Kwa mujibu wa uislamu, mtume au nabii ni muonyaji au mhadhiri aliyetumwa na Mwenyezi mungu kwenda jamii fulani ya watu ila kuwaonya, kuwafundisha na kuwakumbusha juu ya Mungu mmoja aliyewaumba na ambaye wanapaswa kumuabudu. Mitume/nabii walikuwa ni kiigizo chema kwa jamii zao kimatendo na wenye imani thabiti kwa muumba wao.
Kwa mujibu wa mafundisho ya kiislamu, kuna manabii zaidi ya laki moja, ila quran imewataja 25 tu kwa majina. Mitume wote ni manabii, ila sio manabii wote ni mitume.
Mtume/ messenger-- ili uwe mtume,ni lazima uwe umepewa ujumbe( message, kitabu) cha kuwaletea watu. Kwa mujibu wa mafundisho ya kiislamu mitume ni wa 4 tu nao ni:
Musa -- torati
Daudi -- zaburi
Issa--- injili
Muhammad -- furqan. (Quran).
Waliobaki wote wanabaki kuwa manabii (prophets) pekee, kwa maana ya kuwa hawakupewa kitabu ila walitekeleza mafundisho ya vitabu waliopewa mitume wengine.
Kwa mujibu wa uislamu, muhammad alikua mtume na nabii wa mwisho hivyo uislamu hautambui mtume/ nabii yoyote baada yake, na hio inamaanisha kuwa hakuna tena revelations, wahyi utaoshuka duniani baada ya mafundisho yaliyopo.