Ntiyakama
Member
- Sep 19, 2021
- 32
- 37
Saratani ya matiti hutokea zaidi kwa wanawake, ingawa WANAUME pia wanaweza kuipata. Watu wengi hawafahamu kama wanaume pia wanayo matiti hivyo wanaweza kupata saratani ya matiti (American Cancer Society, 2020).
Andiko hili litaeleza zaidi kuhusu SARATANI YA MATITI; ni nini, mitindo gani ya maisha inaweza kupelekea saratani hii, sababu hatarishi zisizo na madhara wazi juu ya saratani ya matiti na njia zinazoweza kupunguza hatari ya kupata saratani hii.
SARATANI YA MATITI;
Saratani ya titi ni ugonjwa ambao husababisha seli katika tishu ya titi kubadilika na kukua kusiko ratibika (kuliko pindukia/ kusiko ratibiwa / ovyo ovyo) ambapo hupelekea kutokea kwa donge au uvimbe kwenye titi.
Mara nyingi hii hutokea kwenye tezi zinazozalisha maziwa (lobules/milk glands) au katika mirija inayounganisha tezi hizo na chuchu ya titi.
SABABU HATARISHI ZITOKANAZO NA MITINDO YA MAISHA.
Sababu hatarishi ni kitu chochote kinachoweza kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa flani, kama vile saratani ya matiti.
Ingawa si kila uwepo wa sababu hatarishi unamaanisha kuwa lazima utapata ugonjwa, hapana. Zifuatazo ni sababu hizo.
1. UNYWAJI POMBE
Unywaji pombe unahusishwa moja kwa moja na ongezeko la hatari ya kupata saratani ya matiti. Hatari huongezeka sambamba na kiwango cha matumizi ya pombe.
Wanawake wanaokunywa pombe mara moja kwa siku wana ongezeko la 7%-10% ya hatari ya kupata saratani ya matiti wakilinganishwa na wasiotumia kabisa pombe, ni zaidi kwa wanawakewanaokunywa pombe mara 2 hadi 3 kwa siku, hawa wana 20% zaidi ya hatari yakupata saratani hii wakilinganishwa na wasiotumia pombe (American Cancer Society, 2020).
Si saratani ya matiti pekee, pombe inahusishwa na ongezeko la hatari ya kupata saratani nyinginezo pia. Ni bora zaidi kuacha kabisa unywaji pombe.
2. KUWA NA UZITO ULIOPITILIZA
Uzito uliopitiliza hasa baada ya ukomo wa hedhi (menopause) unaongeza uwezekano wa kupata saratani ya matiti.
Kabla ya ukomo wa hedhi ovary za mwanamke hutengeneza homoni nyingi zaidi ya estrogen na nyingine kidogo hutoka kwenye hifadhi ya mafuta mwilini (fatty tissue).
Baada ya hedhi kufika ukomo (ambapo ovary zinasimama kuzalisha estrogen) estrogen nyingi huanza kuzalishwa kutoka katika hifadhi ya mafuta iliyopo mwilini.
Kuwepo kwa mafuta mengi mwilini baada ya ukomo wa hedhi huongeza kiasi cha estrogen inayozalisha ambayo hupelekea ongezeko la uwezakano wa kapata saratani ya matiti.
Wanawake wenye uzito uliopitiliza pia huwa na kiwango kikubwa cha insulin homoni; kiwango kikubwa cha insulin homoni mwilini kinahusishwa na ongezeko la uwezekano wa kapata saratani.
3. KUTOFANYA MAZOEZI
Tafiti zinathibitisha kuwa shunguli za miili zilizo katika mfumo mzuri hupunguza uwezekano wa kupata saratani ya matiti, hasa kwa wanawake waliofikia ukomo wa hedhi.
Swali la msingi linaweza kuwa ni kwa kiasi gani shughuli / mazoezi yanahitajika?. Baadhi ya tafiti zimebainisha kuwa mazoezi kidoogo tu hata kwa masaa mawili kila wiki yanaweza kusaidia, ingawa zaidi ya hapo inaonekana kuwa nzuri zaidi.
Haswa ni kwa namna gani mazoezi yanaweza kupunguza uwezekano wa kupata saratani, haifahamiki bado, ingawa yanahusishwa pia na uzito wa mwli, homoni na msawazo wa nguvu katika mwili.
