Miundo mbinu ya reli ikiwemo stesheni za reli, nyaya za umeme , hata lifti ktk majengo ya stesheni za reli nchini Afrika ya Kusini imekwapuliwa na vibaka waliowasili wakiwa na malori hivyo kufanya uharibifu mkubwa kwa mtandao wa reli wa Afrika ya Kusini ambao umekuwa ukitiliwa mfano na kutajwa kuwa ni wa kuigwa kwa kuwa na huduma safi kwa abiria wa treni.
Serikali ya Afrika ya Kusini imejaribu kuwekeza miradi ya bilioni 6 za dolari za Kimarekani kufufua uchumi wake kipindi cha lockdown cha ugonjwa wa Covid-19 ktk miradi kama reli, majenzi ya nyumba 50,000 n.k itakayoleta ajira zaidi ya 100,000 lakini uharibifu unaofanyika kwa miundo mbinu iliyomalizika na iliyokuwa inatumika inaleta sikitiko na maswali mengi juu ya tabia na hulka za wakaazi Barani Afrika ...
Source: BBC News Swahili