MITIHANI yaibwa UDSM

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Katika hali isiyo ya kawaida,karatasi za majibu za wanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya Kwanza ya Sheria wa UDSM zimeibwa zikiwa kwa Mhadhiri wa somo. Karatasi hizo za somo la Legal Drafting,zimeibwa toka kwa Dr. Ringo Tenga,Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Sheria-UDSM.

Ingawa Utawala wa Kitivo unafanya siri juu ya jambo hilo,taarifa za uhakika zinadai kuwa karatasi za majibu za mtihani husika zimeibwa. Alama kwa wanafunzi wote wa mwaka wa tatu haziwezekani kupatikana.Hivyo,wanafunzi husika watatakiwa kufanya tena mtihani wa somo tajwa. Hadi sasa,Kitivo hakijapanga tarehe ya kufanyika kwa mtihani huo.

Je,ni halali mambo haya kuwa hivi?
 
Walijua watadsco kwenye hiyo paper ndo wamecheza game ili warudie
 
Halali kwa jambo lipi? Umetaja mambo matatu ambayo yote yamekushangaza

la kwanza, ni majibu ya mitihani kuibiwa
la pili, kwa Kitivo cha sheria kufanya siri juu ya jambo hili
la tatu, Wanafunzi husika kutakiwa kurudiwa mtihani

Sasa unataka ujibiwe lipi hapo Mzee tupatupa?
 
Mkuu wangu,ni yote matatu
 
Hakuna kitu kibaya kwa Mhadhiri kama 'kupoteza' karatasi za mtihani!
 
Mkuu wangu,ni yote matatu

la kwanza; wizi ni wizi tu kama ajali...sio halali lakini ndio hali ilivyo
la pili: Ni halali kuficha ili wajipange kwakuwa..labda hawana uhakika kama ni kweli imeibwa ama la
La tatu; ni halali kwa wanafunzi husika kurudi na kufanya mitihani upya..
Vinginevyo itakuwa ngumu kupima matokeo ya watahiniwa hao wa somo hilo bila kipimio hiki cha mtihani!!
 
mhhhhhhh....hapo linalofwata litakua lijiwe hata zaid ya waliloiba.....
 
..Tatizo UDSM wanabana sana, hasa kwa kitivo cha sheria. Mimi sio shabiki wa kulegezea wanafunzi kama vyuo vingine vinavyofanya, lakin kwa UDSM, baadhi ya idara imekuwa kero kubwa sana. Watu wenyewe wavivu kufundisha, kutwa kucha wako kwenye mambo yao, halafu bado wanabana.

Inabid watanzania tubadilike, elimu sio huduma tu kama ilivyokuwa zamani- ni biashara pia. Wahadhiri, chonde wajali wateja wenu!
 
Hao wanafunzi wa UDSM si wanajiita 'Gifted' warudie pepa. Acha vilaza wa vyuo vya kata tulalamikie kurudia pepa. Haf nimekuwa nikidhani kuwa kwa kuwa dsm kina higher ranks tz n.k. then kina wahadhiri makini..,sasa kama wahidhiri hao ndo wanaopoteza scripts sijui huku kwenye vyuo vyetu vya kata hali ikoje. Naomba kuwasilisha.
 
sheria za chuo husika kuhusu mitihani kuibiwa zinasemaje?
rudi kwenye bylaws utajua kama ni halali au haramu
kidumu chama cha mapinduzi - ah sory cha wizi wa matokeo
tatizo walijua ni matokeo ya kura za uchaguzi maana ndo walizozoea kuiba
 
Umevujisha siri.Wangeweza kupewa hata za mezani kwa kuangalia 'course work' zao.
 

baba T a.k.a Dr.Tenga,mvivu wa kumark pepa,fix izo,hapo kashndwa ku meet deadlyln...! Poleni LL.B 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…