Taasisi ya American Cancer Society inapendekeza kuwa, mtu mzima apate dakika 150 hadi 300 za kufanya mazoezi ya kawaida au dakika 75 hadi 150 za kufanya mazoezi ya nguvu kila wiki. (au yote kwa pamoja) kufanya zaidi ya hapo pia ni salama.
4. KUTO KUZAA KABISA
Wanawake ambao wanaamua kuto kuzaa kabisa au wanao pata zao la kwanza baada ya umri wa miaka 30, kwa kiasi wanalo ongezeko la uwezekano wa kupata saratani ya matiti.
Kuzaa watoto wengi na kupata ujauzito katika umri wa mapema hupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti.
5. KUAMUA KUTO KUNYONYESHA
Tafiti nyingi zinabainisha kuwa kunyonyesha kunapunguza kwa kiasi hatari ya kupata saratani ya matiti hasa kunapoendelezwa kwa mwaka na zaidi.
Maelezo kuhusu hili inaweza kuwa kunyonyesha kunampunguzia mwanamke idadi ya mizunguko ya hedhi katika kipindi chote cha maisha yake (kama ilivyo kwa mwanamke aliyeanza hedhi mapema zaidi na aliyechelewa kufikia ukomo wa hedhi).
6. NJIA ZA KUPANGA UZAZI
Baadhi ya njia za kupanga uzazi hutumia homoni, ambazo zinaweza kuwa na mchango mkubwa kwenye ongezeko la hatari ya kupata saratani ya matiti.
• Vidonge (Oral contraceptives),
Tafiti zinabainisha kuwa wanawake wanaotumia vidonge vya kupanga uzazi wanaongezeko la hatari ya kupata saratani ya matiti kuliko wanawake wasio tumia dawa hizo.
Mtumiaji atakapoamua kusitisha matumizi ya vidonge, hatari hii huendelea kuwepo kwa mpaka miaka 10 zaidi kisha kuludi katika hali yake
Sindano (Birth control shot):
• Depo-Provera,
Ni homoni (progesterone) inayotolewa kupitia kuchomwa sindano, hutolewa kila baada ya miezi 3 ili kupanga uzazi.
Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wanaotumia sindano hizi wapo katika hatari zaidi ya kupata saratani ya matiti
• Vipandikizi,
Aina hii ya kupanga uzazi pia huhusisha matumizi ya homoni ambazo kwa nadharia huchochea uwezekano wa kupata saratani ya matiti.
Baadhi ya tafiti zimeonyesha uhusiano uliopo kati ya vipandikizi na hatari ya kupata saratani ya matiti. (American Cancer Society, 2020)
SABABU HATARISHI ZISIZO NA MADHARA WAZI JUU YA SARATANI YA MATITI
Viko vitu vingine ambavyo vinaweza kuwa ni sababu hatarishi, ingawa tafiti bado hazijaweka wazi kuwa ni kweli vitu hivyo vinahusishwa na saratani ya matiti.
1. VYAKULA NA VITAMINI
Wakati kuwa na uzito uliopitiliza au kupindukia na kutofanya mazoezi kunahusishwa na saratani ya matiti, uhusiano kati ya chakula na saratani ya matiti haujawekwa wazi.
Kukosekana kwa uhusiano uliothibitika kati ya chakula na saratani ya matiti katika tafiti zilizopo hivi sasa haimaanishi kuwa hakuna maana katika kula vizuri kiafya (mlo kamili).
Chakula chenye kiasi kidogo cha mafuta, nyama zisizo nyekundu, matunda na mbogamboga zinaweza kuwa na faida nyingi kiafya ikiwemo kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya aina yeyote.
2. KEMIKALI KATIKA MAZINGIRA
Uwepo wa kemikali katika mazingira hasa zenye asili ya estrogen homoni ina mchango wa kipekee. Mafano vitu vinavyopatikana kwenye baadhi ya plastiki, mapambo, dawa za kuulia wadudu. Kwa nadhalia vinaonekana kuwa na matokea kwenye hatari ya kupata saratani ya matiti.
3. MATUMIZI YA TUMBAKU
Tafiti zinaonyesha kuwa uvutaji wa tumbaku uliopindukia kwa muda mrefu unahusishwa na ongezeko la hatari ya kupata saratani ya matiti kwa kiasi.
Tafiti pia zimethibitisha kuwa hatari ni kubwa zaidi kwa baadhi ya makundi ya wanawake mfano, wanawake walioanza kutumia tumbaku kabla ya kupata mtoto wao wa kwanza.
Mwaka 2014 umoja wa madaktari wa upasuaji wa marekani walithibitisha kuwauvutaji sigara unachangia ingawa sio sababu inayoweza kujitosheleza yenyewe kupelekea ongezeko la hatari ya kupata saratani ya matiti.
4. KAZI ZA USIKU (Night Shift Works)
Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wanawake wanaofanya kazi usiku, kama wauguzi katika zamu za usiku, inawezekana kuwa na ongezeko la hatari ya kupata saratani ya matiti.
Jambo hili linazidi kufanyiwa utafiti zaidi. Baadhi ya watafiti wanalihusisha swala hili na mabadiliko ya kiwango cha homoni melatonin. Homoni hii pia bado inafanyiwa utafiti.
NAMNA YA KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA SARATANI YA MATITI
Hakuna njia rasmi ya kuzuia saratani ya matiti, ingawa yapo mambo unayoweza kufanya ili kupunguza hatari ya kupata ugonjwa huu, visababishi vingi viko nje ya uwezo wako kuzuia kama kuzaliwa mwanamke na kuuelekea uzee.
Visababishi vingine pia vinaweza kuwa kama vile mitindo ya maisha kubadilishwa ili kupunguza hatari ya ugonjwa huu.
a) Hakikisha upo katika uzito unaokubalika kiafya:
Uzito uliopitiliza na kuongezeka uzito zaidi hasa baada ya kufikia ukomo wa hedhi unahusishwa na hatari ya kupata saratani ya matiti
b) Fanya mazoezi: Tafiti zinaonyesha mazoezi ya kawaida mpaka yale yanayohusisha nguvu zaidi yanaweza kupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti.
Taasisi ya American Cancer Society inapendekeza kuwa, mtu mzima apate dakika 150 hadi 300 za kufanya mazoezi ya kawaida au dakika 75 hadi 150 za kufanya mazoezi ya nguvu kila wiki. (au yote kwa pamoja) kufanya zaidi ya hapo pia ni salama;
• Mazoezi ya kawaida;ni kitu chochote unachoweza kufanya kikakupelekea kupumua kwa nguvu kama ukitembea kwa kasi.
Yatasababisha kuongezeka kasi ya mapigo ya moyo na kasi ya kupumua. Bado utakuwa na uwezo wa kuongea lakini si kuimba ufanyapo mazoezi haya
• Mazoezi ya nguvu;haya hufanyika kwa kasi na nguvu zaidi, yanasababisha upumue kwa kasi zaidi, mapigo ya moyo yaongezeke na kutokwa na jasho.
c) Acha kabisa au punguza matumizi ya pombe: Pombe huongeza hatari ya kupata saratani ya matiti, hata kiasi kidogo cha pombe kinahusishwa bado na ongezeko la hatari hii. Ni vyema kuacha kabisa kutumia pombe.
d) Kula vizuri kiafya; Baadhi ya tafiti zinashauri kwamba vyakula vilivyo na wingi wa mbogambaoga, matunda, vilivyo na madini ya Calicium, kiwango kidogo cha nyama nyekundu na kuepuka matumizi ya nyama zilizo chakatwa viwandani (za makopo) vinaweza kupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti.
Tafiti nyingine pia zinaonyesha kuwa kupunguza matumizi ya mafuta inaweza kupnguza hatari ya kupoteza maisha mapema kwa sababu ya saratani ya matiti.
e) Amua kupata watoto, nyonyesha watoto: Kama kupata watoto ni swala lililopo ndani ya uwezo wako, amua kufanya hivyo, amua kufanya mapema, pia wanyonyeshe kwa muda mrefu kama inavyo shauriwa.
f) Kujifungua mapema (chini ya umri wa miaka 30), kujifungua watoto wengi na kunyonyesha kwa muda yote yanahusishwa na kupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti.
USIKOSE ANDIKO KUHUSU SARATANI YA MATITI KWA WANAUME.
Karibu kupigia kura andiko hili.
Afisa Muuguzi, BFN.
Ahsante.

Upvote
0