john gharish
Member
- Nov 9, 2011
- 13
- 1
Habari za leo wana JF!
Nina nia ya kununua gari dogo la kunisaidia kwenye mizunguko yangu ya maisha. Nafikiria kununua Mitusbishi Pajero iO (GDI), lakini kusema ukweli sifahamu uzuri na ubaya wa aina hii ya magari. Kama kuna anayefahamu/wanaofahamu naomba a/wa-nisaidie, sitaki kukurupuka. Unaweza pia kurecommend aina nyingine unayoimani kwa ubora.
Natanguliza shukrani za dhati sana.
Exav na Tonge , Mimi nilinunua hiyo gari 2007 mpaka leo ni nzuri sijagusa chocho zaidi ya Pancha tu na Matairi yote yaleyale toka Japan na Spare tyre sijaitumia bado ,wengine nasikia wananiambia gari yako vipi haikusumbui nawaambia hawaamini , lakini mimi kwa upeo wangu Japan kuna magari mengi tu aina ya hiyo GDI Jipinde nunua gari isiyozidi Km 40,000-50,000 itakuwa bado bomba lakini ukinunua 80,000- 100,000 baada ya muda itakuwa shida tusinunue magari yaliyotembea sana , na spare zipo nyingi maana gari hizo sasa zipo nyingi ,ila zinaibiwa power window sana , Otherwise ni gari nzuri na Sasa nimemuachia Wife na bado iko bomba saana tuu!
Afadhali umepokea ushauri.Hiyo GDI ni upumbavu mtupu.ukiwa nayo utafikiri kuna mtu amekutupia mkosi.nimesikia wengi wanaisifia hiyo Gdi mitisubishi.nadhani wana malengo yao au wao wenyewewe hawajawhi yamiliki .mimi sijamiliki ila aina hiyo ya magari ila kuna jamaa zangu wa karibu waliyashabikia kwamba yana suspension nzuri wakanunua.wote wakapata taabu inayofanana hasa kwenye injini.wakishia kuwa wanashinda ilala kwa wapemba kutafuta injia used za kubadilisha.nimewahi kuwa na Rv4 old model, ilikuwa kawaida kabisa.sema spare ni nyingi na bei ndogo tu.ila fake ni nyingi ila bei ndogo kwa kuanza naweza sema hiyo itakufaa kujifunzia.Naomba nichukue fursa hii kuwashukuru wote mliotoa michango yenu ya mawazo na uzoefu kwenye maada hii. Ukweli nawashukuruni sana wote na MUNGU aendelee kuwabariki. Nathamini sana mawazo yote mliyoyatoa na naendelea kuyafanyia kazi kama mliyonishauri na kunielekeza. Hata hivyo, wakati zoezi hilo likiendelea, nimeanza kufikiria RAV 4 na nahisi aina hii ni nzuri (sina ushahidi). Mwenye uzoefu na aina hii anielimishe. Ikiwa aina hii ya magari itaonekana ni bora, nitaanza kutafuta mwenye RAV 4 ya kuuza tutawasiliane kwa exav@live.com au hapahapa jamvini - kadri atakavyopenda. Nitapenda iwe na hali nzuri, mileage at most 100,000km, engine size at most 2000cc, milango 5. Kwa ujumla isiwe na matatizo.
Natanguliza shukrani kwenu.
Habari za leo wana JF!
Nina nia ya kununua gari dogo la kunisaidia kwenye mizunguko yangu ya maisha. Nafikiria kununua Mitusbishi Pajero iO (GDI), lakini kusema ukweli sifahamu uzuri na ubaya wa aina hii ya magari. Kama kuna anayefahamu/wanaofahamu naomba a/wa-nisaidie, sitaki kukurupuka. Unaweza pia kurecommend aina nyingine unayoimani kwa ubora.
Natanguliza shukrani za dhati sana.