Mitume wa Yesu wangerudishwa leo duniani wangehubiri huu upuuzi unaohubiriwa na mitume na walimu mamboleo?

Mitume wa Yesu wangerudishwa leo duniani wangehubiri huu upuuzi unaohubiriwa na mitume na walimu mamboleo?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
2,351
Reaction score
2,255
Wewe unaueyumbishwa na wimbi la hawa matapeli wanaojiita mitume, manabii na walimu tafakari vizuri. Mitume wale waliotembea ma Yesu wangepewa kazi warudi duniani wangekuja kuhuburi hii injili uchwara inayohubiriwa leo makanisani na redioni? Wangekuwa wanabwabwaja kwa lugha za mashetani zisizoeleweka? Wangekuwa na ajenda ya pesa kwa asilimia 90 ya mahubiri yao? Wangekuwa wanabwabwaja usiku kucha kupigana na mapepo na laana? Kuna mtu humu aliniambia niache kubeza kwa sababu watu wanakimbilia huko na wanafaidika. Kwake na kwa yeyote mwenye muono huo nasema anayewafaidisha si Mungu wa kweli. Hata shetani ana vitu vingi na humpa kila anayejisalimisha kwake( rejea simulizi ya majaribu ya Yesu alipokuwa akifunga siku arobaini jangwani). Biblia imesema wazi kwamba mtu yeyote akihubiri injili tofauti na ile iliyohubiriwa na mitume ALAANIWE!! Hata angejiita mtume, nabii, mwalimu au hata malaika, ALAANIWE!
 
Screenshot_20250213-132147_Chrome.jpg
 
Hao Mitume wa Zamani na Yesu mwenyewe walitabiri haya, kwa hiyo yakitokea ni vyema, acha kulia lia wewe Mkristo fala, soma Biblia yako vizuri ujue nyakati na Majira Mbwira wewe!
 
Hao Mitume wa Zamani na Yesu mwenyewe walitabiri haya, kwa hiyo yakitokea ni vyema, acha kulia lia wewe Mkristo fala, soma Biblia yako vizuri ujue nyakati na Majira Mbwira wewe!
Umejibu kwa jazba na kwa utovu wa nidhamu matokeo yake hata swali lenyewe hukulijibu! Bora ungekaa kimya.
 
Hawa wanahubiri tofauti kabisa na walichohubiri wale.

Wale walifundisha watu kujitambua na kuwafanya wawe huru.
Hawa wanawafundisha watu wawe mazoba na tegemezi.
 
Back
Top Bottom