DOKEZO Mitumba inayopita Bandari ya Dar haina ubora, ni michafu, imechakaa, ni tofauti na ile inayopitia Nairobi, kuna kitu hakipo sawa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ukiwa Kilimanjaro Soko La Memorial
Mtumba Wake Unakuwa Mzuri Sana Tena Wa Kiwango Kizuri Sana Hata Viatu
Nilitaka kuongea jambo kama hili hata mashuka ya mitumba ya memorial ni mazuri sana

Viatu ndo usiseme ni mbingu na ardhi in short karume mitumba yake mibovu alafu bei ni kubwa maradufu
 
Inaweza ikawa fursa au kuna mapapa watakupoteza?
 
Kenya wanaruhusu mitumba grade A tu. Tanzania wanaruhusu mitumba kiwango cha chini pia hivyo wanaoleta mitumba (wholesalers) wanaleta kiwango cha chini hawaleti grade A. Tangu zamani wanaotaka grade A wanaagiza Nairobi.
Sasa hawa bei za grade A ikijumlishwa na kodi wataziweza?
 
Mkome kuagiza vitu china. Wewe uliona wapi bidhaa za kichina za maana.
Wachina na bidhaa zao ni vimeo +++
 
tafuta pa
paspot nenda Nairobi
lala namanga...tafuta namna ya kupata mtu wa exchange....unganishwa na mtu
kanunue mwenyewe
kila siku wanalala watu mamia namanga wanavuka kuanzia saa nane usiku

mambo mengine uwezi yabadili haswaa kama kuna masiasa humo
wewe usisubir kuletewa nenda nairob
 
Hii ni kweli, Kuna Mkenya ananiuziaga Suruaji za Jens ananitumiaga yaani aisee ni gred sana ingawa na bei yake imechangamka sana make inaaziaga 30,000, na kuendelea ila ni quality haswa.
 
Hii ni kweli, Kuna Mkenya ananiuziaga Suruaji za Jens ananitumiaga yaani aisee ni gred sana ingawa na bei yake imechangamka sana make inaaziaga 30,000, na kuendelea ila ni quality haswa.

Niunganishe na mimi mkuu.
Mimi napenda vitu vizuri Quality.

Hadi niliacha kuvaa mtumba kwasababu ya Maronya ya Bongo
 
Mitumba bongo inatoka china ndio mjue china wanamaliza uchumi wenu sababu mmewaacha waweze kufanya wanacho taka
 
Hii itatusaidia kulinda viwanda vyetu vya ndani vya ushonaji na hivyo kulinda ajira za mafundi cherehani wetu!
... LENGO NI KUPELEKA MITUMBA YETU KENYA!
 
Hivi ukiachana na mtumba ni bidhaa zipi nyingine huko ni bei nafuu kuliko huku?
 
Wale waandishi wa habari waliopelekwa Iran na kituo cha utamadani cha Iran Dar es Salaam, kuna siku walionesha video za maduka ya Iran ambapo kila kitu cha Iran ni made in Iran. Zilioneshwa nguo mpya ambazo ni made in Iran. Sasa tuulizane, kwa nini Tanzania tumeshindwa kunufaika na soko la ndani la nguo kwa kuzalisha nguo mpya ikiwa miaka ya nyuma tulikuwa tunatajwa kuzalisha pamba nyingi duniani? Kuna sehemu tutakuwa tunawalaumu mabeberu lakini na sisi akili ni nzito!
 
Agiza kenya mkuu tulipofika hatuhitaji kujieleza unafanya kilichondani ya uwezo, kuepuka kuitwa mchochezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…