Mitihani ya sets inaharibu elimu nchini

Mitihani ya sets inaharibu elimu nchini

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Miaka ya hivi karibuni, kumeibuka mitihani ya sets kwa madarasa ya mitihani.

Mitihani hii inaonekana kuwa ndo suluhu ya kufelisha watoto kwenye mitihani ya kitaifa, walianza taasisi binafsi na hivi karibuni shule za serikali zimefuata.

Tatizo la hii mitihani, imejikita kubahatisha maeneo muhimu ya mitihani ya taifa, hivyo mwanafunzi akiwabahatisha vizuri NECTA, ndiye anaonekana giant wa taifa.

Ukweli ni kwamba, tumeachana na ufundishaji wa utulivu unaozingatia UMAHIRI/COMPETENCE, Mitaala ya elimu inazingatia SERA ZA ELIMU NCHINI, na sera ya elimu hailengi kufauli kwenye mitihani bali kwenye UMAHIRI.

UMAHIRI ndiyo unafanya kuwa na wasomi wenye kufikili KIMANTIKI, WENYE KUTATUA CHANGAMOTO ZAO WAO WENYEWE.

Mitihani ya sets inawafanya walimu kujikita kutafuta mbinu za kujibu mitihani tu, hamna UMAHIRI WOWOTE.

tamisemi liangalieni hili maana nyinyi ndio mnashinikiza ufaulu wa watoto kwenye mitihani na mmekuwa mkienda kinyume na malengo ya elimu nchini hata mitaala. Msifuate matamanio ya kisiasa, zingatieni utaalamu.
 
Miaka ya hivi karibuni, kumeibuka mitihani ya sets kwa madarasa ya mitihani. Mitihani hii inaonekana kuwa ndo suluhu ya kufelisha watoto kwenye mitihani ya kitaifa, walianza taasisi binafsi na hivi karibuni shule za serikali zimefuata. Tatizo la hii mitihani, imejikita kubahatisha maeneo muhimu ya mitihani ya taifa, hivyo mwanafunzi akiwabahatisha vizuri NECTA, ndiye anaonekana giant wa taifa. Ukweli ni kwamba, tumeachana na ufundishaji wa utulivu unaozingatia UMAHIRI/COMPETENCE, Mitaala ya elimu inazingatia SERA ZA ELIMU NCHINI, na sera ya elimu hailengi kufauli kwenye mitihani bali kwenye UMAHIRI.
UMAHIRI ndiyo unafanya kuwa na wasomi wenye kufikili KIMANTIKI, WENYE KUTATUA CHANGAMOTO ZAO WAO WENYEWE.
Mitihani ya sets inawafanya walimu kujikita kutafuta mbinu za kujibu mitihani tu, hamna UMAHIRI WOWOTE.
tamisemi liangalieni hili maana nyinyi ndio mnashinikiza ufaulu wa watoto kwenye mitihani na mmekuwa mkienda kinyume na malengo ya elimu nchini hata mitaala. Msifuate matamanio ya kisiasa, zingatieni utaalamu.
Mitihani ya sets unamaanisha nini
 
Ajabu hiii unaleta mada unashindwa kuwaelesha watu vzuri, kwanza ungesema hio mitihani ya sets ni nini na ipoje
 
Mbaya kabisa wanaweka somo moja la kiswaz. Mtu anapata c moja na miswaka yote
 
Mitihani ya SETs ndio takataka gani?
Umeandika kitu kama upo darasani na wanafunzi wenzako
Fafanua unamaanisha nini?
Toa habari isiyoacha maswali ya Msingi nyuma au baada ya kathread kako
 
Hata kama lengo la set na kufaulu mitihani..ni bora zaidi sasa tutaotaje mainginia kama sio kufaulu mitihani?.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mitihani ya sets unamaanisha nini
Ingawa mtoa mada atakuja pia kujibia hili, ila ninavyofahamu mimi;

Mitihani ya sets anamaanisha ile mitihani ya majaribio inayotayarishwa na Mamlaka ya serikali za Mitaa kwa Ngazi ya Wilaya na Mikoa chini ya Wakurugenzi na Maafisa Elimu Wilaya na Mikoa kwa ajili ya wanafunzi hasa katika Shule za Msingi na Sekondari hadi kidato cha 4.

Ni mitihani ambayo inatayarishwa na watu fulani ama kununuliwa na viongozi kutoka wanapopajua wao na kuelekeza mitihani hiyo wafanye wanafunzi katika shule zote za Wilaya ama Mkoa. Lengo kuu ya mitihani hiyo ni kuongeza uwezo kwa wanafunzi kujibu maswali ya mitihani ili kuondoa aibu kwa mkoa kwenye ZERO. Iliwnza na ile kampeni ya 'Tokomeza Zero Mashuleni'. Kwa hiyo, imelengw zaidi kumkaririsha mtoto majibu ya maswali mbalimbali na sio Competence / Ujuzi na maarifa yaliyolengwa kwenye mtaala husika.
 
Mitihani ya SETs ndio takataka gani?
Umeandika kitu kama upo darasani na wanafunzi wenzako
Fafanua unamaanisha nini?
Toa habari isiyoacha maswali ya Msingi nyuma au baada ya kathread kako
Mitihani ya sets ni mitihani inayoandaliwa na watu binafsi au kuchukua mitihani ya maeneo tofauti tofauti, wanafunzi hufanya kwa mfululizo kwa mpangilio Kama series.
 
Ingawa mtoa mada atakuja pia kujibia hili, ila ninavyofahamu mimi;

Mitihani ya sets anamaanisha ile mitihani ya majaribio inayotayarishwa na Mamlaka ya serikali za Mitaa kwa Ngazi ya Wilaya na Mikoa chini ya Wakurugenzi na Maafisa Elimu Wilaya na Mikoa kwa ajili ya wanafunzi hasa katika Shule za Msingi na Sekondari hadi kidato cha 4.

Ni mitihani ambayo inatayarishwa na watu fulani ama kununuliwa na viongozi kutoka wanapopajua wao na kuelekeza mitihani hiyo wafanye wanafunzi katika shule zote za Wilaya ama Mkoa. Lengo kuu ya mitihani hiyo ni kuongeza uwezo kwa wanafunzi kujibu maswali ya mitihani ili kuondoa aibu kwa mkoa kwenye ZERO. Iliwnza na ile kampeni ya 'Tokomeza Zero Mashuleni'. Kwa hiyo, imelengw zaidi kumkaririsha mtoto majibu ya maswali mbalimbali na sio Competence / Ujuzi na maarifa yaliyolengwa kwenye mtaala husika.
Ahsante kwa kunisaidia kufafanunua, nadhani imeeleweka
 
Sasa wasipopimwa kwa mitihan wapimwe kwa kitu gani unataka mkuu?

Kikubwa hizo unazoziita seti zizingatie ubora wa utungaji na kukover mada zote kulingana na mtaala

Usilaumu seti kinachitakiwa mtaala wetu ubadirishwe tuachane na mambo ya mitihani
 
Ingawa mtoa mada atakuja pia kujibia hili, ila ninavyofahamu mimi;

Mitihani ya sets anamaanisha ile mitihani ya majaribio inayotayarishwa na Mamlaka ya serikali za Mitaa kwa Ngazi ya Wilaya na Mikoa chini ya Wakurugenzi na Maafisa Elimu Wilaya na Mikoa kwa ajili ya wanafunzi hasa katika Shule za Msingi na Sekondari hadi kidato cha 4.

Ni mitihani ambayo inatayarishwa na watu fulani ama kununuliwa na viongozi kutoka wanapopajua wao na kuelekeza mitihani hiyo wafanye wanafunzi katika shule zote za Wilaya ama Mkoa. Lengo kuu ya mitihani hiyo ni kuongeza uwezo kwa wanafunzi kujibu maswali ya mitihani ili kuondoa aibu kwa mkoa kwenye ZERO. Iliwnza na ile kampeni ya 'Tokomeza Zero Mashuleni'. Kwa hiyo, imelengw zaidi kumkaririsha mtoto majibu ya maswali mbalimbali na sio Competence / Ujuzi na maarifa yaliyolengwa kwenye mtaala husika.
Sets = ...............?
.[Tupe kirefu chake]
 
Mitihani ya sets ni mitihani inayoandaliwa na watu binafsi au kuchukua mitihani ya maeneo tofauti tofauti, wanafunzi hufanya kwa mfululizo kwa mpangilio Kama series.
Safi sana
Mitihani hii ipo pia kwenye level ya shule za msingi?
Wewe una connection nayo???
 
Watu wana mbinu za kuleta matangazo huu
Kiongozi lete connection sisi wa mbwinde tupate tuwape wanafunzi na watoto wetu
Mjini vijana mnatumia zaidi ya akili kuleta matangazo
Kweli hii ni great sinkers
 
Elimu Bure maana yake kila mtoto afike Chuo.

Mwisho tunakuwa na taifa la vilaza
 
Labda kama utakuwa unamaanisha SATs
Standard Assessments Tests
Huu ni mfumo wa elimu ya UK na labda kwingineko
Yaani inakuwa matokeo ya darasa au level iliyopo haya aamuliwi na mtihani wa mwisho wa kuvuka wa darasa au level yaani mfano kutoka Darasa la kwanza kwenda la pili au kutoka Primary kwenda Secondary...
Ufaulu wako unaamuliwa na mitihani midogo na course work zote ulizofanya mwaka mzima wa darasa au level yote kutoka la kwanza mpaka la saba au form 1 mpaka form 4..
 
Siyo hivyo ndugu, Kama haupo idara ya msingi au secondary huwezi kuelewa Sana, wahusika wananielewa Sana. Yaani kwa madarasa ya mitihani, hivi sasa wanaendelea na mitihani ya kununua inayoandaliwa na wataalamu fulani, siwezi kuwaharibia soko lao kwa kuwataja lakini siyo kosa lao maana ndiyo matamanio ya TAMISEMI kufaulisha watoto wengi. Shida inakuja, tumeacha kujikita kuandaa Vijana wenye maarifa tarajiwa na ujuzi,badala yake imebidi shule ziitazame mitihani. Natumai hata waandaa mitaala haiwavutii Sana lakini hawezi kuzuia kwasababu imekuwa ni fashion kufaulisha mitihani kuliko kuangalia competence kwa watoto
 
Mtoa mada hujui unachoraumu kipi, nadhani hoja yako ilipaswa iwe zidi ya mfumo wa Elimu na si mitiahini sijui ya Sets ikiwa mitihani yote ina formality ileile.

Kimsingi hujaijua hoja yako
 
Mitihani ya sets ni mitihani inayoandaliwa na watu binafsi au kuchukua mitihani ya maeneo tofauti tofauti, wanafunzi hufanya kwa mfululizo kwa mpangilio Kama series.
Kama ni mitihani inayoandaliwa kupima wanafunzi inauaje elimu?
Ebu jazia nyama kidogo mwanafunzi akipewa mtihani inaathili vipi uwezo wake kitaaluma?
 
Back
Top Bottom