Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Kaburi alilozikwa Yesu baada ya kufa msalabani, limehifadhiwa katika nchi ya Israeli hadi leo. Watu wanaoingia ndani ya kaburi hilo, wamekuwa wakishuhudia uwepo wa Mungu na miujiza mingi. Katika kaburi hilo ndipo ulipofanyika muujiza mkubwa wa kufufuka kwa Yesu. Baada ya hapo miujiza mingine ya kushangaza imeendelea kufanyika katika kaburi hilo mpaka leo!
Mtu mmoja kutoka Romania, macho yake yalikuwa hayaoni vizuri mpaka avae miwani. Alipoingia katika kaburi hilo, kwa ghafla macho yake yalipona, akaweza kuona vizuri mpaka alama ndogo ya msalaba iliyochorwa kwenye ukuta wa kaburi hilo. Akaanza kupaza sauti: "Ninaona, ninaona!"
Muujiza mwingine ulifanyika kwa kijana Jean Carlo Rodriguez kutoka Ecuador, aliyekuwa anaumwa ugonjwa wa hatari sana(hydrophilis). Ugonjwa huu ulisababisha majimaji kujaa kwenye ubongo wa kijana huyo na kuifanya sehemu kubwa ya mwili wake ipooze(paralysed). Siku moja, familia ya Jean ilitembelea Israeli. Wazazi wake walimuingiza Jean kwenye kaburi hilo, wakaanza kumuomba Mungu. Ghafla Jean alianza kulia, akaweza kusimama mwenyewe.
Dada yake Jean, alikuwa anamlaumu Mungu kama Atheists wanavyofanya kwa kusema: "kwanini Mungu aliruhusu ugonjwa huo umpate kaka yake?" Baada ya muujiza huo wa uponyaji, dada yake huyo alibadilika, akamwamini Yesu, na sasa anamtumikia Mungu.
Shuhuda ni nyingi. Endelea kusoma...