Naomba nichukue fursa hii kuwashukuru wote mliotoa michango yenu ya mawazo na uzoefu kwenye maada hii. Ukweli nawashukuruni sana wote na MUNGU aendelee kuwabariki. Nathamini sana mawazo yote mliyoyatoa na naendelea kuyafanyia kazi kama mliyonishauri na kunielekeza. Hata hivyo, wakati zoezi hilo likiendelea, nimeanza kufikiria RAV 4 na nahisi aina hii ni nzuri (sina ushahidi). Mwenye uzoefu na aina hii anielimishe. Ikiwa aina hii ya magari itaonekana ni bora, nitaanza kutafuta mwenye RAV 4 ya kuuza tutawasiliane kwa
exav@live.com au hapahapa jamvini - kadri atakavyopenda. Nitapenda iwe na hali nzuri, mileage at most 100,000km, engine size at most 2000cc, milango 5. Kwa ujumla isiwe na matatizo.
Natanguliza shukrani kwenu.