kuna variation kubwa.
 
kwa ujumla wahadhiri wa tanzania kwao sifa ni kufelisha
wakati wahadhiri wa nchi za wenzetu mwanafunzi akifeli anawekwa kitimoto na hata kushushwa daraja.
nawashangaa wafrika tuna uroho wa kwanini watu wafaulu wakati nae kafaulu ndio kafika hapo alipo.
Yuko Prof mmoja wanafunzi walisha mnyonga na kumwacha kwenye gari lake kwa hasira ya kuwaharibia maisha.
 

mleta mada ana majungu, licha ya internal medicine kuongoza kwa kukamata wanafunzi lutale siyo mkamataji. Kuna watu wake wako ile department kama komba, matuja, munseri, loh! Hawa watu ni balaa! Mama anakuwaga fair sana, hata walioshikwa mara nyingi na wengine huwa wanakimbilia kwake. Hapo amelinganisha mtihani wenu wa theory na clinical ameona ni mbingu na dunia! Haiwezekani mtu mmoja clinical ambayo ndo inatoaga watu upate 10/40 aafu theory upate 90 na siyo mmoja tu aliyepata hivyo.
 
Huenda waliiba mitihani...Pale Muhas wizi wa mitihani ni jambo la kawaida...Kwani nakumbuka hao hao mwaka wa Tano wa sasa pindi wakiwa mwaka wa Pili waliiba paper ya Pathology ngoma ikashtukiwa Dr. vuhahula akabadilisha paper asubuhi na paper ilikuwa ngumu balaa...Huenda paper ilivuja na Pro. akastukia ishu..
 
Mkuu, piga kitabu utoke. Unataka wanaharakati wakufanyie mtihani?
 

Kweli mjasiri haachi asili...Hawa hawa ndo waliiba paper ya Pathology wakiwa mwaka wa pili nakumbuka sana na paper ikabadilishwa asubuhi asubuhi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…