Kabla ya kututoka Mwl alisema akifa tutamkumbuka. Wakati hule sikuweza kuelewa kwa sababu nilijua watanzania tupo wengi na tusingekaa na kumfikilia mwalimu. Lakini tangu serikali hii ya nne ilipoingia na ubabe fulani uliyoonyeshwa na serikali ya tatu ndipo nikatambua kuwa mwalimu alitambua fika kuwa aliacha watu walafi wenye kupenda sifa waliokuwa na tamaa ya kuingia ikulu pasipo kuwa na nia dhabiti ya kuendeleza taifa ili. Mwalimu aligundua ni jinsi gani tamaa ilitawala kundi kubwa la viongozi. Mwl alitambua umbumbumbu wa watanzania na ile imani ya undugu kuwa ingewapelekea kumchagua mtu asiyekuwa na sifa, mtovu wa maadili asiyeijua nchi na mwenyeupeo mdogo kuchukua dhamana ya kuendeleza Taifa hili.
Mwalimu hata wakati wa uhai wake alitamka kuwa watanzania tulipaswa kuwaogopa kama ukoma wale waliokuwa na tamaa ya kuingia ikulu kwa mapesa na mbinu nyingine chafu. Pia baba wa Taifa alisema IKULU si maala pa kukimbilia. Ikulu si maala pa mchezo. Ni maala pagumu sana. Hupati usingizi ukifikiria shida za watu wako.
Pamoja na yote aliyonena Mwl. Watanzania tumetoa nafasi kwa mtu ambaye alionyesha tamaa kubwa ktk umri mdogo wa kuichukua nchi. Na hata aliposhindwa 1995, mwaka 2005 mtu huyu alikuja kwa namna ya pekee akionyesha tamaa kubwa ya kuingia ikulu huku akiwa na kundi kubwa la marafiki wenye pesa na pia kuzungukwa na watendaji wabovu. Mtu huyu ujiosha machoni mwa watanzania na kujivua pale lawama zinapotolewa na kusukuma mzigo kwa watendaji wake. Ni ndani ya miaka 2, mh. huyo anaitangazia dunia kuwa hajui ni kwa nini nchi ambayo yeye anaiongoza ni maskini licha ya kuwa na mali lukuki. Nilifikiri ili ni swali ambalo kabla ya kuitaji kura zetu alikuwa amelipatia jibu na tayari alikwisha andaa namna ya kutatua. Kwa wakati huu ambapo mweshimiwa hajui je watanzania tutarajie nini wakati tatizo letu ni umaskini?
Ni katika bunge la budget la mwaka huu ilidhihirika kuwa serikali haikuwa imejenga barabara mpya hata km 1. Na ni miezi 5 kwa sasa tangu budget ya 2007/2008 ipite huku serikali ya nne ikisifiwa kwa kuweka kipaumbele kwenye barabara kwa kutenga mabilioni ya fedha lakini mpaka sasa tunaongea swala la kupata makandarasi, je kazi itaanza lini wakati inatambulika fika kuwa mwaka jana miundo mbinu yetu iliaribiwa na mvua kubwa? Mikakati ya budget kwa 2008/2009 imeanza huku tukishindwa kusimamia utekelezaji wa budget iliyopo. Swala la kujiuliza je, fungu lilitengwa kwa ualisia wake au ilikuwa kiini macho ili kuondoa aibu kwa serikali baada ya kubanwa na mh Zitto? Tuwe macho maana longolongo na sifa zimezidi. Tunaweza hata kupewa budget hewa ilimradi tu wajisifu.
Ni kweli miaka 46 tangu tujipatie uhuru. Leo hii kuna baadhi ya maeneo hapa Dar unakuta alama ya lami mitahani kuonyesha kuwa Mwl aliweka kipaumbele kuifanya Dar na maeneo mengine kuweza kufikika. Ilikuwa ni matarajio yetu kuona viongozi waliomfuata kutia msukumo zaidi. Lakini ukiachilia mbali mipangilio dhabiti iliyowekwa na Mzee wetu Ruksa na jitiada zake za kuomba fedha nje ambayo ndiyo haswa ilikuja kusimamiwa na Ben hakuna tena mikakati hiyo na usimamizi ulimefikia ukingoni. Upcountry kumeachwa tupu. Tambua Ben kwa kutambua kuondoka kwake ikulu basi hakuacha mipangilio bora na hata fedha akazipitishia mlango wa nyuma ili kujiandaa kuwa chinga mtaani na si rais mstaafu.
Nafikiri imefikia hatua serikali kuu kupunguziwa kabisa uwezo wa kumiliki kodi za nchi hii na badala yake kuwepo na uwiano wa mgawanyo moja kwa moja from source wa kodi, mikopo na misaada ili halmashauri ziwezeshwe kusimamia miundo mbinu wakiwa na fungu kuliko hivi sasa. Lakini pia lazima jina la mh lijumuishwe na matokeo mabovu ya serikali yake badala ya kumsifia na kufikiri mbovu ni Edu, kara na wengine. Yeye ni kichwa, alivua nguo mwenyewe kwani hakujua maji yalikuwa ni ya baridi matokeo yake anagoma kuyaoga? Thanks JF
TANZANIA INA NEHEMA TANGU ENZI INAITAJI WASIMAMIZI WAWAJIBIKAJI NA WENYE KUIONA MAANA IMEWEKWA NA MWENYEZI NA SI WALE WANAOTAKA KUITAFUTA KWA NJIA ZAO ZA KIBINADAMU.
Jamani kuna picha nimeiweka hapa chini nisaidieni kuibandika (mimi sijui kubandika picha JF)
Ukiangalia hiyo barabara na hayo magari kweli unaweza kuikana hata nchi yako. Hivi kweli maisha bora hata barabara za mikoani tuu tunashindwa kuweka hata changarawe? Tunazunguka kutafuta wawekezaji hivi ni mwekezaji gani atawekeza sehemu kama hizi za Kigoma japo kuna opportunities nyingi?
Hii bara bara inanikumbusha siku moja nilikuwa naenda Lindi na Mtwara tukalala Nangurukuru siku 3.