Mitsubishi Outlander ni gari bora na ngumu sana ila hazina wapiga kelele kuzifanya zishike chati midomoni mwa Watanzania

Mitsubishi Outlander ni gari bora na ngumu sana ila hazina wapiga kelele kuzifanya zishike chati midomoni mwa Watanzania

Gari nzuri zisizoongelewa sana na wabongo

Mitsubishi Outlander ni gari bora na ngumu sana, ila hazina wapiga kelele kuzifanya zishike chati midomoni mwa watanzania.

Gari hizi zina vitu vingi sana ambapo gari nyingine kama Toyota huwezi pata hasa ukilinganisha bei yake.

Mitsubishi outlander 2006 - 2015
1. Ni gari inakuja na charging system ya laptop, yaani unaweza kuchomeka switch socket na ukaweka charger yako vizuri... Kwa kifupi gari hili linabadili umeme wa dc kwenda ac.

Kwa watu wanaopenda kutumia laptop wakiwa safari hii gari unaweza kutumia laptop toka Dar mpaka Mwanza, bila kuizima unafanya kazi tu au unaangalia series.

2. Gari hii inakuja na kifridge kidogo kuweka vivywaji uwapo safarini.

3. Gari hii ina option ya 4WD

4. Gari hii inakuambia muda wa kupumzika ukichoka safarini.

5. Gari hii inakuja na mziki mzito yaani subwoofer isiyojaza buti.

6. Gari inakuja na seat 7.

7. Gari hii ina option ya manual na automatic.

8. GARI hii ina gear 6, inaifanya itumie mafuta kidogo.

Hii gari bei yake ipo chini ya kina harrier, kulger na Vanguard. Kitu ambacho hivi vitu vyote vingekuwa kwenye hizo gari bei zake zisingeshikika.
Umedadavua vyema sana mkuu
 
Hahaha acha kuwaogopesha watu, hizi gari ziko vizuri sana. Nitawaletea Changamoto zake ambazo ni common, ila kwa kutumia kama hutaki kwenda garage kila mara kama toyota hizi ni gari ngumu mno. Tofauti kabisa na toyota.

Tujitahidi kuleta taarifa za uhakika kutoka kwa watumiaji. Ili watu wapate uelewa.

Comment moja inaweza muogopesha mtu. Wakati asingeogopa ange save pesa nyingi na akatumia gari nzuri.

Mfano ulikuwa na mpango wa kununua Vanguard ya 35M, ukaacha ukaenda nunua Outlander 19M hapo ume save pesa nyingi mno karibia 16M.

Spare za hizi gari bei yake fatilia ni kama Toyota tu, hizo Harrier, kurger na vanguad.

Tena kuna spare zipo chini zaidi ya hizo gari za Toyota.

Fuel consumption hii gari ipo vizuri.


Mfano hai mwingine

Oil ya Gearbox ya Outlander ambayo ni Mitsubishi CVT J1.
litre 4 unaipata kwa elfu 50,000 bei ya jumla makopo 6.

Au Tsh 120,000/= kwa bei ya mtumiaji.

Ukiweka oil hii utabadili baada ya
30,000km.

Mie nataka watanzania wafunguke wasikariri magari. Mwisho wa siku gari zote, Toyota, Honda, Mazda zitakuwa na bei sawa.

Na mafundi wetu watajifunza na kujua mengi.

All in all
Outlander is the best car ever
Ubarikiwe kwa moyo wako mkuu,usichoke kutuletea taarifa za magari mengine pia maana sio wote tunajua upana wa magari ulivyo zaidi ya kuona kwa watu walionunua
 
Back
Top Bottom