Swali linakuja mafuta yapi,hayo mafuta yanatokana na mini,mafuta wanayotumia akina mwamposya mnajua yanatoka wapi,mnajua yamewekewa nn,bakini ni ujinga wenu,mmesoma ila zero brain,wake zenu wamewazidi akili
Mafuta ni mamoja tuu
Mafuta ya mzeituni. Tena yale yasiyochakachuliwa
WAAMUZI 9:8-15
8 Siku moja miti ilitoka ili kuutia mmoja mafuta uwe mfalme juu yao; ikauambia mti mzeituni, Tawala wewe juu yetu.
9 Lakini huo mzeituni ukaiambia, Je! Niache mafuta yangu, ambayo kwangu mimi watu wamheshimu Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya miti?
10 Kisha miti ikauambia mtini, Njoo wewe, utawale juu yetu.
11 Lakini huo mtini ukaiambia, Je! Niuache utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende nikayonge-yonge juu ya miti?
12 Kisha miti ikauambia mzabibu, Njoo wewe, utawale juu yetu.
13 Huo mzabibu nao ukaiambia, Je! Niiache divai yangu, ambayo humfurahisha Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya miti?
14 Ndipo hiyo miti yote ikauambia mti wa miiba, Njoo wewe, utawale juu yetu.
15 Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Kwamba ninyi mwanitia mafuta niwe mfalme juu yenu kwelikweli, basi njoni mtumaini kivuli changu; na kwamba sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni.