Mitsubishi Pajero iO inanitesa

Tatizo la hizo gari ni mafuta zinataka unleaded tu!
 
Nashukuru kwa ushauri. Nami nilitaka nijiingize huko kwenye Mitsubishi
 
never drive mitshubishi! Labda Fuso ndio wamejitahidi na mafundi wa bongo wapo, lakini magari madogo sio mazuri kwa soko la Tanzania ila Kenya naona yapo mengi na wanayapenda
 

D4 ni (Direct injection 4 stroke engine) kwa Toyota na GDI (Gasoline Direct Engine) kwa Mitsubishi


Kampuni hizi mbili walikaa pamoja wakakubaliana kutengeneza engine yenye ufanisi mkubwa na kutumia mafuta machache na kufanya vizuri kwa spidi pia kuwa na emmision ndogo(euro 2-3),
Walichokifanya hapa ni kuruhusu injection iwe direct kama engine za diesel kwa ku-inject mafuta mengi kwa interval kwenye combustion chamber
Sasa shida inakuja watumiaji wa kwetu wanatumia mafuta ambayo si salama kwa engine husika ambayo inafanya kujaza mabaki ya carbon,wakati engine ikaperform sasa kwa kua inafanya kwa interval mafuta yanaenda kidogo kidogo inaanza kumiss na kupunguza nguvu na kwakua inatumia umeme,ikifanya hivyo mara kadhaa ina fail,ikifikia hapo lazima uivute,
sasa mafundi wetu hawajui hilo ama jinsi ya kutengeneza ikisumbua
 

Mwizi tu huyo dennis hajui kiti2 GDI yangu ilika kwake wiki mwisho akaniambia wafungue ingine wabadili
Ingine

Tatizo kubwa la GDI ni fuel pump ya mbele new from japan costs $1400 with dhl frieght to dar

Used utapata shauri moyo ni laki 6 hadi 8

Avoid fuel from oilcom other than that it"s quite a good performer
 
hivi kwa nini mechanical engineers hamfungui garage mkatunusuria magari yetu? wengine hatuogopi gharama ili mradi tufanyiwe kazi iliyoenda shule.
 
kumbe ni bei za kawaida tu! check up kwa only 65,000 mtu unaona ni ghali! kwani gari umenunua shingapi?
 
mkuu pole sana mim mwenyewe ni fundi umeme sio mtaalam sana wa hizo GDI ila kiukweli watu wengi huzitupia lawama kibao kwamba sio gari ni mbovu n.k mim nishakutana nazo sana nilitaka niingie kwenye mkumbo wa kuzilaum lakin ikawa tofauti kidogo nimetokea kuzipenda sana kutokana na watu wanavyo sadikishwa kuwa ni mbovu basi ukimtengenezea mtu na ikatengamaa unamtandika bei nzuri sana. Kiukweli gari hizi siyo mbovu bali sisi watumiaji ndio wabovu.kesi kubwa ya GDI huwa kwenye air flow sensor kama air clener itakuwa chafu tu. Basi ujue itakuzingua sana huwa inakuwa na kamiss kaajabu sana some times huwa inagoma kuless kabisaa na huwa ina vibrate. Na kama utampelekea fundi na kuichokoa kwenye sensor ya kwenye acceletar pedar huwa napo inazingua sana. Gari hii inasensor kadhaa sasa wewe unaweka mafuta mabovu yaliyo chakachuliwa vilevile unaacha air clener mpaka linakuwa chafu kabisaa wewe unategemea nin?? Ikiwa binadam tu ukivuta hewa chafu unaugua na pia ukila chakula kibovu unaugua mbona kwa gari mnashangaa??? Si mnakumbuka yale magari ya msafara wa raisi yalivyo sumbua kwa kuzima pindi yalipo wekwa mafuta mabovu??
 
Nimeelimika vya kutosha kupitia uzi huu. Shukrani kwa wote waliochangia
 
wapendwa poleni sana na matatizo ya gari aina ya pajero io,chariot grands,dion,diamante,outlander,Airtreck na zote jamii hizo.Wanazita GDI maana yake Gasoline direct injection.Tatizo kubwa la mafundi huwa hawajui mfumo wa hizo gari ndio maana zinawapatia taabu sana.pia hizo gari hazitaki mafuta nusu nusu lazima zikuletee shida tu hutakwepa.unatakiwa uweke fuel tank yakipungua yawe nusu tank oh utaipenda yako.pia hizo gari zinahitaji umakini sana.ukweli sijisifu kwa hili lakini ninauwezo mkubwa wa kuwasaidia kwa mantengenezo yote ya umeme na mechanical,nimekuwa Technician wa kwanza kutengeneza hizo gari 2005 nikiwa bosch company.pia nilipata course NAIROBI kwa miezi 3.ukweli nazifahamu hizo gari vizuri.Tuko Tabata roundabout kama hatua kumi kutoka roundabout kulia utaona gate jekundu,yakuelekea st mary college.mawasiliano +255755 399613,+255715 399613.karibuni sana.
 
Ukitumia Regular or Supper haijarishi umeinunua kutoka gas station gani mafuta yanatakiwa kuwa sawasawa. unataka kunambia unaposafiri kwenda mikoani itakuwaje ukienda sehemu ambako hakuna gas station uliyoizoea?
 
Weka nashine ya 3S Mi pia ninayo haina Shida kabisaaa
 
Hapo ninavyoona hapo angalia torque converter Kama IPO salama lakini hata clutch zake Kama ziko salama inawezekana converter Haina fluid imekauka au clutch zimeisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…